Na Marco Maduhu, SHINYANGA
WAKALA wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga, Wizara ya Maji na Fedha,wametoa mafunzo kwa vyombo vya watoa huduma ya maji ngazi ya jamii (CBWSOs), namna ya kukusanya mapato fedha za Ankra za maji kutoka kwenye malipo ya kawaida kwenda mfumo wa Kielektroniki kwa kutumia namba ya malipo (Control Namba) GePG.
Mafunzo hayo yameanza kutolewa leo Novemba 20,2023 kwa vyombo vya watoa huduma ya maji ngazi ya jamii (CBWSOs),kutoka wilaya zote za Mkoa wa Shinyanga ambayo yatachukua muda wa siku 10, namna ya kuhamisha taarifa za vyombo hivyo kwenda kwenye mfumo wa malipo ya Ankra za maji kwa njia ya kielektroniki (GePG) kwa kutumia Control namba.
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Juliety Payovela, awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi kufungua mafunzo hayo, amesema mfumo huo wa malipo ya Ankra za maji kwa kutumia Control namba utasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza ukusanyaji wa mapato mengi ya mauzo ya maji.
“Kupitia mfumo huu makusanyo ya fedha utaongezeka ukiangalia kila Robo CBWSO hua zinaingiza kiasi cha fedha Sh.milioni 500, hivyo Ankra za Maji zikianza kulipwa kwa Control namba mapato yatakuwa mengi, na mara baada ya mafunzo haya kumalizika mfumo huu utaanza kutumika na hakuna tena malipo ya fedha Mkononi,”amesema Mhandisi Payovela.
Mratibu mambo ya fedha kwa CBWSOs Tanzania Adam Mzengi, amesema malipo hayo ya Ankra za Maji yakikusanya vizuri kwa mfumo huo wa Control namba mapato yataongezeka, na hata RUWASA kuendelea kutekeleza miradi mingi ya maji na kumtua Ndoo kichwani Mwanamke sababu fedha zipo.
Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Dafroza Ndalichako akifungua Mafunzo hayo kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Prof; Siza Tumbo, amesema kupitia mafunzo hayo hatarajii kupelekewa kesi kwamba kiongozi wa CBWSO amekusanya fedha za maji kinyume na mfumo huo mpya wa Control Namba.
“Kila Chombo (CBWSO) kihakikishe taarifa za wateja wote zinaingizwa kwenye mfumo huu mpya wa malipo ya Ankra za maji kwa Control namba kwa usahihi, kinyume na hivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watumishi wasio waadilifu, sababu kufanya ubadhilifu wa fedha ni kosa la uhujumu uchumi,”amesema Ndalichako.
Ameongeza kuwa “Fedha hizo ni fedha za umma na ikitokea umezitumia vibaya bila kufuata taratibu za matumizi ya fedha za umma utawajibishwa, na naomba niwaambie kuwa katika hili serikali ya Mkoa iko makini sana, tukikubaini unatumia vibaya fedha za umma hatutakuacha salama, kwani chombo chenu kipo kisheria, kwa mujibu wa sheria ya maji namba 5 ya mwaka 2019.”
Nao baadhi ya Washiri wa Mafunzo hayo akiwamo Kubini Masalu kutoka CBWSO ya Kahama, amesema mfumo huo wa malipo ya Ankra za maji kwa Control namba utawaongezea ufanisi wa utendaji kazi pamoja na wateja kulipa Ankra zao kwa wakati pamoja na kulimarisha usalama wao kwa kutotembea na fedha mkononi bali zitakwenda benki moja kwa moja.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Dafroza Ndalichako akifungua mafunzo hayo kwaniaba ya RAS Prof; Siza Tumbo.
Meneja RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Juliety Payovela akiungumza kwenye mafunzo hayo.
Mratibu na Msimamizi wa Mfumo wa Maji kutoka Wizara ya Maji Mhandisi Masoud Almasi akizungumza kwenye Mafunzo hayo.
Mratibu wa Fedha kwa Vyombo Vya Utoaji Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii (CBWSOs) Tanzania, Adam Mzengi akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo.
Mratibu wa Uingizaji Vyombo vya Watumiaji Maji Ngazi ya Jamii (CBWSO) RUWASA Makao Makuu Dodoma, George Busunzu akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo.
Mshiriki wa mafunzo Kubini Masalu kutoka CBWSO ya Kahama akielezea umuhimu wa mafunzo hayo katika ukusanyaji wa Ankra za maji kwa mfumo wa Control Namba.
Viongozi wa RUWASA wakiwa katika Mafunzo hayo.
Washiriki wakiwa kwenye ufunguzi wa mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye ufunguzi wa mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye ufunguzi wa mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye ufunguzi wa mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye ufunguzi wa mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye ufunguzi wa mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye ufunguzi wa mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye ufunguzi wa mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye ufunguzi wa mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye ufunguzi wa mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye ufunguzi wa mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye ufunguzi wa mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye ufunguzi wa mafunzo..
Washiriki wakiwa kwenye ufunguzi wa mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye ufunguzi wa mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye ufunguzi wa mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye ufunguzi wa mafunzo.