Mbunge wa jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Boniface Butondo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ipeja Kata ya Itilima wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga.
Suzy Luhende Shinyanga press Blog
Wananchi wa vijiji nane katika kata ya Itilima halmashauli ya Kishapu Mkoani Shinyanga wametoa kilio chao mbele ya mbunge wa jimbo hilo Boniface Butondo kwamba serikali imewasahau kuwapelekea maji safi na salama hali ambayo imekuwa ikisababisha ndoa nyingi kuachika na wanawake kupigwa na waume zao kwa kuchelewa wakati wakitafuta maji.
Kilio hicho wamekitoa leo mbele ya mbunge wao Boniface Butondo, alipokuwa kwenye ziara ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi ambapo wamesema serikali inaendelea kufanya maendeleo makubwa, lakini imewasahau kwenye huduma ya maji wanapata shida ndoa zao hazina amani wanawake wanapigwa wanapochelewa wakati wakitafuta maji.
Rejina Kasembe mkazi wa kijiji cha Ilebelebe kata ya Itilima amesema hali ya afya ni mbaya wamekuwa wakiumwa matumbo mara kwa mara na wanawake ndio wanateseka zaidi kutafuta maji, wakitoka usiku saa 10 wanarudi saa mbili ya asubuhi wanagombezwa na waume zao wengine wanapigwa.
"Tunashukuru sana mheshimiwa mbunge kwa kututembelea siku ya leo tunaziona kazi zako na tunaona maendeleo unayoyafanya katika jimbo letu kwa kushirikiana na Rais watu Samia Suluhu, ila shida yetu iliyobaki ni maji safi na salama, kwani toka uhuru tunakunywa maji yasiyo salama na kuyapata ni mpaka uhangaike tunakuomba utupelekee kilio hiki kwa Rais wetu mpendw tupate maji na sisi ili tupate amani,"amesema Rejina Kasembe.
"Kero yangu kubwa ni maji tu sisi wanawake hatulali tunakesha tukitafuta maji tunaomba sana serikali yetu isikie hiki kilio itukumbuke maana tunaonekana tumesahaurika kabisa, tumelia muda mrefu sasa tunaomba mtufute machozi kwa kutuletea maji tunakujua wewe ni jembe maana tunakusikia kwenye radio tv unavyotutetea"amesema Kija Masanja.
Mseven Nkuba mkazi wa kata ya Itilima amesema kweli kero kubwa iliyopo katika kata ya Itilima ni maji wanawake wanatoka usiku kufuata maji wakati mwingine wanaume wanakuwa na hofu wanawafuatilia, hivyo amani haipo kwenye ndoa kwa sababu ya maji.
"Hata tendo la ndoa imekuwa ni shida kulipata kwa wanandoa kwa sababu wanawake wanadai wamechoka kwa sababu ya kutafuta maji, hivyo tunaomba serikali inusuru ndoa zetu, wanaume wengi wanahisi labda wanawake wanawanaume wengine huko wanakofuata maji, wasiwasi umetanda ndani ya ndoa zetu tunakuamini mbunge wetu unapiga kazi, katupambanie bajeti iongezwe tupate maji jamani"amesema Kashinje Luhende.
Kwa upande wake kaimu meneja wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira vijijini Ruwasa mhandisi Hamis Kiswala amesema kweli kata ya Itilima ina shida ya maji ambayo ina vijiji nane,hivyo miundombinu ya maji itaanza kujengwa mwaka huu wa fedha 2324 wanaenda taratibu kulingana na bajeti.
"Mkakati wetu ni kuhakikisha mnapata maji najua mna adha kubwa ya maji na ni lazima tuhakikishe tunawaletea maji tunaanza na visima virefu katika mpango mfupi na mpango wa muda mrefu ni kuhakikisha mnapata maji ya ziwa victoria,"amesema Kiswala.
Kiswala amesema zaidi ya Sh 3 bilioni zitatumika kwa ajili ya kuleta maji katika kijiji cha Ilebelebe Ikoma Ipeja na Itilima hivyo wataanza na vijiji vinne tunaanza huku wakijiandaa na vijiji vingine kuyatoa kata ya ukunyenge kuja Nhobola awamu ya kwanza yataingia kwenye mfumo wa visima na katika mpango wa mda mrefu watapata maji ya ziwa victoria.
Aidha Mbunge wa jimbo hilo Boniface Butondo amesema kweli hali ni mbaya ya maji katika kata hii na baadhi ya kata zingine, hivyo ataendelea kuhakikisha anahangaika ili kuhakikisha zinapatikana fedha, kata ya Itilima na kata zingine zinapata maji, na mkakati uliopo Itilima ipate maji safi na salama.
" Kwanza poleni sana ndugu zangu kwa kilio hiki cha ukosefu wa maji kwa muda mrefu, mimi kama mbunge wenu nimekuwa nikipiga kelele siku zote ili mpate maji na maendeleo mengine na nitaendelea kuhangaika usiku na mchana ili kuhakikisha mnapata maji safi na salama na kila kitongoji kitakuwa na maji kwani pasipo maji mambo mengi ya kifamilia hayaendi,"amesema Butondo
"Kweli wanaume wanakaa na wasi wasi kwa sababu ya wanawake kuamka asubuhi, hivyo tukileta maji tutapunguza adha kubwa sana, hilo tumeliona tunaomba mtuvumilie kidogo na mtuamini tatizo hili tunaenda kuliondoa kabisa katika kata na jimbo lote kwa ujumla, serikali ya mama yetu mpendwa mama Samia haidanganyi inafanya kazi kwa vitendo na mimi nipo kwa ajili
yenu nitumeni nitatumika,"ameongeza.
Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniface Butondo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ikoma kata ya Itilima

Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniface Butondo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ipeja kata ya Itilima

Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniface Butondo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ilebelebe kata ya Itilima

Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniface Butondo akiwa amefungwa nguo na wanawake wa Kijiji cha Ipeja kata ya Itilima.
Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniface Butondo akishukuru kwa mwananchi aliyemshukuru kwa kuwapelekea miradi ya maendeleo mbalimbali ambaye alilia kwa machozi na kuhoji alikuwa wapi siku zote hawakuwa na barabara baada ya kuingia yeye madarakani barabara zinatengenezwa na zinapitika
Wananchi wa kijiji cha Ikoma kata ya Itlilima wilayani Kishapu wakimsikiliza mbunge wa jimbo hilo Boniface Butondo

Mwananchi wa kijiji cha Ilebelebe akitoa shukrani kwa mbunge kwa utetezi anaoufanya huko bungeni kwani wanamuona anafanya kazi kubwa na utekelezaji unafanyika katika awamu ya sita
Mwenyekiti wa kijiji cha Ikoma akizungumza kwenye mkutano wa Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniface Butondo
Mwananchi wa kijiji cha Ilebelebe akizungumza kwenye mkutano wa Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniface Butondo
Diwani wa kata ya Talaga Richard Dominiko akizungumza na wananchi wa kata ya Ilebelebe kwenye mkutano wa mbunge wa jimbo hilo
Kaimu meneja wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira vijijini Ruwasa mhandisi Hamis Kiswala akitoa majibu kwa wananchi
Wananchi wa kijiji cha Ikoma wakimsikiliza mbunge wa jimbo la Kishapu Boniface Butondo