Mgeni rasmi ambaye meneja wa benki ya NMB tawi la Manonga Shinyanga akiongea kwenye Mahafali ya tisa ya kidato cha nne katika shule ya Mtakatifu Fransisco wa Asizi.
Kareny Masasy, Shinyanga
WAZAZI wanaosomesha shule ya sekondari ya Mtakatifu Fransisco wa Asizi inayomilikiwa na kanisa katoliki la mama mwenye huruma Ngokolo mkoani Shinyanga wamepongezwa kuwasomesha watoto wao bila kukata tamaa kwani kufanya hivyo hawajapoteza wamejenga maisha ya watoto wao ya baadaye.
Hayo yamesemwa leo na mgeni rasmi Gadiel Sawe ambaye ni meneja wa benki ya NMB tawi la Manonga mjini Shinyanga katika mahafali ya tisa ya shule hiyo kwa kidato cha nne ambapo amechangia mifuko kumi ya saruji kuendeleza ujenzi wa majengo shuleni hapo.
“Ninawaomba wale wanafunzi wanaohitimi tunawatakia maandalizi mema ya mtihani wa taifa na maisha yenye utii wanapokwenda kuishi mitaani na majumbani mwao wakawe mfano wa kuigwa.”amesema Sawe.
Mwalimu mkuu msaidizi wa shule hiyo Maduhu Shauri akisoma taarifa ya shule katika mahafali amesema dhamira ya yao wamekuwa wakisisitiza bidii katika masomo na mazingira mazuri ya kujifunzia.
Mwalimu Maduhu amesema wamelenga pia kuwafundisha wanafunzi elimu ya dini na kijamii kwa kuamini shughuli zote wazifanyazo mungu yupo hasa kutafuta mafanikio.
“Malengo
yetu ni nguvu ya pamoja,mshikamano na
upendo lakini yapo mafanikio mazuri ya
kitaaluma kwa ufaulu mzuri wa kidato cha
pili na kidato nne na matarajio ya matokeo ya mwaka huu kuondoa kabila sifuri
na ufaulu wa daraja la nne"amesema Shauri.
Mwanafunzi Anatory Anicet kwa niaba ya wanafunzi wenzake aliyesoma risala kwa kueleza changamoto za shuleni hapo amesema shule ni mchanganyiko wavulana na wasichana ina mazingira mazuri ya kujifunzia na maabara kwa kujifunza kwa vitendo pia kuna mabweni.
Wahitimu wa kidato cha nne wakijiandaa kuingia ukumbini.
Mgeni rasmi ambaye ni Meneja wa benki ya NMB tawi la Manonga Shinyanga akiwasili kwenye Mahafali.
Wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya Mtakatifu Fransisco wa Asizi
Wanafunzi wa kidato cha nne wanaotarajia kuhitimu.
Wanafunzi wa shule hiyo wakitoa burudani kwenye mahafali ya kidato cha nne.
Mkuu wa shule hiyo Elmida Nkulu akimkaribisha mgeni rasmi katika Mahafli ya kidato cha nne.
Wageni waalikwa wakiwa kwenye Mahafali.
Mwalimu mkuu msaidizi wa shule hiyo Maduhu Shauri.
Wanafunzi wakitoa burudani kwenye Mahafali.