Wanawake wa Mkoa wa Shinyanga wakicheza kwenye kongamano la wanawake Mkoani hapa
Suzy Luhende, Shinyanga press blog
Wanawake Mkoani Shinyanga limempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi ya kufanya miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoani hapa na mikoa mingine, ikiwemo ya sekta ya afya, elimu, nishati ya umeme na maji.
Pongezi hizo wamezitoa leo oktoba 12, 2023 kwenye kongamano lililofanyika leo mjini Shinyanga likiongozwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme lililohudhuliwa na mwenyekiti wa chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa Mabala Mlolwa na mwenyekiti wa chama Cha Mapinduzi mkoa wa Simiyu Shemsa Mohamed, pamoja na viongozi mbalimba wa kimkoa na kitaifa.
Mndeme aliwaeleza wanawake hao kuwa Serikali ya awamu ya sita imeleta fedha nyingi za maendeleo, na kila Kijiji kimefikiwa na mradi, ambapo katika sekta ya elimu Serikali imeleta zaidi ya Sh 53.6 bilioni shule mpya 24 hivyo zimeongezeka, maabara 57 kwa shule za sekondari na nyumba za walimu 69.
Alisema upande wa nishati ya Umeme Serikali imeleta zaidi ya Sh 323 bilioni kwaajili ya mradi mkubwa wa nishati ya Umeme ukiwemo umeme wa jua ambao utakuwa kwenye Kijiji Cha Talagha wilayani Kishapu utakuwa ni mradi mkubwa kwa Afrika Mashariki .
"Tunampongeza sana Rais wetu kwa kufanya maendeleo katika Mkoa wetu na Taifa kwa ujumla, umeme huo utatarajia kutoa Megawati 150 na kuondokana na changamoto ya wananchi kukosa Umeme kwa tatizo la kukatikakatika pia tunampongeza kwa kuweza kupata PHD ya heshima huko nchini India,"amesema Mndeme.
Mndeme amesema kupitia mradi wa nishati ya umeme vijijini (REA) kwa Mkoa wa Shinyanga kuna jumla ya vijiji 240 vimepitiwa na umeme huo, hayo ni mafanikio makubwa, hivyo wanawake hatuna budi kumpongeza na kumuombea ili mwaka 2025 aweze kushinda ushindi wa kishindo.
Aidha amesema katika sekta ya Afya Mkoani Shinyanga hospitali zilikuwa nane na sasa zimeongezeka mbili nakufikia hospitali kumi ambapo hospitali ya halmashauri Ushetu na halmashauri ya wilaya ya Shinyanga zimeanza kufanya kazi na Vituo vya afya vimeongezeka sita nakufikia 25 na zahanati kumi na moja zimeongezeka nakufikia zahanati 242.
"Serikali yetu imeleta zaidi ya Sh 102 bilioni na kutekeleza miradi ya maji 47 sawa na ongezeko la miradi 15, huku miradi mipya 66 ikianzishwa katika vijiji mbalimbali kwa lengo la kumtua ndoo mwanamke kichwani"amesema Mndeme.
Pia amesema ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM imetekelezwa kwa uwazi na ukweli miradi mbalimbali ya maendeleo, kwani maendeleo wanayaona hawana cha kusema zaidi ya kusema Rais asante, kwani mkoa wa Shinyanga mwaka 2021 haukuwa kama ulivyo sasa ameubadilika.
Diwani viti Maalum Ester Matone na makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Msalala Flora Sagasaga wamesema katika miradi ya maji na afya wananchi wameondokana na changamoto zilizokupo zamani za kuchangia maji na wanyama na tatizo la kuzalia njiani kwa huduma za afya kuwa mbali.
Kwa upande wake Daktari bingwa wa watoto kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga Justina Tizeba amesema katika sekta ya afya upo ushuhuda wa kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga sababu ya uwepo wa hospitali karibu na wananchi katika maeneo mengi.
Katika kongamano hilo viongozi mbalimbali wa Mkoa na wilaya walihudhulia wakiwemo wabunge wa viti maalumu Mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga, Santiel Kirumba na Chrisitina Mzava.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiwa na viongozi mbalimbali kwenye kongamano la wanawake Mkoa wa Shinyanga
Wanawake wa Mkoa wa Shinyanga wakicheza kwenye kongamano la wanawake Mkoani hapa
Wanawake wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa akizungumza kwenye kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu kwakufanya maendeleo makubwa
Wanawake wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa akizungumza kwenye kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu kwakufanya maendeleo makubwa
Wanawake wakifurahia jambo baada ya Mkuu wa Mkoa kuzungumza kwenye kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu kwakufanya maendeleo makubwa
Wanawake wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa akizungumza kwenye kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu kwakufanya maendeleo makubwa
Wanawake wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa akizungumza kwenye kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu kwakufanya maendeleo makubwa