RAS SHINYANGA AFUNGUA KIKAO CHA VYAMA VIKUU VYA USHIRIKA NA WARAJIS WASAIDIZI WA MIKOA
Na. Shinyanga RS.
KATIBU Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza D. Tumbo amefungua kikao cha vyama vya ushirika na warajisi wasaidizi wa mikoa ya kanda ya ziwa na baadhi ya mikoa ya singida na Tabora chenye lengo la kuhabarishana juu ya kuanza kwa matumizi ya Mfumo wa Stakabadhi Ghalani huku akiwasisitiza kwenda kuwa wazalendo katika utekelezaji wa mfumo huu ili ulete tija kama serikali ilivyokusudia.
Prof. Tumbo amesema kuwa, serikali hii ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yeye mwenyewe Mhe. Rais ameamua kurejesha mfumo huu kwetu ili sasa unufaishe vema pande zote, na kwamba kinachotakiwa kwa viomgozi hawa sasa ni kwenda kuutndea haki katika maeneo yao.
"Niwaagize viongozi wote wa Muungano wa Vyama vya Msingi vya Ushirika kwenda kutanguliza uzalendo, weledi na umakini zaidi katika kutekeleza mfumo huu wa stakabadhi ghalani ili ulete tija kwa pande zote kama ambavyo serikali ioivyokuwa na nia njema na wananchi wake kupitia ninyi," alisema Prof. Tumbo.
Kwa upande wake Mrajis Msaidizi Mkoa wa Shinyanga Ni. Hilda Boniphace ambaye pia katika kikao cha leo alikuwa Mwenyekiti aliwakumhusha washiriki kwenda kuanza maandalizi hivi sasa ya namna bora ya utumiaji wa mfumo huu, huku akiwasisitiza kwenda kushirikisha makundi yote muhimu katika kuwapatia elimu na taarifa ili wakati utakapofika iwe rahisi katika utekelezaji wake.
Nao washiriki wa kikao hiki kwa kauli moja wameazimia kwenda kusimamia yale yote waliyokubaliana ili kuleta tija kwao na kwa nyingine za wadau kama ambavyo serikali imekusudia.
Katika kikao hiki pia kimehudhuriwa na Augustino Mbulumi ambaye ni Meneja Uendeshaji Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), Witness Temba Afisa Udhibiyi Ubora kutoka Bodi ya Usimamizi wa Stajabadhi za Ghala Tanzania na Robert Nsunza kutoka Masoko na Uwekezaji Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania.
Stakabadhi ghalani ina lengo la kumsaidia mkulima kuuza zao lake kwa bei ya soko, uhakika wa soko, uhakika wa kuhifadhi zao lake na ushindani kulingana na hali ya soko, kujuwa hali ya soko kidigitali.