MAHAFALI YA 41 MWAKA WA PILI CHUO CHA VETA SHINYANGA YAFANA


MAHAFALI YA 41 MWAKA WA PILI CHUO CHA VETA SHINYANGA YAFANA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MAHAFALI ya 41 ya Mwaka wa Pili katika Chuo cha Ufundi Stad VETA mkoani Shinyanga yamefana, huku wafanyabiashara wakitakiwa kuchangamkia fursa za ujenzi wa hosteli kwa ajili ya kuishi wanafunzi jirani na Chuo hicho, pamoja na kuweka usafari wa Magari(Public Transport)kwa ajili ya kubeba wanafunzi ambao wanaishi mbali na chuo.

Mahafali hayo yamefanyika leo Novemba 24, 2023 katika Chuo hicho na kuhudhuliwa pia na Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Magharibi AsanteRabi Kanza, huku Mgeni Rasmi akiwa ni Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Shinyanga Lucas Mzungu akimwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Alexius Kagunze.
Mkuu wa Chuo cha VETA mkoani Shinyanga Magu Mabelele, akisoma taarifa ya Chuo hicho kwa Mgeni Rasmi, amesema VETA Shinyanga ilianzishwa mwaka 1989 ikiwa na Fani moja ya Ujenzi, na Mwaka 2010 ikaongeza Fani na kufika 10, huku uwezo wa Chuo ni kubeba wanafunzi 400 wa Fani za muda mrefu na sasa wapo 417, za Muda Mfupi wanafunzi 1,000 sasa wapo 1,196,na hivyo kukabiliwa na upungufu wa Madarasa na Hosteli.

“Chuo hiki cha VETA tuna wanafunzi wengi, lakini tunakabiliwa na changamoto ya upungufu wa madarasa, hosteli na hivyo kulazimika baadhi ya wanafunzi kwenda kupanga vyumba mitaani, ukosefu wa huduma za afya kwa wanafunzi, uchakavu wa magari na kusababisha wanafunzi 20 wa fani ya udereva kukosa nafasi sababu hakuna Magari,”amsema Mabelele na kuongeza.
“Tunaziomba Taasisi za Serikali ambazo zina Magari chakavu na hayafanyi kazi watupatie sisi tutayatengeneza na kutumika kufundishia wanafunzi.”

Naye Kaimu Msajili wa Chuo hicho cha VETA Shinyanga Rashid Ntahigye, ametaja changamoto nyingine ambayo inawakabili chuoni hapo kuwa ni kuharibika kwa uzio, na hivyo kusababisha wizi wa mali za chuo, huku akitaja idadi ya fani za muda mrefu ambazo hutolewa chuoni hapo kuwa zipo 10, na fani za muda mfupi zipo 26.

Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Magharibi AsanteRabi Kanza, ametoa wito kwa Wahitimu hao kuwa watapokuwa wameajiriwa au kujiajiri wenyewe wajali ubora wa vitu vyao, uadilifu kazini, wawe wazalendo na nchi yao, na wasiwe chanzo cha matatizo bali kutatua matatizo.
Mwanafunzi Felix Dastani akisoma Risala ya Wahitimu, amesema wamehitimu wanafunzi 129, wavulana 82 na wasichana 47, huku wanafunzi 9 wakishindwa kuhitimu kwa sababu mbalimbali, na kutaja fani ambazo wamehitimu kuwa ni UfundiSelemala, Umeme, Mabomba,Ubinifu, Ushonaji na Mapambo, Ujenzi, uchomeleaji, ukataji na ung’arishaji madini ya Vito.

Ametaja changamoto kubwa ambayo wanakwenda kukabiliana nayo baada ya kuhitimu mafunzo yao, kuwa ni ukosefu wa mitaji kwa ajiri ya kujiajiri wenyewe kwa madai ya ugumu uliopo wa kupata mikopo ya Halmashauri asilimia 4 kwa vijana, na kuiomba Serikali ilegeze masharti ili vijana wapate mikopo na kujiajiri,”amesema Dastani.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Shinyanga Lucas Mzungu, akizunguza katika Mahafali hayo amewataka wahitimu hao waende kuwa daraja la mafanikio, pamoja na changamkia fursa katika miradi ya Serikali ambayo inaendelea kutekelezwa kupitia ‘Local Fundi’ na kujipatia kipato.
“Ninyi wanafunzi mmehitimu mafunzo yenu mkiwa na ujuzi, jiungeni kwenye vikundi na kufungua kampuni zenu za ujenzi na kuzisajili mkija kuomba Zabuni za ujenzi Halmashauri tunawapa kazi, na hivi karibuni tuta tangaza Zabuni ukarabati Madarasa shule ya Sekondari Masekelo, ujenzi wa Maabara Shule ya Sekondari Mwangulumbi Chibe,”amesema Mzungu.

Aidha, amewataka pia wanafunzi hao kupitia vikundi vyao wanaweza pia kuanzisha viwanda vidogo sababu pesa za mitaji zipo asilimia 4 za mikopo ya Halmashauri zile za asilimia 10, pamoja na fedha tu za vijana asilimia 4 ambazo hazina Riba na kuendesha maisha yao kupitia ujuzi walioupata VETA.
“Mafanikio ya Serikali ya Viwanda yanategemea sana vijana kutoka VETA,”ameongeza Mzungu.

Katika hatua nyingine amewataka wafanyabiashara wachangamkie fursa ya ujenzi wa hosteli jirani na chuo hicho cha VETA, pamoja na kuweka usafiri wa HAICE kwa kufanya ‘Root’ za kubeba wanafunzi ambao wanaishi mbali na Chuo, huku akitoa wito pia kwa chuo hicho wakae na Shirika la Nyumba (NHC) na kuingia nao ubia wa kujengewa hosteli za wanafunzi.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mgeni Rasmi Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Shinyanga Lucas Mzungu akizungumza kwenye Mahafali ya VETA.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA Kanda ya Magharibi AsanteRabi Kanza akizungumza kwenye Mahafali.
Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga Magu Mabelele akizungumza kwenye Mahafali hayo.
Kaimu Msajili wa VETA Shinyanga Rashid Ntahigiye akisoma taarifa ya Mafunzo kwenye Mahafali hayo.
Mwanafunzi Felix Dastan akisoma Risala ya wahitimu kwenye Mahafali hayo.
Mazazi Rose Makaranga akizumgumza umuhimu wa kusomesha watoto VETA.
Viongozi Meza Kuu wakiwa kwenye Mahafali VETA.
Mahafali yakiendelea.
Wanafunzi wa Mwaka wa Pili VETA Shinyanga wakiwa kwenye Mahafali yao.
Wanafunzi wa Mwaka wa Pili VETA Shinyanga wakiwa kwenye Mahafali yao.
Wanafunzi wa Mwaka wa Pili VETA Shinyanga wakiwa kwenye Mahafali yao.
Wanafunzi wa Mwaka wa Pili VETA Shinyanga wakiwa kwenye Mahafali yao.
Wanafunzi wa Mwaka wa Pili VETA Shinyanga wakiwa kwenye Mahafali yao.
Wanafunzi wa Mwaka wa Pili VETA Shinyanga wakiwa kwenye Mahafali yao.
Wanafunzi wa Mwaka wa Pili VETA Shinyanga wakiwa kwenye Mahafali yao.
Wanafunzi wa Mwaka wa Pili VETA Shinyanga wakiwa kwenye Mahafali yao.
Wanafunzi wa Mwaka wa Pili VETA Shinyanga wakiwa kwenye Mahafali yao.
Watumishi wa VETA Shinyanga wakiwa kwenye Mahafali.
Watumishi wa VETA Shinyanga wakiwa kwenye Mahafali.
Watumishi wa VETA Shinyanga wakiwa kwenye Mahafali.
Wazazi wakiwa kwenye Mahafali.
Wazazi wakiwa kwenye Mahafali.
Wazazi wakiwa kwenye Mahafali.
Wazazi wakiwa kwenye Mahafali.
Mahafali yakiendelea.
Mgeni Rasmi akitoa vyeti kwa wahitimu.
Zoezi la utoaji vyeti likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti likiendelea.
Wahitimu wakitoa burudani
Burudani zikiendelea.
Burudani zikiendelea.
Burudani zikiendelea.
Burudani zikiendelea.
Mgeni Rasmi akiangalia maonyesho ya ubunifu wa ujenzi wa nyumba na uchoraji wa Ramani
Mgeni rasmi akiangalia ubunifu wa mavazi na ushonaji.
Mgeni Rasmi akiangalia fani ya mapambo na saloon.
Mgeni Rasmi akiangalia fani ya umeme.
Fani ya umeme.
Mgeni Rasmi akiangalia fani ya ukataji na ung'arishaji madini ya Vito na kuyaongeza thamani.
Madini ya Vito.
Picha za pamoja zikipigwa katika Mahafali hayo.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Mgeni Rasmi awali akiwasili kwenye Mahafali katika Chuo cha VETA Shinyanga.
Wahitimu wakiingia ukumbini.
Wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464