MAHAKAMA
ya wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga imewahukumu kifungo Cha maisha Jeremia Machunga (18) na Kulwa Lugiko (28) wakazi wa Nyamishiga
halmashauri ya Msalala kwa kukutwa na kosa la kumbaka na kumlawiti
mtoto wa miaka 12 kwa zamu.
Hakimu
mkazi wa mahakama hiyo Christina Chovenye alisema hukumu hiyo
ilitolewa Jana na washtakiwa wote wawili walitenda makosa hayo mwezi
Julai,2023 ambapo mmoja alikuwa akimbaka na kumlawiti mchana na
mwingine usiku kwa siku tofauti tofauti.
Chovenye
amesema washtakiwa wote walikutwa na makosa mawili mawili na kila moja
limetolewa hukumu yake ambapo mshtakiwa wa kwanza ni Jeremia Machunga
amekutwa na kosa la kwanza la ubakaji amehukumiwa kuchapwa viboko
sita kwa mujibu wa sheria na kifungo cha maisha kwa kosa la pili la
kulawiti.
Chovenye
amesema mshtakiwa wa pili ni Kulwa Lugiko amekutwa na kosa la kubaka
amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na kosa la kulawiti amehukumiwa
kifungo cha maisha.
"Adhabu
hizo zimetokakana na kosa la ubakaji kinyume cha kifungu 131 (1) (2)
(e) na 131 (1) na kifungu Cha 154 (1)(a) kwa kosa la kulawiti cha
kanuni ya adhabu kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2022" amesema
Chovenye.
Chovenye
amesema mtoto huyo anaishi na walezi wake ambapo hasomi alikuwa
akiachwa nyumbani kulinda familia ndipo washtakiwa hao walipokuwa
wakipata mwanya wa kwenda kwenye familia hiyo nakumfanyia vitendo hivyo
kwa nyakati tofauti.
Mtoto
huyo alipohojiwa alikiri nakunieleza mahakama kuwa washtakiwa wote
wawili walikuwa wakimfanyia kitendo Cha kumbaka na kumuingilia kinyume
cha maumbile kwa siku tofauti tofauti mwingine mchana na mwingine
usiku.
Upande
wa Mashahidi wa mtoto akiwemo daktari wa kituo cha afya Bugarama
alithibitisha mtoto huyo kubakwa na kulawitiwa,askari na walezi wake
ambao ni dada na shemeji yake walieleza siku moja aliwafuma mchana
wakimfanyia kitendo hicho ndipo mtoto alipowataja wote.
Washtakiwa wote kwa pamoja hawakuwa nala kujitete ikiwa pia mahakama imewaamuru kutoa sh 500,000 kama fidia kwa mtoto huyo.
Mwendesha
Mashtaka ambaye ni wakili wa Serikali Evodia Baimo amesema adhabu
hiyo imetolewa ni sahihi kwa washtakiwa ili iwe fundisho kwa watu
wengine wenye tabia kama hizo.