TCRA YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI MWANZA

Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akitoa mada kuhusu Kazi na Majukumu ya TCRA wakati wa mafunzo kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza leo Ijumaa Oktoba 20,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa mafunzo kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza leo Ijumaa Oktoba 20,2023.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa imetoa mafunzo kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza kuhusu Kazi na Majukumu ya TCRA na Sheria na Kanuni zinazosimamia Sekta ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika leo Ijumaa Oktoba 20,2023 katika ukumbi wa TMDA Jijini Mwanza, Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo amewataka Waandishi wa habari na vyombo vya habari kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazotakiwa ili kuepuka migongano isiyokuwa ya lazima.

“Naomba tutii sheria bila kusukumana, fuateni sheria kusajili vyombo vya habari mtandaoni. Wengine hawajajisajili ukimuuliza kwanini hajasajili mtandao wake anasema alikuwa anajaribu jaribu kwanza aone kama inalipa, fuateni sheria tusije kulaumiana”,amesema Mhandisi Mihayo.

Meneja huyo wa TCRA Kanda ya Ziwa pia amevikumbusha vyombo vya habari kutumia lugha sahihi kwenye vipindi vyao na habari wanazochapisha na kuhakikisha wanaandika habari kwa usawa.

“Utengenezaji wa maudhui kwenye vyombo vya habari hivi sasa ni changamoto makosa ni mengi, maudhui mengi mnayotengeneza hayana afya kwa jamii, mnaigana sana. Hizi stori za kwenye mitandao ya kijamii nyingi haziko balanced (haziandikwi kwa usawa) , zipo upande mmoja, hakuna usawa.

Lugha zinazotumika siyo sahihi, Kiswahili hakieleweki, acheni kuchanganya Kiswahili na Kiingereza. Epukeni kushabikia mambo ambayo hayana tija kwenye vipindi vyenu”,ameongeza Mhandisi Mihayo.

Aidha ameshauri wananchi wanaofanya malipo yoyote ya serikali wahakikishe wanafanya kwa Control number ili kuepuka utapeli na ujanja ujanja unaofanywa na baadhi ya watu wasio waaminifu.

“Ajenda ya kulinda watoto inatakiwa ichukuliwe kwa uzito mkubwa. Lazima tuwalinde watoto dhidi ya matumizi ya mitandao ya kijamii, tuepuke kuchapisha picha za watoto mitandaoni”,amesema.

Hata hivyo amesisitiza kuwa mionzi inayotoka kwenye minara ya simu haina madhara kwa binadamu kwani TCRA huwa inafanya upimaji wa mionzi kila robo ya mwaka kwenye maeneo mbalimbali nchini.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa mafunzo kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza leo Ijumaa Oktoba 20,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akitoa mada kuhusu Kazi na Majukumu ya TCRA wakati wa mafunzo kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza leo Ijumaa Oktoba 20,2023.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza, Edwin Soko akitoa mada kuhusu Sheria na Kanuni zinazosimamia Sekta ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta

Katibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza, Blandina Aristides akizungumza wakati wa mafunzo kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza leo Ijumaa Oktoba 20,2023.

Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza wakifuatilia mafunzo

Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza wakifuatilia mafunzo kwa vitendo kupitia simu za mkononi

Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza wakifuatilia mafunzo kwa vitendo kupitia simu za mkononi.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464