TCRA YAHAMASISHA UANZISHWAJI WA KLABU ZA KIDIJITI KATIKA SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI NA VYUONI

Meneja wa TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Mahafali ya Kwanza shule ya Sekondari Kabela Gold 


Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo ameongoza Mahafali ya Kwanza shule ya Sekondari Kabela Gold iliyopo katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga ambapo jumla ya wanafunzi 69 kati yao wasichana 33 na wavulana 36 wanahitimu elimu ya kidato cha nne mwaka 2023.

Akizungumza wakati wa Mahafali hayo leo Alhamisi Oktoba 19,2023, Mhandisi Mihayo amewatahadhalisha wanafunzi kutumia vizuri mitandao ya kijamii kwa ajili ya maendeleo wakumbuke kuwa kila wanachochapisha ‘post’ kinabaki mtandaoni huku akiwataka wazazi kuwa makini na watoto wao wanapowapatia simu janja au Kompyuta ili kuhakikisha kwamba wanazitumia vizuri katika kujifunza masuala ya TEHAMA.

Aidha amewashauri wazazi kupeleka watoto shule na kufuatilia mienendo yao pia wawaruhusu wafanye michezo na wanafunzi wasome kwa bidii.

Katika hatua nyingine Mhandisi Mihayo amehamasisha shule za msingi, Sekondari na Vyuo kuanzisha Klabu za Kidijiti ambalo ni jukwaa linalowakusanya wanafunzi wanaopenda masomo ya TEHAMA ili kuongeza weledi na ubunifu wa kidijiti kwa majadiliano na kufanya shughuli mbalimbali kwa kutumia Dijitali na vifaa vya kidijiti.
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo

"Nchini, klabu za kitaaluma zimekuwapo katika shule za msingi na sekondari kwa miaka mingi (tangu mwanzoni mwa mwaka 1980) na klabu maarufu zaidi ni za Hisabati, Sayansi na Kiingereza. Klabu hizo zilianzishwa kwa lengo la kuhamasisha na kuongeza ari kwa wanafunzi kuyapenda masomo hayo. Katika muktadha huu ambao masoko na wanajamii wanahamia katika mtandao ni muhimu kuendana na kasi ya mabadiliko haya na kujenga mwelekeo unaolingana na hali halisi.

Katika nyakati hizi za kidijiti ambazo zinahusishwa zaidi na vijana,ni jukumu letu kuanza kuwapa uelewa,matumizi na mazoea ya kutumia teknolojia tangu wakiwa katika shule za awali na kuendelea",amesema Meneja huyo wa TCRA Kanda ya Ziwa.


Amesema ili kupata jamii yenye uelewa na utayari wa mabadiliko ya kidijiti na ushindani katika uchumi wa dunia ya kidijiti, inahitaji kujenga msingi utakaowahusisha vijana ambapo kizazi cha kidijiti kinaanza na vijana lakini pia inahitaji usimamizi na uratibu mzuri.

“Serikali kupitia TCRA sasa hivi inasisitiza zaidi matumizi ya TEHAMA , kwa maana ya kwamba kila mtoto ahakikishe anajibidisha kujua TEHAMA. Hizi simu na Kompyuta pamoja na mabaya yake haziepukiki. Vijana wanahitaji kuwa na mawazo ya ubunifu na wenye maono ili waweze kuanzisha miradi ya maendeleo yenye kufanya maisha kuwa bora Duniani. Kuwapa motisha waweze kufikia mabadiliko kupitia uvumbuzi ni suala lisilo epukika”,amesema Mhandisi Mihayo.


“Kwa kushiriki katika klabu hizi za Kidijiti , wanafunzi watapata maandalizi ya msingi yanayowawezesha kujifunza kwa karne ya 21 teknolojia inayoleta Mapinduzi ya 4 ya Viwanda duniani. Klabu za Kidijiti zitawaongezea ari wanafunzi katika masomo ya sayansi,teknolojia,uhandisi na hisabati, hivyo kukuza fikra za kitaalamu, ubunifu, na uvumbuzi”,ameeleza.

Amefafanua kuwa Klabu za Kidijiti zitawahamasisha  wanafunzi kusoma masomo ya sayansi, teknolojia,uhandisi na hisabati na kuendeleza ujuzi wao katika sayansi na teknolojia ili kukuza udadisi na ujifunzaji wa vitendo, hivyo,zitasaidia kuendeleza ujuzi na maarifa ili kukabiliana na changamoto zilizopo na kuchangia katika maendeleo ya kisayansi, teknolojia na jamii kwa ujumla.


Amesema kwa watakaokuwa tayari kuanzisha Klabu za Kidijiti wawasiliane na TCRA ili iwapelekee watalaamu kwa ajili ya taratibu za uanzishaji wa Klabu hizo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kabela Gold, Daud Yacob Bucheyeki 

Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Sekondari Kabela Gold, Daud Yacob Bucheyeki amesema shule hiyo imeanzishwa mwaka 2020 kwa nguvu za wananchi na wajasiriamali wachimbaji wadogo wadogo wa mgodi wa dhahabu wa Mwime ambapo ilianza na wanafunzi 96 na sasa ina wanafunzi 654 kati yao wavulana ni 292 na wasichana 362.


Amesema licha ya mafanikio makubwa kitaaluma, amezitaja changamoto zilizopo katika shule hiyo ni pamoja na ukosefu wa maabara ya Kompyuta, upungufu wa walimu wa Sayansi, ukosefu wa maktaba ya vitabu, upungufu wa maabara ya Bailojia, Jengo la utawala hali inayosababisha walimu watumie madarasa kama ofisi


Akisoma risala ya wahitimu, Johari Said amesema wanamshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi mbalimbali anazofanya kuboresha sekta elimu mfano kuwaongezea madarasa na vitabu katika shule hiyo.

ANGALIA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI
Wahitimu wakiingia ukumbini leo Alhamisi Oktoba 19,2023 wakati wa Mahafali ya Kwanza shule ya Sekondari Kabela Gold iliyopo katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga ambapo jumla ya wanafunzi 69 kati yao wasichana 33 na wavulana 36 wanahitimu elimu ya kidato cha nne mwaka 2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wahitimu wakiingia ukumbini leo Alhamisi Oktoba 19,2023 wakati wa Mahafali ya Kwanza shule ya Sekondari Kabela Gold iliyopo katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Mahafali ya Kwanza shule ya Sekondari Kabela Gold iliyopo katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kabela Gold, Daud Yacob Bucheyeki akizungumza wakati wa Mahafali ya Kwanza shule ya Sekondari Kabela Gold iliyopo katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Kabela Gold, Joseph Andrea Nalimi akizungumza wakati wa Mahafali ya Kwanza shule ya Sekondari Kabela Gold iliyopo katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilindi kata ya Zongomela ilipo shule ya Sekondari Kabela Gold akizungumza wakati wa Mahafali ya Kwanza shule ya Sekondari Kabela Gold iliyopo katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga
Mdau wa elimu, Meneja wa Chuo cha Madini Kahama Mhandisi Happines Mathias akizungumza wakati wa Mahafali ya Kwanza shule ya Sekondari Kabela Gold 
Mhitimu Johari Said akisoma risala
Keki maalumu wakati wa Mahafali ya Kwanza shule ya Sekondari Kabela Gold iliyopo katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akikata keki wakati wa Mahafali ya Kwanza shule ya Sekondari Kabela Gold iliyopo katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga
Burudani ikiendelea wakati wa Mahafali ya Kwanza shule ya Sekondari Kabela Gold 
Vijana wa Skauti wakitoa burudani wakati wa Mahafali ya Kwanza shule ya Sekondari Kabela Gold 
Burudani ikiendelea wakati wa Mahafali ya Kwanza shule ya Sekondari Kabela Gold 
Burudani ikiendelea wakati wa Mahafali ya Kwanza shule ya Sekondari Kabela Gold 
Burudani ikiendelea wakati wa Mahafali ya Kwanza shule ya Sekondari Kabela Gold 
Burudani ikiendelea wakati wa Mahafali ya Kwanza shule ya Sekondari Kabela Gold 
Vijana wa Skauti wakionesha ukakamavu wa kuvunja tofali wakati wa Mahafali ya Kwanza shule ya Sekondari Kabela Gold
Wahitimu wakicheza muziki na mwalimu wao wakati wa Mahafali ya Kwanza shule ya Sekondari Kabela Gold
Zoezi la kugawa vyeti likiendelea wakati wa Mahafali ya Kwanza shule ya Sekondari Kabela Gold
Zoezi la kugawa vyeti likiendelea wakati wa Mahafali ya Kwanza shule ya Sekondari Kabela Gold
Zoezi la kugawa vyeti likiendelea wakati wa Mahafali ya Kwanza shule ya Sekondari Kabela Gold
Zoezi la kugawa vyeti likiendelea wakati wa Mahafali ya Kwanza shule ya Sekondari Kabela Gold
Zoezi la kugawa vyeti likiendelea wakati wa Mahafali ya Kwanza shule ya Sekondari Kabela Gold
Zoezi la kugawa vyeti likiendelea wakati wa Mahafali ya Kwanza shule ya Sekondari Kabela Gold
Zoezi la kugawa vyeti likiendelea wakati wa Mahafali ya Kwanza shule ya Sekondari Kabela Gold
Zoezi la kugawa vyeti likiendelea wakati wa Mahafali ya Kwanza shule ya Sekondari Kabela Gold
Picha ya kumbukumbu meza kuu na wahitimu 
Wahitimu wakifuatilia matukio wakati Mahafali ya Kwanza shule ya Sekondari Kabela Gold
Wahitimu wakifuatilia matukio wakati Mahafali ya Kwanza shule ya Sekondari Kabela Gold
Wahitimu wakifuatilia matukio wakati Mahafali ya Kwanza shule ya Sekondari Kabela Gold
Wazazi na wageni waalikwa wakiwa kwenye mahafali
Wazazi na wageni waalikwa wakiwa kwenye mahafali
Wazazi na wageni waalikwa wakiwa kwenye mahafali
Wazazi na wageni waalikwa wakiwa kwenye mahafali

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464