Na Mwandishi Wetu, Arusha
Wadau wametakiwa kuondoa hofu na mabadiliko ya Sayansi na kiteknolojia katika utendaji wa shughuli za kila siku ili kupunguza gharama za uendeshaji na uzalishaji.
Hayo yameibuka kwenye mjadala ulioendeshwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika, uliowakutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta binafssi, serikalini, wanazuoni na asasi za kiraia, katika wiki ya AZAKI #WIKIYAAZAKI2023 inayoendelea Jijini Arusha, ambapo pamoja na mengine, ujumbe mkuu ulikuwa ni ubunifu na Teknolojia kama chachu ya usawa wa Kijinsia.
Akizungumza wakati wa jopo, Kaimu Mkuu wa Idara ya Ushawishi na Utetezi, TGNP Florah Ndaba amesema kwamba, Jamii haipaswi kuogopa wala kuwa na hofu juu ya ukoaji wa teknolojia badly ni kuangalia, teknolojia isitumike bibaya kuongeza Ukatili na udhalilishaji wa Kijinsia au kuongeza tofauti za kiuchumi kati ya wanawake na wanaume.
“Teknolojia, inapunguza gharama za utendeshaji na uzalishaji, ndio maana TGNP tuliingia makubaliano ya DIT kusaidiana katika kuendeleza kuhakikisha jitihada za ubinifu wa kisayansi zinazofanywa na DIT zinazingatia usawa wa Kijinsia lakini pia wasichana wanaochagua fani za sayansi na tknolojia wanapata nafasi na kulelewa vipaji vyao hadi waingie kwenye soko la ajira” ,amesema Flora.
Naye Mwanajopo mtaalamu na Mchambuzi wa Masuala ya Kijinsia Deogratius Temba, alisema kwamba, kukosekana kw a usawa wa Kijinsia katika teknolojia kunaikosesha nchi fedha nyingi ambazo zingepatikana kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji.
“Utafiti uliofanywa na UN Women kwa nchi 51 mwaka 2022, umeeleza kwamba, nchi za uchumi wa chini na Kati ambazo hakuna usawa wa Kijinsia katika Teknolojia zinapoteza Dola za Kimarekani Trilion 1 kila mwaka, na ifikapo mwaka 2025, zitapoteza Zaidi ya dola za kimarekani Trilion 1.5. Ukiangalia hii ni kwamba, Usawa wa Kijinsia kwenye eneo la Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati hauepukiki”, alisema Temba.
Aidha, akizungumza Mkufunzi kutoka Taasisi ya Tekonolojia Dar es salaam, (DIT), Nizentha Kimario, alisema kwamba DIT imekuwa na mtazamo wa Kijinsia, mahusiano yake na TGNP yamesaidia pia kujenga uelewa wa masuala ya Kijinsia na kubadili mitazamo hasi juu ya uwezo wa wasichana katika fani za sayansi na Teknolojia, lakini pia kwamba wanafunzi wanaona umuhimu wa kwenda kwenye jamii kuangalia changamoto na mahitaji yao kabla ya kuanza kufanya ubunifu.
“Utaona kwamba, mashine nyingi za kibunifu tumebuni kutokana na mahitaji ya jamii. Wanafunzi wetu baada ya kuona kuna changamoto ya gharama kubwa ya kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo ndio walikuja na mashine hii hapa, lakini pia kuna gharama kubwa kwenye kutunza na kuwawekea dawa watoto wenye changamoto ya kupumua hasa arthima, ndio maana vijana wetu tena wasichana wamebuni hii mashine”, alisema Kimario.
Sambamba na mijadala huo, wanafunzi kutika Chuo cha DIT wameonesha mashine mbalimbali ambazo zimebuniwa na wanafunzi, na Pikipiki ya magurudumu matatu (Bajaji) yenye uwezo wa kubeba abiria saba (7) na Dereva ambayo inatumia nishati ya Betri la kuchaji.
Wiki ya AZAKI 2023 inayoratibiwa na Mfuko wa Asasi za Kiraia (FCS), imeanza Oktiba 23 hadi 27 2023 jijini Arusha ikiwa imewahusisha wakurugenzi, wafanyakazi na wadau mbalimbali wa asasi za kiraia zaidi ya 500, wadau wa maendeleo, wataalamu kutoka serikalini na wanajamii ambao wananufaika na rasilimali na kazi za AZAKI
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464