WAZIRI WA MADINI ANTHONY MAVUNDE APONGEZA JUKWAA LA UZIDUAJI LA HAKIRASILIMALI,ATAJA MIKAKATI YA WIZARA IFIKAPO 2030
Na Marco Maduhu, DODOMA
WAZIRI wa Madini Anthony Mavunde, ameipongeza Taasisi ya HakiRasilimali kwa kuandaa Jukwaa la Sekta ya Uziduaji ambalo wamejadili masuala mbalimbali ya Nishati na Madini kwa ajili ya ukuaji wa uchumi wa nchi na maendeleo endelevu, huku akitaja mikakati ya Wizara katika kuikuza Sekta ya Madini kiuchumi ifikapo 2030 kwa kuwekeza kwanza kwenye utafiti.
Amebainisha hayo leo Novemba 10,2023 wakati akihitimisha Jukwaa la Sekta ya Uziduaji yani Madini, Mafuta na Gesi Asilia ambalo limefanyika kwa muda wa siku mbili Jijini Dodoma lililoandaliwa na Taasisi ya HakiRasilimali.
Amesema anashukuru Taasisi hiyo ya HakiRasilimali kwa kuandaa Jukwaa hilo la Uziduaji, ambalo wadau wamejadili mambo mbalimbali ya msingi hasa katika Sekta ya Nishati na Madini, kwa ajili ya kuziendeleza Sekta hizo kwa uchumi wa Taifa na Maendeleo endelevu, sababu Madini ni Maisha na Utajiri.
“Nashukuru HakiRasilimali kwa kuandaa Jukwaa hili la Uziduaji na kujadili masuala mbalimbali hasa katika Sekta hizi mbili za Nishati na Madini hongereni sana kwa kazi nzuri kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu na sisi Serikali tutaendelea kushirikiana pamoja,”amesema Waziri Mavunde.
Aidha, amesema baada ya Rais Samia kumteua kuwa Waziri wa Madini, aliangalia Sekta ya Madini, Sera ya Madini ya mwaka 2009 na kufuata maelekezo ya CCM kupitia Ilani ya uchaguzi, na maelekezo ya viongozi wakubwa akiwamo Mheshimiwa Rais, kuona namna ya kuikuza Sekta hiyo na kuchangia uchumi wanchi kwa kiwango kikubwa.
Amesema wao kama Wizara ya Madini pamoja na viongozi wenzake walikuja na jambo la Vission 2030 yani Madini ni Maisha na Utajiri, na kujiwekea malengo kwamba hadi ifikapo mwaka huo 2030 kwamba nchi ya Tanzania kupitia Sekta ya Madini wawe wamefanya utafiti wa kina wa Madini tuliyonayo ifikie asilimia 50 na kutoka asilimia 16.
“Moja kati ya Changamoto kubwa tuliyonayo hapa Nchini ni kutokuwa na Taarifa sahihi ya Madini tuliyonayo, lhivyo tukaona sehemu ya kwanza ya kuanzia tuanzie hapa, na njia ya pekee ni kuipa nguvu GST ili waweze kuwa na uwezo wa kufanya kazi zake kwa mujibu wa Sheria, na lengo letu ni kuimarisha Kanzidata yetu kupitia utafiti wa 'Georgyical' Sayansi, na kuongoza wadau wa Sekta ya madini vizuri,”amesema Mavunde.
Amesema kama Wizara waliona ni vyema waweke mikakati ya kuhakikisha wanafanya utafiti wa kina na kulifikia eneo kubwa zaidi na kubainisha kuwa kama eneo tu hilo dogo ambalo limefanyiwa utafiti wa kina kuwa linaingizia mapato mengi Serikali Je eneo hilo kubwa itakuwaje ndiyo maana kwa sasa wapo kwenye utafiti ili kupata taarifa sahihi ya madini.
“Eneo hilo dogo tu ambalo limefanyiwa utafiti wa kina limekuwa na mchango mkubwa wa mauzo ya madini nje ya nchi ambapo kwa mwaka wa fedha uliopita yamefikia kiasi cha Dola Bilioni 3.3 sawa na asilimia 56 ya mauzo yote ya bidhaa nje ya nchi, huku Serikali kuu ikikusanya Maduhuli Bilioni 878, na Mapato ya Kodi ya ndani kiasi kilichokusanywa ni Sh.Trilioni 2,”amesema Mavunde.
Aidha, amesema katika mwaka wa fedha uliopita, kupitia biashara ya Masoko ya Madini 42 na Vituo vya kununua Madini 93 kilikusanywa kiasi cha fedha Sh. Trilioni 1.6, na kuona kwamba kumbe wakiongeza nguvu zaidi kwenye eneo la utafiti na kuongeza maeneo ya uzalishaji kwamba nchi ya Tanzania inauwezo wa kupiga hatua kubwa zaidi kiuchumi.
Katika hatua nyingine amezungumzia suala la Wazawa kutoa huduma kwenye Migodi ya Madini (Local Content) kuwa Wizara ya Madini suala hilo imelipa kipaumbele na mwisho wa mwezi huu wanaangalia namna ya kukutana na watoa huduma kwenye Migodi kote nchini ili wajadiliane na kuona namna ya kusaidia Watanzania wengi kushiriki kwenye uchumi huo.
“Aliyepata nafasi kutoa huduma kwenye Migodi hiyo amvute na mwezake na tutatengeneza utaratibu kwenye Migodi yote katika Plan yao ya mwaka mzima na zipo baadhi ya bidhaa ambazo wanaziangiza nje ya nchi sababu sisi hatuna uwezo, lakini tukishapata Plan itakuwa Rahisi kuwa ambia wawawezeshe Watanzania ili bidhaa hizo zizalishwe hapa nchini ili fedha zibaki hapa hapa,”ameongeza Mavunde.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa HakiRasilimali Adam Anthoy, akizungumza awali kabla ya kumkaribisha Waziri wa Madini kufungwa Jukwaa hilo la Uziduaji, amesema katika Jukwaa hilo wamejadili masuala mbalimbali kwa ajili ya mustakabali wan chi kwa maendeleo endelevu, likiwamo pia suala la Uwazi na Uwajibikaji katika Sekta ya Uziduaji.
Aidha, ametaja ambayo yametolewa na wadau katika Jukwa hilo la Uziduaji kwa watunga Sheria na Sera, kwamba Makampuni ya Nje yafanye kazi na Makampuni ya Wazawa kwenye Migodi, kuwepo na Mazingira Rafiki kwa Wawekezaji wakubwa wa Madini na wachimbaji wadogo, kuthibitisha Sekta ya uchimbaji mdogo, mapato ya Sekta ya Uziduaji yawafikie wananchi pamoja na uwazi wa Mikataba.
Jukwa hilo la Uziduaji la HakiRasilimali limefanyika kwa muda wa siku mbili ambalo lilianza Jana Novemba 9 na limehitimishwa leo Novemba 10 ambalo limekutanisha wadau mbalimbali wa Sekta hiyo kutoka Asasi za Kirai, Wawakilishi wa Serikali Kuu, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Makampuni ya Madini, Wachimbaji Wadogo, Wawakilishi kutoka Jamii husika, Wanataaluma na Waandishi wa habari.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Waziri wa Madini Anthony Mavunde akizungumza wakati wa kuhitimisha Jukwaa la Uziduaji la HakiRasilimali.
Mkurugenzi Mtendaji wa HakiRasilimali Adam Anthony akizungumza kwenye Jukwaa la Uziduaji kabla ya kumkaribisha Waziri wa Madini Anthony Mavunde.
Wadau wakiwa kwenye Jukwaa la Sekta ya Uziduaji.
Jukwaa la Sekta ya Uziduaji.
Wadau wakiwa kwenye Jukwaa la Sekta ya Uziduaji.
Wadau wakiwa kwenye Jukwaa la Sekta ya Uziduaji.
Wadau wakiwa kwenye Jukwaa la Sekta ya Uziduaji.
Wadau wakiwa kwenye Jukwaa la Sekta ya Uziduaji.
Wadau wakiwa kwenye Jukwaa la Sekta ya Uziduaji.
Wadau wakiwa kwenye Jukwaa la Sekta ya Uziduaji.
Waziri wa Madini Anthony Mavunde (kushoto) akipiga picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa HakiRasilimali Adam Anthony.
Waziri wa Madini Anthony Mavunde (kushoto) akipiga picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa HakiRasilimali Adam Anthony.
Waziri wa Madini Anthony Mavunde (kulia) akipiga picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya HakiRasilimali Jimmy Luhende.
Waziri wa Madini Anthony Mavunde akipiga picha ya pamoja.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464