Header Ads Widget

WACHIMBAJI WADOGO WAPAZA SAUTI KWA SERIKALI UFANYIKE UTAFITI WA MAENEO YENYE MADINI

Wachimbaji wadogo wapaza sauti kwa Serikali ufanyike utafiti wa maeneo yenye madini

Na Marco Maduhu, DODOMA.

WACHIMBAJI Wadogo wa Madini wameiomba Serikali kufanya utafiti wa kubaini maeneo yenye Madini na kuyatenga,ili waachane na uchimbaji wa Madini wa kubahatisha na kusabisha uharibifu wa Mazingira.

Hayo yamebainishwa leo Novemba 10,2023 na Mchimbaji Mdogo Renatus Nsangano ambaye ni Mkurugenzi wa Mgodi wa Nsangano Gold Mining uliopo Nyarugusu mkoani Geita kwenye Jukwaa la Uziduaji la HakiRasilimali Jijini Dodoma.
Amesema wachimbaji Wadogo wa Madini ya dhahabu kwa sasa wamekuwa na Mchango Mkubwa kuchangia Pato la Taifa kwa asilimia 40, lakini bado wanakabiliwa na changamoto ya uchimbaji wa Madini wa kubahatisha, kutokana na ukosefu wa maeneo maalumu ambayo yamefanyiwa utafiti kwa ajili ya uchimbaji madini, hata kusabisha uharibifu wa Mazingira sababu ya kufanya uchimbaji holela.

"Tunaomba Serikali ifanye utafiti wa maeneo yenye Madini na kuyatenga ili wachimbaji Wadogo waache kuchimba Madini kwa kubahatisha na kutoharibu Mazingira,"amesema Renatus.
Aidha, amezungumzia pia suala la ukosefu wa mikopo, kuwa wachimbaji Wadogo Serikali inapaswa kuwaezesha pia wapate mikopo sababu kwenye mabenki hawaaminiki kutokana na ukosefu wa taarifa za kijiolojia na hivyo kukwama kupata mitaji ya kununua vifaa vya kisasa vya uchimbaji Madini na kuongeza uzalishaji.

Amezungumzia pia suala la tatizo la wachimbaji kutorosha Madini,kuwa linatokana na Kodi na Tozo kubwa katika Masoko ya Madini, na kutolea mfano Mchimbaji akiuza dhahabu ya Sh.milioni 10 Kodi yake inakatwa zaidi ya Sh.900,000.
Katika hatua nyingine amezungumzia suala la Matumizi ya Kemikali ya Zebaki, kwamba hadi kufikia mwaka 2030 Serikali itasitisha Matumizi ya Kemikali hiyo kwa Wachimbaji wadogo, nakuiomba Serikali iendelee kutafuta njia mbadala na Rafiki ya kukamatia dhahabu kwa wachimbaji Wadogo, ili kutoua uchimbaji mdogo hapa nchini sababu Tekinolojia nyingine ni gharama.

Naye Naibu Kamishina msaidizi wa Madini kutoka Wizara ya Madini Terence Ngole, amesema Serikali kwa sasa imekuwa na mikakati mikubwa kwa Wachimbaji wadogo kuwaendeleza ili waweze kuwa na Mchango Mkubwa zaidi katika kuchangia Pato la Taifa.
Amesema Wachimbaji wadogo kwa sasa wamekuwa na Mchango Mkubwa katika Pato la Taifa asilimia 40, na Wachimbaji wakubwa ni asilimia 60,na kubainisha kuwa wakiwezeshwa kimitaji na vifaa wataweza kuchangia pato jingi na hata kushinda wachimbaji wakubwa.

"Serikali ya Rais Samia imekuwa na Mkakati Mkubwa na Wachimbaji Wadogo katika kuwaendeleza ili wakue na kuendelea kuchangia Pato la Taifa na Rais ameshanunua mitambo kwa ajili ya wachimbaji Wadogo ambayo ipo STAMICO," amesema Ngole.
Akizunguzia suala la Utafiti wa maeneo yenye Madini, amesema Wizara ipo kwenye mipango ya kuanza kufanya utafiti wa maeneo yote yenye Madini, na watatenga maeneo hayo na kuwa maalumu kwa ajili ya uchimbaji wa Madini, pamoja na maeneo ambayo yatatumika kwa ajili ya kuchenjulia dhababu na kuondokana na Matumizi ya Kemikali ya Zebaki.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mchimbaji Mdogo wa Madini ya Dhahabu Renatus Nsangano akizungumza kwenye Jukwaa la Uziduaji la HakiRasilimali.
Naibu Kamishina msaidizi wa Madini kutoka Wizara ya Madini Terence Ngole, akizungumza kwenye Jukwaa la Uziduaji la HakiRasilimali.
Mbunge wa Geita Mjini Costantine Kanyasu akizungumza kwenye Jukwaa la Uziduaji wa HakiRasilimali.
Lucy Shao kutoka HakiRasilimali akiongoza Mjadala kwenye Jukwaa la Uziduaji.
Francis Mkasiwa kutoka HakiRasilimali akiongoza Mjadala katika Jukwaa la Uziduaji.
Evans Rubara kutoka FADev akiongoza Mjadala kwenye Jukwaa la Uziduaji.
Wadau wakiwa kwenye Jukwaa la Uziduaji la HakiRasilimali.
Jukwaa la Uziduaji likiendelea.
Jukwaa la Uziduaji likiendelea.
Mijadala ikiendelea kwenye Jukwaa la Uziduaji.
Jukwaa la Uziduaji likiendelea.
Mhandisi Theonestina Mwasha Mkurugenzi wa FADev akichangia Mada kwenye Jukwaa la Uziduaji.
Jukwaa la Uziduaji likiendelea.
Wadau wakiendelea kuchangia Mada kwenye Jukwaa la Uziduaji.
Jukwaa la Uziduaji likiendelea.
Mijadala ikiendelea kwenye Jukwaa la Uziduaji.
Jukwaa la Uziduaji likiendelea.
Uchangiaji Mada ukiendelea kwenye Jukwaa la Uziduaji.
Mijadala ikiendelea kwenye Jukwaa la Uziduaji.
Jukwaa la Uziduaji likiendelea.
Wadau wakiednelea kuchangia Mada kwenye Jukwaa la Uziduaji.
Jukwaa la Uziduaji likiendelea.
Jukwaa la Uziduaji likiendelea.
Jukwaa la Uziduaji likiendelea.
Uchangiaji Mada ukiendelea kwenye Jukwaa la Uziduaji.
Mijadala ikiendelea kwenye Jukwaa la Uziduaji.
Wadau wakiendelea kuchangia Mada kwenye Jukwaa la Uziduaji.
Wadau wakiendelea kuchangia Mada kwenye Jukwaa la Uziduaji.
Jukwaa la Uziduaji likiendelea.
Jukwaa la Uziduaji likiendelea.
Jukwaa la Uziduaji likiendelea.
Wadau wakiendelea kuchangia Mada kwenye Jukwaa la Uziduaji.
Wadau wakiendelea kuchangia Mada kwenye Jukwaa la Uziduaji.
Uwasilishaji wa Mada ukiendelea kwenye Jukwaa la Uziduaji.
Jukwaa la Uziduaji likiendelea.
Jukwaa la Uziduaji likiendelea.
Jukwaa la Uziduaji likiendelea.
Jukwaa la Uziduaji likiendelea.
Jukwaa la Uziduaji likiendelea.
Wawasilishaji Mada wakipiga picha ya pamoja.
Wawasilishaji Mada wakipiga picha ya pamoja.
Picha za pamoja zikipigwa.

Post a Comment

0 Comments