UWT KOLANDOTO WAMPONGEZA RAIS SAMIA UBORESHAJI HUDUMA ZA AFYA,WATOA MSAADA WODI YA WATOTO HOSPITALI YA KOLANDOTO

UWT Kolandoto wampongeza Rais Samia uboreshaji huduma za Afya, watoa msaada wodi ya watoto Hospitali ya Kolandoto

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

UMOJA wa Wanawake wa CCM Tanzania (UWT) Kata ya Kolandoto wilaya ya Shinyanga Mjini, wamempongeza Rais Samia uboreshaji wa huduma za Afya hapa nchini.

Wametoa pongezi hizo leo Novemba 3,2023 wakati walipotembelea Hospitali ya Kolandoto, na kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika Wodi ya Watoto pamoja na kuwapatia faraja wazazi kuwa watoto wao watapona na kupata Afya njema.
Mwenyekiti wa UWT Kata ya Kolandoto Zinila Kalwani, amesema wameamua kutembelea kwenye Hospitali hiyo ya Kolandoto na kutoa msaada katika Wodi ya watoto na faraja, ikiwa ni sehemu ya kumpongeza Rais Samia katika uboreshaji wa huduma za Afya hapa nchini na kuokoa Afya za wananchi.

“UWT Kata ya Kolandoto tumeguswa sana na uongozi wa Rais Samia ambaye pia ni Mwenyekiti wetu wa Chama cha CCM Taifa, anafanya kazi kubwa ikiwamo uboreshaji wa huduma za Afya, na sisi tukaamua tumpongeze kwa kutoa msaada na faraja kwa Wagonjwa katika Hospitali hii ya Kolandoto,”amesema Zinila.
Aidha, ametaja msaada wa vitu ambavyo wametoa kwenye Wodi ya watoto katika Hospitali hiyo ya Kolandoto, kuwa ni Sabuni za kufulia, vyombo vya kuhifadhia maji ya kunywa kwa watoto, pamoja na Juice.

Nao wazazi katika Wodi hiyo ya watoto,wameeleza kufurahi kutembelewa na Umoja huo wa Wanawake, pamoja na kuwapatia faraja na misaada ya vitu mbalimbali.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya Kolandoto Dk. Joseph Wallace Sahani, amesema kitendo walichokifanya UWT Kata ya Kolandoto kwa kutembelea wagonjwa na kuwapatia misaada na faraja, ni jambo jema sababu wagonjwa hua wanahitaji kupewa faraja wakati wakiendelea na matibabu.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇
Mwenyekiti wa UWT Kata ya Kolandoto Zinila Kalwani akizungumza katika Hospitali ya Kolandoto.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Kolandoto Dk. Joseph Wallace Sahani akizungumza na wanawake wa UWT Kata ya Kolandoto.
Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania (UWT)Kata ya Kolandoto wakitoa msaada na faraja katika Wodi ya watoto katika Hospitali ya Kolandoto.

Zawadi zikiendelea kutolewa.
Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania (UWT)Kata ya Kolandoto wakitoa msaada na faraja katika Wodi ya watoto katika Hospitali ya Kolandoto.
Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania (UWT)Kata ya Kolandoto wakitoa msaada na faraja katika Wodi ya watoto katika Hospitali ya Kolandoto.
Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania (UWT)Kata ya Kolandoto awali wakiwasili katika Hospitali ya Kolandoto.

Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania (UWT) wakipiga picha ya pamoja.
Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania (UWT) wakipiga picha ya pamoja.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464