waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wanaotekeleza mradi wa ukarabati wa uwanja wa ndege
Suzy Luhende Shinyanga press blog
Waandishi wa habari Mkoani Shinyanga wametembelea mradi wa ukarabati wa uwanja wa ndege unaoendelea katika kata ya Ibadakuli manispaa ya Shinyanga, ambao utatumia zaidi ya Sh bilioni 44.8. ikiwa kwa sasa umefikia asilimia 6.5.
Waandishi wa habari walitembelea mradi huo kwa lengo la kujionea na kujua nini kinaendelea na wamefikia hatua gani mpaka sasa, ambapo pia walizungumza na baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Shinyanga .
Ambapo pia wananchi hao wamesema mradi wa uwanja wa ndege utakapokamilika utaongeza fursa nyingi kwa wakazi wa Shinyanga, ambapo wataagiza mizigo ya biashara itafika kwa wakati, pia itaongeza watalii wengi kwa sababu Mkoa wa Shinyanga una madini.
Joseph Mwandu mkazi wa manispaa ya Shinyanga amesema anaishukuru serikali kwa kuikumbuka Shinyanga na na kutoa fedha za kukarabati uwanja wa ndege kwani fursa nyingi zilipotea, lakini kwa kuanza ukarabati huo wananchi wameanza kuona matumaini mapya, watu watapata fursa mbalimbali.
"Tunaishukuru sana serikali ya mama Samia Suluhu kwa kutukumbuka sisi wanashinyanga sisi wafanyabiashara tulikuwa tunatumia gharama kubwa sana kwenda Mwanza kwa ajili yakupanda ndege na wakati mwingine tulikuwa tukipata hasara tunapochelewa na kukuta ndege imeshaondoka"amesema Charles Masasy
Airine Charles Mkazi wa wilaya ya Kishapu Mkoa wa Shinyanga amesema hivi karibuni alikuwa anasafiri kuelekea Dar na tayari alikuwa amekata tiketi ya Ndege Mwanza alitoka Kishapu saa tisa ya usiku kuelekea Mwanza kwa ajili ya kwenda kupanda ndege lakini alichelewa na kukuta ndege hiyo imeshaondoka, hivyo alipata hasara ya fedha ya nauli na alipata hasara ya kukaa hotel kusubiri ndege ya kesho yake.
"Niipongeze sana serikali kwa kujali wananchi na nimpongeze meneja wa Tanroads kwakuendelea kusimamia kikamilifu kazi hii mpaka kufikia asilimia 6.5 na niwaombe waongeze kasi ili tuweze kuondokana na adha hizi"amesema Airine.
Kwa upande wake Meneja wa Tanroads Mkoa wa Shinyanga Mibara Ndirimbi wakati akizungumza na waandishi wa habari wa Mkoa wa Shinyanga waliotembelea uwanja huo amesema ukarabati wa uwanja wa Ndege umefikia asilimia 6.5 ambao mpaka kukamilisha utatumia Sh 44.8 Bilioni na utakapokamilika utawaondolea adha ya kusafiri umbali wa kilomita 1000 na utaongeza fursa kwa wananchi wa Shinyanga.
" Kufikia Decemba 5 mwaka huu
tulitakiwa tuwe tumeshafikia asilimia 9.5 lakini kutokana na changamoto ya mvua kufikia Decemba 5. 2023 tutafikia asilimia 6.5 na mambo mengine tayari kilichobaki ni Rea ya rami, sehemu zilizokuwa zinasumbua kilomita moja imeshakamilika mpaka kiliomita 2 .2 wameongeza mita 200,amesema Ndirimbi.
"Kuwepo kwa uwanja huu kutakuwa na fursa nyingi ambazo zitaufanya mji wa Shinyanga uchangamke,kutakuwa na hotel, mama ntilie, kutakuwa na Tax wafanyabiashara watajiongezea kipato, toka hapa kwenda Dar es salaam ni masaa 14 kwa usafiri wa kawaida, lakini kwa kutumia ndege ni saa moja na nusu tu kwa bombadier mtu atafika na kufanya kazi zake Dar na kurudi Shinyanga"ameongeza Ndirimbi.
Naye Mhandisi mshauri wa mradi wa uwanja huo Sosthenes John Lowe amesema uwanja huo umeboreshwa zaidi kwa ajili ya ndege kubwa, hivyo utakuwa ni uwanja mkubwa ambao utatumiwa na ndege bombadier Q4100
Kwa upande wake mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru amesema baada ya waandishi wa habari kujionea kinachoendelea watawafahamisha wananchi kupitia vyombo vyao vya habari ili kujua hatua zitakazoendelea.
Meneneja wa Tanroads Mkoa wa Shinyanga Mibara Ndirimbi akizungumza na waandishi wa habari
Meneneja wa Tanroads Mkoa wa Shinyanga Mibara Ndirimbi akizungumza na waandishi wa habariViongozi wa klabu ya Shinyanga press wakiwa kwenye picha ya pamoja na meneja wa Tanroads Mkoa wa Shinyanga Mkandarasi anaetekeleza mradi huo na mhandisi mshauri wa mradi huo
Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wanaotekeleza mradi wa ukarabati wa uwanja wa ndege
Kazi ikiendelea katikauwanja wa ndege Ibadakuli manispaa ya Shinyanga
Wandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga wakimsikiliza meneja wa Tanroads Mkoa wa Shinyanga Mibara Ndirimbi akiwaeleza jinsi uwanja huo unavyoendelea na ukarabati
Kazi ikiendelea
Mhandisi mshauri wa mradi wa uwanja huo Sosthenes John Lowe akizungumza na waandishi wa habari
Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wanaotekeleza mradi wa ukarabati wa uwanja wa ndege
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464