Header Ads Widget

KAMATI YA MAAFA YARIDHISHWA NA ULIPWAJI FIDIA WAATHIRIKA TOPE BWAWA LA MGODI WA ALMASI MWADUI


KAMATI YA MAAFA YARIDHISHWA NA ULIPWAJI FIDIA WAATHIRIKA TOPE BWAWA LA MGODI WA ALMASI MWADUI

Na Marco Maduhu, KISHAPU

KAMATI ya Maafa ambayo iliundwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kufuatia janga la kubomoka kwa kingo katika Bwawa la Majitope katika Mgodi wa Almasi Mwadui, na kuleta athari kwa wananchi ikiwamo kupoteza mali zao, mashamba na wengine nyumba, imeridhika na ulipwaji wa fidia kwa wananchi.

Kamati hiyo ambayo inaongozwa na Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude kama Mwenyekiti, imefanya ziara hiyo leo Novemba 13,2023 katika Mgodi huo ili kupata taarifa juu ya hatua ya ulipwaji fidia wananchi na wale ambao walikuwa wakidai nyumba zao, pamoja na kuona bwawa jipya la Majitope katika Mgodi huo na Maendeleo ya uzalishaji Almasi.
Awali akiwasilisha taarifa ya ulipwaji fidia wananchi na maendeleo ya uzalishaji wa Almasi, Mhandisi Mkuu wa Mgodi wa Mwadui Shagembe Mipawa, akimwakilisha Meneja Mkuu wa Mgodi huo, amesema tatizo la kupasuka kingo za Bwawa la Majitope lilitokea Novemba mwaka jana na Wananchi 304 waliathirika na tope hilo.

Amesema mpaka sasa hatu ya fidia ambayo imefikiwa ni Asilimia 99.6 kwamba kati ya wananchi hao 304, mwananchi Moja tu ndiyo ambaye hajalipwa fidia na hajulikani, huku wakiendelea na taratibu zingine za ujenzi wa nyumba kwa Kaya 47 na kuhamisha Makaburi 14.
Akizungumzia suala uzalishaji wa Almasi, amesema wanaendelea vizuri na tangu waanze uzalishaji Julai mwaka huu hadi kufikia Mwezi Septemba wamezalisha Tani Milioni 1.4 sawa na asilimia 48, Carati Laki 106 sawa na asilimia 64 ya malengo yao.

Pia amewahakikishia wananchi kwamba Bwawa hilo Jipya la Majitope ni salama, huku wakiendelea pia kulifanyia ukaguzi wa mara kwa mara pamoja na Bwawa la zamani ili lisije lete madhara kwa wananchi.
Naye Meneja Mahusiano Mgodi wa Almasi Mwadui Benard Mihayo, amesema kwa upande wa Kaya 47 ambazo zinajengewa nyumba, Kaya 4 wamegoma kujengewa wakitaka wapewe fedha, na kubainisha kuwa bado wanaendelea na mazungumzo ili kuwashawishi wajengewe nyumba hizo, sababu wakitaka walipwe fidia ya fedha itakuwa ni kiasi kidogo na hawata weza kujenga nyumba imara.

Amesema ujenzi wa nyumba hizo 43 umefikia asilimia 91.4 na hadi kufikia decemba mwaka huu zitakuwa zimeshakamilika kujengwa, na wananchi kukabidhiwa nyumba zao tayari kwa kuishi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa Kamati hiyo, ameupongeza Mgodi huo kwa kushirikiana vyema na Serikali kwa hatua zote tangu maafa yametokea na hadi sasa wapo kwenye hatua za mwisho za ukamilishaji wa kulipa fidia wananchi.

Amesema kwa wananchi wa Nne ambao wamegoma kujengewa nyumba amewasihi wakubali ili wajengewe nyumba imara, na kuishi mahali salama na kuendelea na maisha yao kama kawaida.
Aidha, ameusisitiza Mgodi wawe wanafanya pia ukaguzi wa mara kwa mara katika Bwawa jipya la Majitope, ili liendelee kuwa imara na lisije na lenyewe kuleta madhara kwa jamii kama bwawa la awali, huku akisisitiza pia upandaji miti katika Mabwawa ambayo yapo kwa jamii na eneo ambalo wananchi wamejengewa nyumba.

Nao baadhi ya wananchi ambao wamejengewa nyumba na Mgodi huo, wameshukuru kujengewa nyumba hizo, na kubainisha kwamba awali walikuwa wakiishi kwenye nyumba za tope, lakini sasa wanakwenda kuishi kwenye nyumba imara za matofari ya saruji ambazo hawakuwa na uwezo wa kuzijenga.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza katika eneo la Bwawa Jipya ya Majitope katika Mgodi wa Almasi Mwadui.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude (kulia) akimsikiliza Mhandisi Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui Shagembe Mipawa.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude (kushoto) akimsikiliza Mhandisi Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui Shagembe Mipawa.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude (kutikati) akimsikiliza Meneja Mahusiano Mgodi wa Almasi Mwadui Benard Mihayo (kushoto).
Kamati ikiendelea na ziara katika Mgodi wa Almasi Mwadui.
Kamati ikiendelea na ziara katika Mgodi wa Almasi Mwadui ikiendelea.
Ziara ikiendelea.
Muonekano wa Bwawa Jipya la kuhifadhia Majitope katika Mgodi wa Almasi Mwadui ambalo kwa sasa ndilo linalotumika.

Muonekano wa Bwawa Jipya la kuhifadhia Majitope katika Mgodi wa Almasi Mwadui.
Muonekano wa Bwawa Jipya la kuhifadhia Majitope katika Mgodi wa Almasi Mwadui.
Muonekano wa Bwawa Jipya la kuhifadhia Majitope katika Mgodi wa Almasi Mwadui. 
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akikagua Nyumba za Waathirika wa Majitope Bwawa la Mgodi wa Almasi Mwadui.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akiendelea na ukaguzi wa Nyumba za Waathirika wa Majitope Bwawa la Mgodi wa Almasi Mwadui.
Muonekano wa Nyumba ambazo wamejengewa Waathirika wa Majitope na Mgodi wa Almasi Mwadui.
Muonekano wa Nyumba.
Muonekano wa Nyumba.
Muonekano wa Nyumba.
Muonekano wa Nyumba.

Post a Comment

0 Comments