HAKIRASILIMALI YAWANOA WAANDISHI WA HABARI KUANDIKA HABARI ZA KUKABILIANA NA UHAMISHAJI HARAMU WA FEDHA KATIKA SEKTA YA UZIDUAJI TANZANIA
Na Marco Maduhu,DODOMA
TAASISI ya HakiRasilimali imetoa mafunzo kwa Waandishi wa habari, namna ya kuandika habari za kukabiliana na uhamishaji haramu wa fedha katika Sekta ya Uziduaji inayohusisha Madini, Mafuta na Gesi, (Illicit Financial Flows in Exctractive Sector) kwa ajili ya maendeleo ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania.
Uhamishaji huo haramu wa fedha katika Sekta ya Uziduaji, unatokana na ukwepaji Kodi, Utakatishaji fedha,Utoroshaji fedha na Madini Nje ya Nchi.
Mkurugenzi wa HakiRasilimali Adam Anthony.
Mafunzo hayo yametolewa leo Novemba 8,2023 Jijini Dodoma yakihusisha Waandishi wa habari kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini, ambayo yanaendana sambamba na Jukwaa la Uziduaji litakalo fanyika Kesho na Kesho kutwa ambayo yamefadhiliwa na Global Financial Itergrity.
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa HakiRasilimali Lucy Shao, amesema wameandaa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari, ili watumie Kalamu zao kuandika habari za kuzuia uhamishaji haramu wa fedha katika Sekta ya Uziduaji, na utoroshaji wa fedha na Madini nje ya nchi kwa ajili ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania.
Lucy Shao.
"Uhamishaji huu wa fedha haramu katika Sekta ya Uziduaji,utoroshaji fedha na madini nje ya nchi, una madhara makubwa katika mapato na uchumi wa nchi yetu,"amesema Shao.
Naye Mwezeshaji katika Mafunzo hayo Prof: Abel Kinyondo, amesema Sekta ya Uziduaji inamchango mkubwa katika pato la Taifa, na dhahabu pekee huchangia asilimia 86 na katika asilimia hiyo wachimbaji wadogo huchangia asilimia 30.
Prof; Abel Kinyondo.
Aidha, amesema kwa mujibu wa ‘Policy Memo kupitia Global Financial Intergrity’ Serikali ya Tanzania kwa mwaka hupoteza fedha Dola bilioni 1.5 kutokana na uhamishaji huo haramu wa fedha.
Akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa HakiRasilimali Adam Anthony, amesema mafunzo hayo kwa Waandishi wa Habari yatakuwa na mchango mkubwa katika kuongeza uwazi na uwajibikaji katika Sekta ya Uziduaji.
Katika mafunzo hayo Waandishi wa habari wamefundishwa pia namna ya kuandika habari za uchaguzi hasusani katika Sekta hiyo ya Uziduaji.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Lucy Shao akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa HakiRasilimali Adam Anthony.
Lucy Shao akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa HakiRasilimali Adam Anthony.
Francis Mkasiwa kutoka HakiRasilimali akizungumza kwenye Mafunzo hayo.
Mwezeshaji Abel Kinyondo akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya uhamishaji haramu wa fedha katika Sekta ya Uziduaji (Illicit Financial Flows).
Mwezeshaji Obiajulu Elinami kutoka Policy Forum akitoa mafunzo kwa Waandishi habari, namna ya kuandika habari za uchunguzi hususani katika Sekta ya Uziduaji, Madini, Mafuta na Gesi.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Waandishi wa Habari wakiendelea na Mafunzo.
Waandishi wa Habari wakiendelea na Mafunzo.
Waandishi wa Habari wakiendelea na Mafunzo.
Waandishi wa Habari wakiendelea na Mafunzo.
Waandishi wa Habari wakiendelea na Mafunzo.
Waandishi wa Habari wakiendelea na Mafunzo.
Waandishi wa Habari wakiendelea na Mafunzo.
Waandishi wa Habari wakiendelea na Mafunzo.
Picha ya pamoja ikipigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464