AMREF TANZANIA YAONESHA SHUGHULI INAZOFANYA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI

 

Mkurugenzi mkazi wa Amref Health Africa Tanzania, Dkt Florence Temu akitoa maelezo kwa Mratibu wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) nchini Tanzania Bi. Jessica Greene (wa pili kushoto) pamoja na mkurugenzi mkazi wa Shirika la Kimarekani la Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa (CDC), Dk. Mahesh Swaminathan (wa kwanza kulia) wakiongozana na wawakilishi wa (U.S Government  Agency Leads (USAID, Peace Corps na WRAIR) katika banda la Amref Tanzania wakati wa maonesho ya shughuli zinazofanywa na wadau katika mapambano dhidi ya UKIMWI katika Viwanja vya Morogoro Sekondari mkoani Morogoro.


Hii ni katika wiki ya maadhimisho kuelekea siku ya UKIMWI duniani. Kwa ufadhili wa PEPFAR kupitia U.S CDC Tanzania, Amref Tanzania inatekeleza mradi wa Afya Thabiti kwa kushirikiana na CIHEB na TCDC katika mikoa ya Simiyu na Mara kwa Tanzania Bara pamoja na Zanzibar.

Mradi huo una lengo la kuimarisha utoaji wa huduma na matibabu ya kufubaza VVU katika Kliniki za VVU/UKIMWI za serikali na za hospitali teule kuongeza kasi ya kufikia malengo ya 95-95-95 ya kudhibiti janga la Ukimwi nchini.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Prof. Joyce L. Ndalichako ( wa tatu kushoto) akiwa katika Banda la Wasichana Balehe na Wanawake Vijana (AGYW) walio chini ya Programu ya Global Fund Timiza Malengo na kujionea shughuli zinazofanywa na vijana hao katika viwanja vya Morogoro Sekondari mkoani Morogoro.

Amref Tanzania inashirikiana na TAYOA katika programu ya Timiza Malengo kupitia ufadhili wa Global fund ambapo wasichana balehe na wanawake vijana hunufaika na programu hiyo kwa kupewa elimu ya mabadiliko ya tabia na kuanzishiwa miradi ya ujasiriamali ili kuepuka vishawishi vitakavyowaweka katika hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Prof. Joyce L. Ndalichako ( wa tatu kushoto) akiwa katika Banda la Wasichana Balehe na Wanawake Vijana (AGYW) walio chini ya Programu ya Global Fund Timiza Malengo na kujionea shughuli zinazofanywa na vijana hao katika viwanja vya Morogoro Sekondari mkoani Morogoro.


Mkurugenzi Mkazi wa Amref Heath Africa Tanzania Dkt Florence Temu alipotembelea banda la TAYOA nakusikia shuhuda za wanufaika wa mradi wa Timiza Malengo kupitia ufadhili wa Global Fund. Amref Tanzania inashirikiana na TAYOA katika programu ya Timiza Malengo ambayo wasichana balehe na wanawake vijana hunufaika na programu hiyo kwa kupewa elimu ya mabadiliko ya tabia na kuanzishiwa miradi ya ujasiriamali ili kuepuka vishawishi vitakavyowaweka katika hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI.



Kwa miaka zaidi ya 30 sasa, Shirika la Amref limekuwa likishirikiana na serikali pamoja na wadau wengine kuboresha mifumo ya afya nchini.




Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464