Header Ads Widget

SERIKALI KISHAPU YARIDHISHWA NA MIRADI INAYOTEKELEZWA NA TCRS KUBADILISHA MAISHA YA WANANCHI KIUCHUMI

SERIKALI KISHAPU YARIDHISHWA NA MIRADI INAYOTEKELEZWA NA TCRS KUBADILISHA MAISHA YA WANANCHI KIUCHUMI

Na Marco Maduhu,KISHAPU

SERIKALI wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, imeridhishwa na Miradi ya Maendeleo ambayo inatekelezwa na Shirika la Tanganyika Christian Refugee Service (TCRS) kwa wananchi wilayani humo na kuwainua kiuchumi.

Shirika hilo la TCRS kwa ufadhili wa shirika la Kimataifa la Norwegian Church Aid (NCA) linatekeleza mradi wa Kilimo Stahimilivu Mabadiliko ya Tabia Nchi na Kukuza Uchumi (Climate Smart Economic Empowerment) cha Mboga Mboga na ufugaji kuku chotara, ili kuongeza Usalama wa Chakula, kupunguza njaa na kukuza kipato, katika Kata Mbili za Mondo na Sekebugolo wilayani Kishapu.
Kiongozi wa Mradi kutoka TCRS Dkt.Oscar Rutenge, awali akielezea mradi huo amesema ulianza mwaka 2020, kwamba wamekuwa wakitoa elimu kwa wananchi wa Kata hizo mbili kwa kuwapatia mafunzo kupitia vikundi, namna ya Kulima kilimo cha umwagiliaji kwa njia ya matone na ufugaji wa kuku chotara aina ya sasso.

Amesema pia tangu mwezi Julai 2023, TCRS imekuwa kitekeleza mradi kama huo katika Kata ya Mwalukwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, na wamefikisha vikundi 27 katika wilaya zote mbili, na kueleza kuwa mbali na mafunzo hayo wamekuwa wakiwawezesha wananchi kuwanunulia mifumo ya kisasa kwa ajili ya Kilimo cha umwagiliaji kwa njia ya matone, kuwapa mbegu bora za bustani na vifaranga vya kuku chotara.
“TCRS tumeamua kufanya ziara hii na viongozi wa Serikali wilayani Kishapu, kutembelea miradi ambayo tumekuwa tukiitekeleza kwa wananchi ili wajionee wenyewe mafanikio ambayo wamepata, na tunapoandika taarifa zetu kwao wawe na uhakika nazo sababu wamefika eneo la mradi (field) na kujionea kwa macho,”amesema Dkt. Rutenge.

Aidha, amesema katika utekelazaji wa mradi huo ambao unaisha mwakani (2024),wamekuwa wakishirikiana na Watalaamu wa Serikali kuutekeleza wakiwamo Maofisa Kilimo, Mifugo na Maendeleo ya Jamii, ambao ndiyo wamekuwa wakitoa elimu kwa wananchi.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Joseph Swalala, ambaye alikuwa kiongozi wa msafara kutembelea miradi hiyo ya TCRS akiwa na Watalaamu mbalimbali wakiwamo Maofisa Kilimo, Mifugo na Umwagiliaji, amelipongeza Shirika hilo kwa mradi mzuri na kuwainua wananchi kiuchumi.

Amesema yeye pamoja na Wataalamu wenzake kutoka Halmashauri ya Kishapu, wamejionea namna wananchi wanavyofanya Kilimo cha Umwangiliaji kwa njia ya Matone na Ufugaji wa kuku chotara, pamoja na mafaniko ambayo wamepata ikiwamo ujenzi wa Nyumba za kisasa, kununua Viwanja na kuweza kumudu mahitaji mengine muhimu kwa ustawi wa familia.
Ametoa wito kwa wananchi kuwa miradi hiyo waifanye kuwa ni yao na siyo kusema ya TCRS ili wafadhili hao watakapo maliza muda wao mwakani,waweze kujisimamia na kuitekeleza wenyewe na kuendelea kujiimarisha kiuchumi, na siyo wafadhili wakiondoka wanarudi kwenye umaskini.

Afisa Umwagiliaji Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mwinula Mtwangi, amesema Kilimo ambacho ni cha uhakika kwa sasa ni Kilimo cha Umwagiliaji, na kuwashauri wananchi ambao wamepata elimu hiyo kuwa mashamba hayo yawe darasa la kutoa elimu kwa wenzao.
Diwani wa Kata ya Sekebugolo Frednand Mpogomi, amewashukuru wadau hao kutoka TCRS kwa kutekeleza mradi huo kwa wananchi ambao imewainua kiuchumi, na kuahidi kuendelea kuwapatia ushirikiano.

Nao baadhi ya wanufaika wa mradi huo kutoka TCRS, wamesema kwa sasa maisha yao yamebadilika kiuchumi, huku wengine wakitoa ushuhuda wa kununua Viwanja, Ng’ombe, kujenga Nyumba imara na kutoka kuishi kwenye nyumba za Tembe, pamoja na kupata fedha za kukidhi mahitaji ya familia zao.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Kiongozi wa Mradi kutoka TCRS Dkt.Oscar Rutenge akizungumza katika Ziara hiyo ya Viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu.
Afisa Mifugo Kata ya Sekebugolo Frank Lunyembeleka ambaye anafanya kazi na TCRS akielezea namna wanavyotekeleza mradi katika ziara hiyo ya viongozi wiayani Kishapu kutembelea miradi ya TCRS kuona namna wanavyoitekeleza kwa jamii.
Diwani wa Sekobungolo Frednand Mpogomi akipongeza miradi ya TCRS ambayo inatekelezwa kwa wananchi na kuinua kiuchumi kupitia ufugaji wa Kuku Chotara, na Kilimo cha Mboga kwa njia ya matone.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Joseph Swalala, akizungumza mara baada ya kujionea miradi ya TCRS namna inavyotekelezwa kwa wananchi.
Awali Katibu wa kikundi cha Msimamo Hamis Jilala akisoma taarifa ya kikundi hicho na mafanikio ambayo wameyapata kupitia mradi wa TCRS.
Wanakikundi wakiendelea kusoma risala za mafaniko ambayo wamepata kupitia Mradi wa TCRS.
Katibu wa kikundi cha Shirikisho Yustina Lucas akisoma taarifa ya kikundi hicho na mafanikio ambayo wameyapata kupitia mradi wa TCRS.
Katibu wa kikundi wa Shirikisho katika Kijiji cha Wishiteleja wilayani Kishapu Yustina Lucas, akionyesha nyumba yake ambayo ameipata kupitia mradi wa TCRS wa Kilimo cha Mboga,Ufugaji Kuku Chotara na kucheza hisa.
Viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu na TCRS wakiwa katika nyumba ya Yustina Lucas ambaye ni mmoja wa wanufaika wa Mradi wa TCRS katika kuwainua Wananchi kiuchumi.
Wiliam Ndindi akionyesha Kiwanja ambacho amenunua kupitia Mradi wa TCRS.
Kiongozi wa Mradi kutoka TCRS Dkt.Oscar Rutenge (kulia) akiwa na Mtaalamu wa Kilimo na Mifugo Petro Mathias kwenye mashamba ya Mboga Mboga ya Kilimo cha Umwagiliaji kwa njia ya Matone katika kijiji cha Wishiteleja wilayani Kishapu.
Kiongozi wa Mradi kutoka TCRS Dkt.Oscar Rutenge akionyesha namna maji yanavyopenya kwenye mimea kupitia Kilimo cha Umwagiliaji kwa njia ya Matone.
Afisa Kilimo wilayani Kishapu Richard Mangua akiangalia zao la Nyanya ambalo limelimwa kupitia Kilimo cha Umwagiliaji wa njia ya Matone.
Ziara ya kuangalia miradi ya TCRS ambayo imetekelezwa kwa wananchi kupitai Kilimo cha Mboga Mboga kwa njia ya Matone katika Kijiji cha Wishiteleja Kata ya Mondo wilayani Kishapu.
Afisa Umwagiliaji Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mwinula Mtwangi akiangalia namna maji yanavyopenya kwenye mmea kupitia Kilimo cha Umwagiliaji wa njia ya Matone.
Muonekano wa Shamba la Nyanya ambalo limelimwa kupitia Kilimo cha Umwagiliaji kwa njia ya Matone.

Ziara ya kuangalia miradi ya TCRS ambayo imetekelezwa kwa wananchi kupitai Kilimo cha Mboga Mboga kwa njia ya Matone katika Kijiji cha Wishiteleja Kata ya Mondo wilayani Kishapu.
Tangi la Maji ambalo linatumika kuhifadhia maji kwa ajili ya Kilimo cha Umwagiliaji wa njia ya Matone
iara ya kuangalia miradi ya TCRS ambayo imetekelezwa kwa wananchi kupitai Kilimo cha Mboga Mboga kwa njia ya Matone katika Kijiji cha Wishiteleja Kata ya Mondo wilayani Kishapu.
iara ya kuangalia miradi ya TCRS ambayo imetekelezwa kwa wananchi kupitai Kilimo cha Mboga Mboga kwa njia ya Matone katika Kijiji cha Dulisi Kata ya Sekebugolo wilayani Kishapu.
Viongozi wakiangalia Shamba la Vitunguu katika Kijiji cha Dulisi wilayani Kishapu ambalo limelimwa kupitia Kilimo cha Umwagiliaji kwa njia ya Matone
Viongozi wakiangalia Shamba la Vitunguu katika Kijiji cha Dulisi wilayani Kishapu ambalo limelimwa kupitia Kilimo cha Umwagiliaji kwa njia ya Matone
Muonekano wa Shamba la Vitunguu katika Kijiji cha Dulisi Kata ya Sekebugolo wilayani Kishapu.
Muonekano wa Shamba la Vitunguu katika Kijiji cha Dulisi Kata ya Sekebugolo wilayani Kishapu.
Muonekano wa Shamba la Vitunguu katika Kijiji cha Dulisi Kata ya Sekebugolo wilayani Kishapu.
Ziara ikiendelea katika Mashamba ya Vitunguu katika Kijiji cha Dulisi kupitia Kilimo cha Umwagiliaji wa njia ya Matone.

Viongozi wa halmashauri wakiangalia Shamba la Nyanya katika Kijiji cha Dulisi wilayani Kishapu ambalo limelimwa kupitia Kilimo cha Umwagiliaji kwa njia ya Matone
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmshauri ya wilaya ya Kishapu Joseph Swalala akiangalia Shamba la Nyanya katika Kijiji cha Dulisi wilayani Kishapu ambalo limelimwa kupitia Kilimo cha Umwagiliaji kwa njia ya Matone
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmshauri ya wilaya ya Kishapu Joseph Swalala, akiwa na Wataalamu wengine wa Halmashauri wakiangalia Shamba la Nyanya katika Kijiji cha Dulisi wilayani Kishapu ambalo limelimwa kupitia Kilimo cha Umwagiliaji kwa njia ya Matone

Muonekano wa Shamba la Nyanya katika Kijiji cha Dulisi ambalo limelimwa kupitia Kilimo cha Umwagiliaji kwa njia ya Matone.
Wataalamu wa Halmashauri wilayani Kishapu wakiendelea kuangalia Shamba la Nyanya ambalo limelimwa kupitia Kilimo cha Umwagiliaji kwa njia ya Matone.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmshauri ya wilaya ya Kishapu Joseph Swalala, akiwa na Wataalamu wengine wa Halmashauri wakiangalia Shamba la Nyanya katika Kijiji cha Dulisi wilayani Kishapu ambalo limelimwa kupitia Kilimo cha Umwagiliaji kwa njia ya Matone
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmshauri ya wilaya ya Kishapu Joseph Swalala, akiwa na Wataalamu wengine wa Halmashauri wakiangalia Shamba la Nyanya katika Kijiji cha Dulisi wilayani Kishapu ambalo limelimwa kupitia Kilimo cha Umwagiliaji kwa njia ya Matone.
Muonekano wa Shamba la Nyanya katika Kijiji cha Dulisi ambalo limelimwa kupitia Kilimo cha Umwagiliaji kwa njia ya Matone.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmshauri ya wilaya ya Kishapu Joseph Swalala, akiwa na Wataalamu wengine wa Halmashauri wakiangalia Shamba la Nyanya katika Kijiji cha Dulisi wilayani Kishapu ambalo limelimwa kupitia Kilimo cha Umwagiliaji kwa njia ya Matone
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmshauri ya wilaya ya Kishapu Joseph Swalala, akiwa na Wataalamu wengine wa Halmashauri wakiangalia Shamba la Nyanya katika Kijiji cha Dulisi wilayani Kishapu ambalo limelimwa kupitia Kilimo cha Umwagiliaji kwa njia ya Matone.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmshauri ya wilaya ya Kishapu Joseph Swalala, akiwa na Wataalamu wengine wa Halmashauri wakiangalia Shamba la Nyanya katika Kijiji cha Dulisi wilayani Kishapu ambalo limelimwa kupitia Kilimo cha Umwagiliaji kwa njia ya Matone.
Wataalamu wa Halmshauri ya wilaya ya Kishapu wakiwa katika Kaya ya Pius Mungo wakiangalia ufugaji wa Kuku Chotara kupitia Mradi wa TCRS.
Muonekano wa Kuku Chotara.
Wataalamu wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Awali wakisikiliza Mafanikio ambayo wamepata wananchi kupitia Mradi wa TCRS katika Kijiji cha Wishiteleja wilayaniu Kishapu.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Joseph Swalala akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya Wananchi wa Kijiji cha Wishiteleja jinsi walivyofanikiwa kiuchumi kupitia Mradi wa TCRS.
Wanavikundi mbalimbali wakiwa kwenye kikao na viongozi wa Serikali Halmashauri ya wilaya ya Kishapu wakielezea mafanikio ambayo wameyapata kupitia Mradi wa TCRS.

Ziara ya viongozi wa Halamashauri ya wilaya Kishapu wakiwa katika ziara ya kutembelea miradi ya Kilimo cha Umwagiliaji kwa njia ya Matone na Ufugaji Kuku wa Chotara ambayo inatekelezwa na TCRS kwa Wananchi kupitia Vikundi ili kujionea uhalisia wa Miradi hiyo.

Post a Comment

0 Comments