MAKAMU MWENYEKITI HALMASHAURI YA SHINYANGA ANG’AKA UKUSANYAJI MAPATO,BARAZA LA MADIWANI


MAKAMU MWENYEKITI HALMASHAURI YA SHINYANGA ANG’AKA UKUSANYAJI MAPATO,BARAZA LA MADIWANI

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MAKAMU Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nicodemus Simoni, amesema haridhishwi na ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri hiyo, pamoja na baadhi ya Watumishi kubaki na fedha za mapato mifukoni badala ya kuzipeleka Benki.

Amebainisha hayo leo Novemba 2, 2023 kwenye kikao cha siku ya pili cha Baraza la Madiwani katika Halmashauri hiyo ya wilaya ya Shinyanga.
Amesema hali ya ukusanyaji wa mapato katika halmashauri hiyo hauridhishi, huku akikemea suala la baadhi ya Watumishi ambao hukusanya mapato hubaki na fedha hizo mifukoni na kutozipeleka benki.

“Mapato katika Halmashauri yetu hayapo sawa, pia kuna fedha za mapato Sh.milioni 107 zimekusanywa zimebaki kwenye mifuko ya watu badala ya kuzipeleka benki, itapendeza Mkurugenzi watu hawa uwachukulie hatua,”amesema Simon.
Aidha, ameeleza kusikitishwa na jambo jingine la fedha za Miradi ya Maendeleo ambazo zimekuwa zikiletwa wilayani humo na kushindwa kufanya kazi iliyokusudiwa na matokea yake zinarudi hazina, na wakati wanakabiliwa na tatizo umaliziaji wa miradi viporo yakiwamo maboma ambayo yameanzishwa kwa nguvu za wananchi kwamba fedha hizo zingefanya kazi hiyo.

“Sasa hivi tuna Sh.bilioni 3.3 fedha ambazo zimeletwa kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo, na Rais Samia katika Halmashauri yetu amekuwa akileta fedha nyingi kweli, tunataka fedha hizi zitumike zisirudi, na yule ambaye atatukwamisha hatutasita kumchulia hatua,”amesema Simon.
Nao Madiwani wa Halmashauri hiyo wakati wa kuuliza maswali ya papo kwa papo pamoja na kuchangia taarifa za Kamati mbalimbali, walihoji juu ya ukusanyaji mapato, ukamilishwaji Jengo la Utawala la Halmashauri hiyo, Mgogoro wa mpaka kati ya Mwakitolyo na Nyan’hwale Geita na kusababisha kukosa mapato kwa wachimbaji.

Maswali mengine ni ubovu wa Miundombinu ya Barabara, ukosefu wa Maji, ukamilishaji wa ujenzi wa maboma yakiwamo ya Zahanati, na ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Lyabusalu.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga David Rwazo, akizungumza kwenye kikao hicho, aliwaomba Madiwani kwa kushirikiana na Wataalamu kuendelea kubuni vyanzo mbalimbali vya kuongeza mapato, ili halmashauri ipate mapato mengi na kuendesha shughuli mbalimbali ikiwamo utekelezaji wa miradi ya maendeleo hasa viporo.

Amesema maelekezo yote yalitolewa kwenye kikao hicho cha Baraza la Madiwani wameyapokea na watayafanyia kazi, kwa mustakabali wa Maendeleo ya Halmashauri hiyo.
Nazo baadhi Taasisi za Serikali zikiwasilisha taarifa zao kwenye kikao cha Baraza hilo la Madiwani na kujibu hoja, ikiwamo TARURA ambapo Kaimu Meneja wa TARURA wilaya ya Shinyanga Mhandisi Kulwa Maige, amesema katika mwaka wa fedha (2023/2024)wametenga kias cha fedha Sh. Bilioni 2.6 kwa ajili ya matengenezo ya Barabara, Madaraja na Makaravati

Kwa upande wa RUWASA Kaimu Meneja wa RUWASA Mhandisi Andrew Mongella, amesema wao wametenga zaidi ya Sh.bilioni 4.3 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji katika maeneo mbalimbali wilayani huo.
TAZAMA PICHA KIKAO BARAZA LA MADIWANI👇
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nicodemus Simon akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga David Rwazo akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Shinyanga Abrahim Makana akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani
Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga Said Kitinga akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Edward Ngelela akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Kaimu Meneja wa TARURA Wilaya ya Shinyanga Mhandisi Kulwa Maige akiwasilisha taarifa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Kaimu Meneja wa RUWASA Wilaya ya Shinyanga Mhandisi Andrew Mongella akiwasilisha taarifa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza.
Diwani wa Solwa Awadhi Mbaraka akichangia hoja kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza.
Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza.
Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza.
Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza.
Diwani wa Iselamagazi Isack Sengerema akichangia hoja kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza.
Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza.
Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza.
Diwani wa Lyamidati Veronica Ndutwa akichangia hoja kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza.
Kikao cha Baraza la Madiwani kikiendelea.
Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza.
Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza.
Baraza la Madiwani likiendelea.
Baraza la Madiwani likiendelea.
Baraza la Madiwani likiendelea.
Baraza la Madiwani likiendelea.
Baraza la Madiwani likiendelea.
Baraza la Madiwani likiendelea.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464