Excavator ya halmashauri ya wilaya ya Kishapu ikindelea na kazi ya kutengeneza mifereji katika kijiji cha Mihama kata ya Lagana halmashauri ya Kishapu
Suzy Luhende Shinyanga press blog
Wananchi wa vijiji 22 vya halmashauri ya Kishapu Mkoani Shinyanga wameanza kunufaika na mradi wa mabadiliko ya tabia nchi, ili kuondokana na janga la njaa ambalo limekuwa likijitokeza mara kwa mara wilayani humo kutokana wilaya hiyo kuwa na ukame uliokithiri.
Baadhi ya wananchi wa vijiji hivyo wakizungumza na mwandishi wa habari hii aliyetembelea kijijini hapo jana ambapo wamesema wanaishukuru serikali kwa kusikia kilio chao cha muda mrefu kwa kuanza kutekeleza mradi huo ili waweze kulima kilimo cha umwagiliaji na kujikwamua kiuchumi.
Kabea Joseph mkazi wa kijiji cha Mwajiginya kata ya Mwaweja amesema kilio chao kikubwa kilikuwa ni ukame, hivyo kupitia mradi huo ukikamilika watakuwa na mavuno mengi ya kutosha wataondokana kilio cha njaa kilichokuwa kikijitokeza kila mwaka baada ya mvua kunyesha kidogo.
"Kwa kweli baada ya kuletewa mradi huu tumehamasika sana ndiyo maana tumeamua na sisi kutoa michango yetu kwa ajili ya kuleta mawe kwa ajili ya mradi huu, ili tuweze kutengenezewa banio letu,kwani tukitegemea mvua kila mwaka tutakuwa watu wa kulialia tu, hivyo tunaishukuru sana serikali yetu ya mama Samia Suluhu kwa kusikia kilio chetu,amesema Joseph.
Mihambo Njile mkazi wa kijiji cha Mihama Kata ya Lagana amesema kutokana na kutengenezwa kwa mfereji huo anatarajia kulima mpunga kwa wingi ili aweze kuvuna tani 10 tofauti na awali hali ilikuwa mbaya maji yalikuwa yanapelekwa na mto, lakini sasa yataelekea kwenye mashamba yao hayatapitiliza tena.
Mange Nyalulu mkazi wa kijiji cha Mihama amesema walikuwa hawana matarajio ya kulima mpunga katika eneo lao lakini kwa sasa serikali imewakumbuka wanashukuru sana kwa juhudi ya viongozi wao akiwemo mbunge wa jimbo hilo Boniface Butondo amewatetea hadi mradi huo umeanza kutekelezwa, kwani hali ilikuwa mbaya.
"Tunatarajia kupata mpunga wa kutosha ambao utatusaidia kusomesha watoto wetu,kwa kweli sisi huku mlo wetu ilikuwa ni ugali tu,wali tulikuwa tukiusikia tu maeneo mengine wakati mwingine mpaka tuende mijini ndio tunakula wali ulikuwa ni dhahabu tunashukuru sana viongozi wetu wa sasa wametuwezesha mradi huu na sisi tuko imara katika kilimo"amesema Gwisu Nkuba.

Mihambo Ngusa mkazi wa kijiji cha Mihama kata ya Lagana, amesema tumeteseka sana toka uhuru lakini baada ya kuja huyu mbunge wetu Boniface Butondo ("Ng"wanang"wanza) kwa kushirikiana na Rais wetu mpendwa mama Samia Suluhu Hasan na kutuletea mradi huu tunawashukuru sana
Naye Mtendaji wa kijiji cha Mihama David Joseph amesema wananchi walikuwa hawalimi mpunga kwa sababu maji yalikuwa hayatoshi, pia kulikuwa na mitaro ambayo ilikuwa inatorosha maji baada ya wakulima kupaza sauti na madiwani kupeleka hoja hizo halmashauri wamesikilizwa na mradi unatekelezwa.
"Kazi inayoendelea hapa ni uchimbaji wa mitaro jumla ya Sh 30 milioni zimetengwa kwa ajili ya uboreshaji wa mifereji hii ili wakulima walime kilimo chenye tija na mitaro hii ni kwa ajili ya kijiji kimoja cha Mihama, ambapo wananchi wameufurahia mradi huu utakaosaidia kuongeza uchumi wao tofauti na awali "amesema mtendaji Joseph.
Aidha afisa umwagiliaji wa halmashauri ya Kishapu Mwinula Ntwangi amesema mradi wa Mwaweja utahudumia vijiji saba lengo kuhamasisha wakulima kurudi katika kilimo cha mpunga, kwani zao hilo wananchi walikuwa hawalimi kwa sababu ya kuwa na ukame, lakini baada ya mifereji hiyo baadae wanatarajia kuwa na mitaro ya kisasa zaidi ili kumuokoa mkulima.
"Katika kijiji cha Mwaweja na Mwajiginya jumla ya sh 3.5 milioni zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu,na kutokana na ukame huu tumeona tutumie mito iliyopo katika baadhi ya maeneo yaliyopo katika baadhi ya vijiji ili mkulima aweze kupoza uchungu wa njaa kwa sababu zao la mpunga ni zao mtambuka na hivyo mradi huu utakamilika ndani ya siku saba tu,"amesema Ntwangi
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Kishapu Sabinus Chaula ambaye ndiye afisa kilimo mifugo na uvuvi amesema kutokana na ukame uliopo katika halmashauri ya Kishapu wameamua kutumia fursa na kupata maeneo kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji,ambapo walianza kutengeneza mifereji kilomita 20 na mwaka huu wametengeneza mifereji ya kilomita 32 ambayo itasaidia, katika kupata mpunga mwingi.
"Pamoja na kwamba wilaya yetu ni kame Tumepata eneo ambalo linafaa kwa umwagiliaji na tuna vijiji 22 ambavyo vinafaa kwa ajili wa kilimo cha umwagiliaji,kutokana na bajeti,katika vijiji hivyo awamu ya kwanza tumefanya vijiji vinne na mwaka huu tumeongeza vimekuwa vijiji saba, hivyo tuna jumla ya vijiji 11,"amesema Chaula.
"Na kuongeza awamu ya kwanza tumetengeneza mifereji ya kilomita 20 mwaka huu kilomita 32 tutabaki na vijiji 11 ambayo itakuwa bajeti ya mwakani na mradi wa mabadiliko ya tabia nchi unasimamiwa na ofisi ya makamu wa Rais," amesema Chaula.
"Pia tumewekeza kwenye malambo ambapo katika kijiji cha Beledi tumetumia gharama ya sh 260 milioni Muguda sh 15 milioni, Kiloleli Sh 300 milioni na kijiji cha Mihama sh 125 milioni haya yote yataongeza ufanisi wa kupata maji, hivyo wananchi wataendelea kuyatumia haya maji kwa ajili ya mifugo na umwagiliaji"ameongeza Chaula.
Excavator ya halmashauri ya wilaya ya Kishapu ikendelea na kazi ya kutengeneza mifereji katika kijiji cha Mihama kata ya Lagana halmashauri ya Kishapu
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Kishapu Sabinus Chaula ambaye ndiye afisa kilimo mifugo na uvuvi akizungumzia masuala ya kilimo cha umwagiliaji

Afisa umwagiliaji wa halmashauri ya Kishapu Mwinula Ntwangi
Wananchi wa kijiji cha Mihama Kata ya Lagana halmashauri ya Kishapu wakiwa kwenye mradi waumwagiliaji wakimsikiliza afisa umwagiliaji afisa umwagiliaji wa halmashauri ya Kishapu Mwinula Ntwangi
Mtendaji wa kijiji cha Mihama David Joseph akizungumza
Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Mihama kata ya Lagana akizungumza jinsi alivyoupokea mradi huo kwa furaha
Afisa kilimo wa kata ya Mwaweja akizungumzia mradi huo

Mwenyekiti wa kijiji cha Mihama kata ya Lagana akizungumza jinsi alivyoupokea mradi huo kwa furaha

Kazi ya kutengeneza banio katika kata ya Mwaweja ikiendelea

Wananchi wa kijiji cha Mihama wakiangalia jinsi Excavator ikiendelea kutengeneza

mifereji katika kijiji hicho