WANANCHI KISHAPU WAOMBA KUTENGENEZEWA BARABARA




Mbunge wa jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Boniface Butondo akizungumza na wananchi wa kata ya Itilima Mkoani Shinyanga

Suzy Luhende, Shinyanga press blog

Wananchi wa kata ya Itilima halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga wameiomba serikali iwatengenezee barabara ambazo hazipitiki, kwani wanapata shida katika nyakati za mvua wanapohitaji kuvuka kwenda maeneo mengine kwa ajili ya shughuli za kiuchumi.

Hayo wameyasema leo mbele ya mbunge wa jimbo hilo Boniface Butondo alipokuwa akifanya ziara wilayani humo, ambapo wamesema kuwa serikali kupitia viongozi wake inafanya maendeleo makubwa sana katika awamu ya sita hivyo wamesema barabara zilizoharibika ziweze kukarabatiwa kabla ya mvua.

Wananchi hao akiwemo Joseph Mwandu wa kijiji cha Ikoma amesema ungonjwa mkubwa katika kijiji hicho ni barabara ya
Mwamala A kuja Ikoma imeharibika

hivyo ombi lao kubwa wakarabatiwe barabara zilizopo, kwani wakati wa mvua hata pikipiki magari hayawezi kupitika, hata wanapokuwa na mgonjwa anaweza kufariki kutokana na kukwama kwenye matope usafiri anaotumia.

"Tunakushukuru sana mbunge wetu kwa kuendelea kutukumbuka na kuja kusikia kero zetu na tunashukuru toka uingie madarakani tunaona mabadiliko makubwa kuna barabara zilikuwa mbaya kabisa sasa zinapitika, hivyo tunaomba tena zile ambazo zimeharibika zitengenezwe ili ziweze kupitika vizuri,"amesema Mwandu.

Nkuba Mboje mkazi wa kata ya Itilima amesema wakandarasi wanaofika kata hiyo kutengeneza barabara zao waanze mapema kabla ya mvua haijaanza kunyesha ili inaponyesha mvua zikutwe ziko imara.

Aidha meneja wa wakala wa barabara za mijini na vijijini Tarura mhandisi Richard Kachwele amesema zaidi Sh158 milioni zimetengwa kwa ajili ya kutengeneza barabara za kijiji cha Ipeja Itilima lengo ni kuinua tuta,na kwa sasa kuna barabara 1400 na zikiunganishwa na za Tasaf zinafika 1500, hivyo serikali imefanya kazi kubwa mpaka sasa.

"Barabara zote zipo kwenye mpango wa kutengenezwa na hii inafanyika kwa sababu viongozi wenu wako shupavu na mbunge anapokuwa bungeni tunamuona anakuwa moto kwelikweli,na sisi kama Tarura tumejipanga kutekeleza vizuri irani ya Chama Cha Mapinduzi CCM na sasa tumejipanga kutengeneza kilomita 1200 za barabara,"amesema Kachwele.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo hilo Boniface Butondo amesema serikali ya awamu ya sita inampango wa kutengeneza barabara zote zinazosumbua kuanzia kijiji hiki mpaka jimbo lote, tayari barabara nyingi zimeshatengenezwa zinapitika vizuri, hizi zilizobaki tayari zipo katika bajeti ya kutengenezwa ili zipitike vizuri.

"Barabara ya Ikoma tunataka tulinyanyue kilomita mbili na tuongeze Culvate, hivyo tunahitaji mkandarasi mzuri wa kutengeneza na kuimarisha vizuri barabara kinachotakiwa ni kusomba moram za kutosha ili pasiendelee kuwa na shimo ili magari yasikwame tukomeshe tatizo hili la barabara,"amesema Butondo

"Rais wetu mama Samia Suluhu anatoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo zikiwemo barabara hali ya barabara nyingingi ni nzuri tofauti na awali kwa hiyo hata hizi zilizobaki zitaboreshwa tu msiwe na wasiwasi kabisa nipo kwa ajili yenu nawapigania wananchi wangu ili kuhakikisha tunaondokana kabisa na kero za barabara, "ameongeza.

"Hii miradi yote iliyofanyika ni ndani ya miaka mitatu, na haya yote ni kwa sababu ya kuikomboa Itilima ninafanya haya kwa sababu niliahidi,sinaga ahadi hewa mimi nilichokiahidi ndiyo kinafanyika kwa wakati mwafaka ,"amesma Butondo

Mbunge wa jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Boniface Butondo akizungumza na wananchi wa kata ya Itilima Mkoani Shinyanga

Mbunge wa jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Boniface Butondo akizungumza na wananchi wa kata ya Itilima Mkoani Shinyanga
Meneja wa wakala wa barabara za  mijini na vijijini Tarura mhandisi Richard Kachwele akitoa majibu kwa wananchi wa kata ya Itilima
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga  Shija Ntelezu akizungumza na wananchi kwenye kikao cha Mbunge Kijiji cha Ikoma 
Wananchi wakimsikiliza mbunge wa jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga











Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464