MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA WALALAMIKIA KUTOKAMILISHWA MABOMA YALIYOANZISHWA KWA NGUVU ZA WANANCHI

MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA WALALAMIKIA KUTOKAMILISHWA MABOMA YALIYOANZISHWA KWA NGUVU ZA WANANCHI

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MADIWANI wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wamewasilisha taarifa za utekelezaji wa shughuli za Maendeleo kwenye Kata zao, na kulalamikia tatizo la kushindwa kukamilishwa maboma ambayo yalianzishwa kwa nguvu za wananchi.

Wamewasilisha taarifa zao leo Novemba 1,2023 kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Madiwani hao kutoka Kata 26 za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, kila mmoja wakati akiwasilisha taarifa za kwenye Kata yake changamoto ambazo zilionekana kugusa kila Kata ni kilio cha ukamilishwaji wa maboma ambayo yalianzishwa kwa nguvu za wananchi ikiwamo Sekta ya Afya na Elimu.

Changamoto zingine ambazo ziliwasilishwa na Madiwani hao ni ukosefu wa Miundombinu ya Barabara, Maji kutoka Ziwa Victoria, Umeme, upungufu wa watumishi, mrudikano wanafunzi darasani, pamoja na Mgogoro wa mipaka Kati ya Mwakitolyo na Nyanh'wale Geita.
Naye diwani wa Bukene Majaliwa Luhende, amesema kutokana changamoto zote zilizowasilishwa na Madiwani zinafanana kila Kata, ni vyema sasa Halmashauri kupitia mapato yake ya ndani ikazitatua changamoto hizo kwa awamu awamu ili kumaliza kero hizo kwa wananchi, ikiwamo ukamilishwaji huo wa maboma na kutoa huduma.

"Changamoto nyingi katika taarifa ambazo zimesomwa na Madiwani karibia zote zinajirudia tu, ni vyema sasa Halmashauri ikaangalia zile ambazo wana uwezonazo kuanza kuzitatua," amesema Luhende.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nicodemas Simoni, amesema kutokana na changamoto nyingi kujirudia kwa kila Kata, Menejiment ya Halmashauri ianishe changamoto zote ambazo wanauwezo wa kuzitatua kupitia mapato ya ndani.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga David Rwazo, amesema suala la ukamilishwaji wa maboma yaliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi wataendelea na juhudi za kuyakamilisha kupitia mapato ya ndani, huku akibainisha kuwa maboma 42 yamesha yakabidhi TAMISEM kwa ajili ya kusaidia kuyakamilisha.
Amesema kwa upande wa upungufu wa Watumishi tayari limeshaanza kufanyiwa kazi na Watumishi 168 wameajiriwa wilayani humo kutoka Kanda mbalimbali, huku wakiendelea kuomba maombi ya kupatiwa Watumishi wengine, na kwa Changamoto zingine ambazo zimewasilishwa zitaendelea kutatuliwa kwa kushirikiana na Taasisi za Serikali.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga David Rwazo akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nicodemas Simon akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga likiendelea.
Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga likiendelea.
Diwani wa Lyamidati Veronica Mabeja akisoma taarifa ya kwenye Kata hiyo kikao cha Baraza la Madiwani.
Madiwani wakiendelea na kikao cha Baraza.
Diwani wa Vitimaalum Mengi Zengo akisoma taarifa ya Kata ya Didia kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Kikao cha Baraza la Madiwani kikiendelea.
Madiwani wakiendelea na kikao cha Baraza.
Madiwani wakiendelea na kikao cha Baraza.
Madiwani wakiendelea na kikao cha Baraza.
Diwani wa Solwa Awadhi Mbaraka akiwasilisha taarifa ya Kata hiyo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Madiwani wakiendelea na kikao cha Baraza.
Kikao cha Baraza la Madiwani kikiendelea.
Madiwani wakiendelea na kikao cha Baraza.
Madiwani wakiendelea na kikao cha Baraza.
Madiwani wakiendelea kuwasilisha taarifa za Kata.

Baraza la Madiwani likiendelea.
Madiwani wakiendelea na kikao cha Baraza.
Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga likiendelea.
Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga likiendelea.
Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga likiendelea.
Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga likiendelea.
Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga likiendelea.
Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga likiendelea.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464