Mratibu wa vituo vya taarifa na maarifa mkoa wa Shinyanga
Na Kareny Masasy,
FREDINA Makeleja ni mratibu wa vituo vya taarifa na maarifa mkoa wa Shinyanga anaeleza mafanikio yaliyopatikana katika mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP).
Makeleja anasema mtandao huo uliingia mkoa wa Shinyanga mwaka 2012 kwa kuanzia na halmashauri ya Kishapu na kujikita kwenye kata moja ya Songwa na baadaye kata zingine .
Halmashauri ya Kishapu imeweza kutujengea uwezo kwa vituo vya taarifa na maarifa kwa kutupa mbinu ya ulaghibishi na kuibua changamoto mbalimbali zinazo tukabili.
Makeleja anasema kwa kusherekea miaka 30 ya uwepo wa TGNP ni jambo ambalo linakumbusha wananchi kwenye vituo vyao wapi wametoka na wamefika wapi kwa kupiga hatua.
Makeleja anasema TGNP ilianza halmashauri ya Kishapu mwaka 2012 kwa kuanzia kata ya Songwa na baadaye kuhamia kata nane ambazo ni Mondo,Bunambiu,Kishapu Ukenyenge Mganzo Mwadui Lohumbo Mwaweja na Kiloleli na sasa vituo vya taarifa na maarifa vipo kwenye kata tisa.
“TGNP hawakuishia hapo wameweza tena kutoa elimu ya ulaghibishi kwa uibuaji wa changamoto na kuishawishi serikali katika kata mbili za halmashauri ya Msalala ambazo ni kata ya Shilela na Lunguya”anasema Makeleja.
Makeleja anasema baada ya kufundishwa ulaghibishi wa kuibua changamoto mbalimbali ambapo kila kata iliona vikwazo na kuishawishi serikali na eneo ambalo kulikuwa na changamoto walikuwa wakizipa kipaumbele.
Makeleja anasema sehemu ambayo kulikuwa hakuna miundombinu mizuri sasa ipo upungufu wa matundu ya vyoo shuleni vituo vilikuwa vikiibua serikali inafuatilia na inatekeleza.
“Shule ya sekondari Ukenyenge kulikuwa na matundu ya vyoo mawili lakini sasa yapo matundu 12 sita kwa wavulana na sita mengine kwa wasichana.”Makeleja.
Makeleja anasema sasa wanacho jivunia kwa TGNP iliwapatia jamii muwamko wa kujua changamoto zao na namna ya kuzitatua kwa kupitia ushawishi wala sio kugombana na serikali.
“Shule nyingi kwenye kata walizo vituo vya taarifa na maarifa vina matundu ya vyoo 18 hadi 24 mfano kijiji cha Bulimba shule kulikuwa na changamoto ya uhaba wa matundu ya vyoo na miundombinu yake mibovu walijitoa wananchi kwa pamoja kwa kushirikiana na serikali na kupata matundu ya vyoo bora”.
Makeleja anasema TGNP iliwafundisha lazima wawe na jicho la kijinsia wakati wa kuundwa kwa bajeti kuanzia ngazi za vitongoji na vijiji ambapo waliona kuna changamoto nyingi zinahitaji kutengewe bajeti ili kusaidia wanawake mfano uwepo wa maji,taulo za kike na nyumba za kujistiri watoto wa kike.
Makeleja anasema upande wa kutolea huduma za afya mfano Zahanati ya Negezi ilikuwa na changamoto ya ukosefu wa maji na umeme lakini sasa changamoto hizo hazipo tena wanakituo cha taarifa na maarifa wanaona mafanikio.
“Miaka 30 ya TGNP imeleta mabadiliko makubwa kwa wanawake wa pembezoni ambapo wanawake walikuwa hawajitokezi kujieleza kweye hadhara wala kugombea nafasi za maamuzi na kuchangia hoja sasa wanaweza ”.
Makeleja anasema elimu ya ufeminia iliwagusa wanawake na wengi kujitokeza kugombea na nafasi za kwenye kamati mbalimbali za vijiji na vitongoji na kata na wapo waliopata nafasi za uwenyeviti wavijiji,ujumbe serikali za vijiji na kwenye ngazi hizo na wilaya.
Makeleja anasema yeye binafsi ameweza kuelewa vitu vingi kwa kuvielewa na kuvichambua na amejiona ufahari kuchaguliwa kuwa mjumbe wa kamati ya mpango wa kutokomeza na kupinga ukatili ( Mtakuwwa) ngazi ya wilaya na kata .
Makeleja anasema wameona mabadiliko ya kisera kwenye mrengo wa kijinsia mfano kujenga vyumba vya kujistiri na upatikanaji wa taulo za kike ambapo walipigia kelele na serikali kuelewa kuanzia ngazi ya kijiji hadi taifa.
“ Vituo vya taarifa na maarifa tunajivunia TGNP kutupa nguvu ya pamoja kufanya kazi na serikali,waandishi wa habari na wadau wengine na kuondoa kero mbalimbali zinazoiguza jamii”.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464