MTINDO WA MAISHA UMETAJWA KUCHANGIA MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA,UKIWAMO UNYWAJI WA POMBE

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

AFISA Muuguzi Kitengo cha Magonjwa yasiyo ya kuambukiza Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Shirida Madanka, amesema tatizo ambalo limekuwa likichangia wananchi kuugua Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kikiwamo Kisukari, na Shinikizo la damu(Presha), linatokana na mfumo wa Mtindo wa maisha wa Binadamu usiofaa.

Amebainisha hayo leo Novemba 15, 2023, wakati akiongea na Waandishi wa habari ambao walifika katika hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, kuona namna zoezi linaloendelea la wiki ya upimaji bure Magonjwa yasiyo ya kuambukiza, ambalo lilianza Jumatatu na litahitimishwa siku ya Ijumaa, na baada ya hapo litaendelea katika huduma za kawaida.
Amesema mtindo huo wa maisha usiofaa unatokana na watu kula vyakula vyenye chumvi nyingi,wanga,mafuta, na unyawaji wa pombe, pamoja na kujenga tabia ya kutofanya mazoezi ya mara kwa mara na kupima Afya.

“Huduma hii ya upimaji Magonjwa yasiyo ya kuambukiza tunaitoa bure, na tunaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kuja kucheki Afya zao na kupata ushauri kutoka kwa Wataalamu na wale ambao watakutwa na matatizo waanze Kliniki ya matibabu sababu katika Hospitalii tuna Madaktari Bingwa,”amesema Madanka.
Naye Daktari Emmanuel Sadiki ambaye ni Mtaalamu wa Magonjwa ya Ndani kutoka Hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, amesema ndani ya Siku tatu tangu waanze zoezi hilo la upimaji wa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza wameshapima watu 220.

Amesema katika Idadi hiyo ya watu 220, ambao wamejitokeza kwa wingi ni watu wazima, na tatizo kubwa ambalo kuwa kinara ni ugonjwa wa Shinikizo la damu ambapo Kati ya watu hao 220 waliopatikana na Shinikizo la damu ni 87 sawa na asilimia 37, Kisukari 17 sawa na asilimia 7 na kutoa wito kwa wananchi wajenge tabia ya kupima Afya zao mara kwa mara na kuepuka mtindo wa maisha usiofaa.
Nao baadhi ya wananchi ambao wamejitokeza kupima Afya zao akiwamo Ngusa Kunyanyuki kutoka Shinyanga vijijini, amesema ameamua kupima Afya yake ili apate kujijua pamoja na kupata ushauri kutoka kwa Wataalamu wa Afya.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Afisa Muuguzi kitengo cha Magonjwa yasiyo ya kuambukiza Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Shirida Madanka, akizungumzia zoezi la upimaji Magonjwa hayo ambalo linaendelea katika Hospitali hiyo.
Daktari Emmanuel Sadiki ambaye ni Mtaalamu wa Magonjwa ya Ndani akizungumza kwenye zoezi upimaji Magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Mwananchi Ngussa Kunyanyuki ambaye amejitokeza kupima Afya yake katika Zoezi la upimaji Magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Mwananchi Japhet Ngussa akielezea namna aliyofurahishwa na zoezi hilo la upimaji bure Magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Madaktari katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga wakiendelea na zoezi la upimaji Magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Zoezi la upimaji Magonjwa yasiyo ya kuambukiza likiendelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Elimu ya kuepukana na mtindo mbovu wa maisha ikiendelea kutolewa ili kuepukana na Magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464