Mkuu wa shule ya sekondari Don Bosco Felix Wagi akizungumza kwenye mahafali ya kidato cha nne ambayo yamefanyika leo katika ukumbi wa shule hiyo
Na Stella Herman,Shinyanga
Wahitimu wa kidato cha nne shule ya sekondari Don Bosco Didia Wilaya ya Shinyanga,wametakiwa kuwa wazalendo kwa nchi yao na kujiepusha na makundi maovu ambayo yanaweza kuharibu maisha yao na kushindwa kufikia ndoto zao.
Akizungumza leo Octoba 21,2023 kwenye mahafali ya kidato cha nne shule ya sekondari Don Bosco,mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga David Rwazo amewataka wahitimu kuzingatia maadili waliyofundishwa shuleni.
Amesema kwa sasa kuna wimbi kubwa la vijana kujihusisha na vitendo ambavyo vinachangia kuporomoka maadili,ambapo amewasisitiza watakapoenda mitaani wawe waadilifu ili waweze kufikia ndoto zao walizojiwekea.
"Hapa kila mmoja ana malengo yake na ndoto zake alizojiwekea kufikia,nitumie fursa hii kuwasihi msijihusishe na makundi ambayo yanaweza kuharibu mafanikio yenu yote ya miaka minne mliyosoma na kuishia pabaya"amesema David
Kwa upande wake Mkuu wa shule ya Sekondari Don Bosco Felix Wagi ameseme wanafunzi hao wamewalea katika maadili mazuri na wanaamini hata watakapo kwenda kwenye jamii watakuwa walimu wazuri wa kufundisha wengine kuwa na matendo mema .
Katika hatua nyingine amezungumzia changamoto zilizopo ikiwa ni pamoja na tatizo la umeme kukatika muda mrefu ambapo wamekuwa wakishindwa kufanya shughuli ambazo zinahitaji kuwa na nishati hiyo hivyo kupoteza muda mwingi bila kukamilisha kazi hiyo.
Changamoto nyingine ni kukosa maji ya Ziwa Victoria ambapo kwa sasa wanatumia ya kisima kilichopo shuleni na wakati mwingine kinazidiwa kutokana na matumizi makubwa na ameiomba serikali kuwasaidia ili kumaliza tatizo hilo kwa kufikisha maji ya Ziwa Victoria.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga David Rwazo,akitoa neno kwa wahitimu na kuwataka kuwa wazalendo.
Mkuu wa shule ya sekondari Don Bosco Felix Wagi akimkabidhi mgeni rasmi CD ya kwaya ambayo imeandaliwa na wanafunzi wa shule hiyo kwa ajili ya kuizindua rasmi
Wahitimu wakifuatilia.
Wahitimu wakifurahia jambo
Baadhi ya wahitimu.
Wahitimu wa kidato cha nne shule ya sekondari Don Bosco
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464