WATOTO 752,877 KUPEWA KINGA TIBA YA DAWA ZA KICHOCHO NA MINYOO YA TUMBO MKOANI SHINYANGA ILI KUWAKINGA NA MARADHI HAYO

WATOTO 752,877 KUPEWA KINGA TIBA YA DAWA ZA KICHOCHO NA MINYOO YA TUMBO MKOANI SHINYANGA ILI KUWAKINGA NA MARADHI HAYO

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MKOA wa Shinyanga unatarajia kutoa Kinga tiba ya dawa za Kichocho na Minyoo ya Tumbo, kwa watoto wenye umri wa miaka 5-14, wapatao 752,877 katika Kampeni ambayo itafanyika Novemba 24 mwaka huu.

Hayo yamebainisha leo Novemba 17, 2023 na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, kwenye kikao cha Uraghabishi kwa ajili ya Maandalizi ya Kampeni hiyo ya kutoa Kinga tiba ya dawa hizo za Kichocho na Minyoo ya Tumbo, kilichofanyika kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Amesema katika Kampeni hiyo ya kutoa Kinga tiba, watoto 286,782 watapewa dawa za Kichocho, na watoto 466,095 dawa za Minyoo ya Tumbo ambapo jumla yao ni 752,877, na kutoa wito kwa wazazi wahamasike ili watoto wao wapate dawa hizo ili kuwakinga dhidi ya Maradhi hayo na kuimarisha Afya zao.

“Ukweli usiopingika kutoa Kinga tiba kwa jamii ni Mkakati Muafaka katika kutokomeza Maradhi na kupunguza Vifo vya Watoto,”amesema Mndeme.
Aidha, amesema Kinga hiyo tiba pia itasaidia kupunguza gharama kubwa ambazo familia na Taifa kwa ujumla ingetumie kutibu Maradhi yatokanayo na Magonjwa hayo yasiyopewa kipaumbele.

Naye Mratibu wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele Mkoa wa Shinyanga Timothy Sosoma, amesema Kampeni hiyo ya utoaji Kinga tiba ya dawa za Kichocho na Minyoo ya Tumbo kwa watoto, itafanyika kwa siku moja ambayo ni Novemba 24 katika shule zote mkoani humo.
Amesema katika Mkoa wa Shinyanga tatizo hilo lipo kwa watoto kuugua Kichocho na Minyoo ya Tumbo, kutokana na kupenda kuogelea kwenye Madimbwi ya Maji na Majaruba ya Mpunga hasa katika kipindi hiki cha msimu wa mvua.

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Faustine Mlyutu, amesisitiza utoaji elimu kwa wazazi juu ya kuwapatia watoto wao Kinga tiba ya dawa hizo, pamoja na dawa zifike kwa wakati eneo husika siku ya kuwapatia watoto ili zoezi hilo lipate kufanikiwa kwa malengo ambayo wamejiwekea.
Faustine Mlyutu.
Gaspar Manana kutoka NIMR akizungumzia Kampeni hiyo ya Kinga tiba ya dawa za Kichocho na Minyoo ya Tumbo kwa watoto.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464