Wanafunzi wa shule ya sekondari Uhuru manispaa ya Shinyanga ambao wameunda klabu ya maadili shuleni hapo.
Na Kareny
Masasy, Shinyanga
SHULE za msingi, sekondari na vyuo mkoani Shinyanga zimetakiwa kuanzisha vilabu vya maadili kwa wanafunzi ili kuweza kuwajenga kuwa wazalendo,wenye uwajibikaji na uaminifu hata kwenye jamii na pindi watakapo kuwa na majukumu ya kikazi na familia.
Hayo yamesemwa leo tarehe 23,Oktoba ,2023 na Gerald Mwaitebela ambaye ni katibu msaidizi ofisi ya Rais sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kanda ya Magharibi inayojumuisha mikoa ya Tabora,Kigoma,Shinyanga na Simiyu.
Mwaitebela amesema shule zote zinatakiwa kuwa na vilabu vya maadili na walezi wa shule watatakiwa kusimamia muongozo utakaotolewa na kuhakikisha kutoa taarifa za mienendo za klabu hizo na wanafunzi waelezwe kwa kina nia na madhumuni ya kuwa wanachama wa klabu hizo.
“Asilimia 80 ya mafanikio kwa wafanyakazi wote na jamii ni kufuata maadili na vijana wakiwa na maadili watasaidia kulinyanyua taifa hili na leo tumeamua kuwaita walimu kuwapa muongozo huu watautumia shuleni”amesema Mwaibetela.
Afisa maadili kanda ya Magharibi Tabora Onesmo Msalangi akisoma muongozo wa namna ya vilabu vya wanafunzi shuleni viwe mojawapo ni kikundi kitakachokuwa na wanafunzi wasiopungua 20 na mtu akitaka kujitoa atajitoa kwa hiari na watakuwa wakitoa ujumbe wenye maadili kupitia mashairi,nyimbo na Maigizo.
“Siku hizi watoto wanajifunza kupitia mitandao ya kijamii na kuiga kwa yale yanayofanywa na watu wazima au kwenye televisheni hivyo walimu na wazazi washirikiane katika malezi na maadili ili kuleta kizazi yenye maadili na uzalendo hapo badaye”amesema Msalangi.
Kaimu ofisa elimu mkoa wa Shinyanga Bakari Kasinyo akielezea namna ya kudumisha uzalendo mojawapo ni kuipenda na kuiheshimu jamii,kuipenda nchi,kuwa mwadilifu,kuwa wastahilimi,kudumisha Amani,kudumisha demokrasia,kutii sheria pamoja na kutunza mazingira.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo ya walimu walezi wa klabu za maadili mkoani Shinyanga ambaye ni katibu tawala msaidizi Ibrahimu Makana alisema lengo la klabu hizi ni kuwajengea uwezo wanafunzi wawe na misingi bora ya maadili tangu shuleni.
“Sifa za walimu wa malezi ni pamoja na kuwa mwadilifu,mwaminifu,muwazi, mzalendo,mwajibikaji,anayejali anayethamini utu na mwenye mafanikio katika kazi zake na anayekubalika kimaadili na wanafunzi”amesema Makana.
Baadhi ya
walimu walezi wa vilabu vya maadili waliohudhuria kupata mafunzo hayo ambapo Mwalimu wa malezi shule ya msingi Town
Anaeli Yeunge amesema changamoto iliyopo wazazi kutokuwa na
ushirikiano katika malezi.
Kaimu ofisa elimu mkoa wa Shinyanga Bakari Kasinyo akisisitiza maadili kwa wanafunzi na walimu shuleni.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Uhuru
Gerald Mwaitebela ambaye ni katibu msaidizi ofisi ya Rais
sekretarieti ya maadili ya viongozi
wa umma kanda ya Magharibi.
Akiwakilisha ofisi ya mkuu wa mkoa ambaye anatoka ofisi ya katibu tawala Ibrahimu Makana
Wanafunzi wakiimba shairi lao kusisitiza maadili ya wanafunzi shuleni na kwenye jamii.