VIONGOZI WA SENET YA VYUO NA VYUO VIKUU MKOA WA SHINYANGA 'UVCCM' WATINGA NA TELA LA PUNDA CHUO CHA SANYANSI ZA AFYA KOLANDOTO

VIONGOZI WA SENET YA VYUO NA VYUO VIKUU MKOA WA SHINYANGA 'UVCCM' WATINGA NA TELA LA PUNDA CHUO CHA SANYANSI ZA AFYA KOLANDOTO

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

VIONGOZI wa Senet ya vyuo na vyuo vikuu Mkoa wa Shinyanga wa Umoja wa Vijana (UVCCM), wamefanya ziara katika Chuo Cha Sayansi za Afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga, kutoa elimu ya Itikadi kwa Wanachama wa Senet pamoja na kuwapatia Kadi za CCM.

Ziara hiyo Imefanyika leo Novemba 18,2023 ikiongozwa na Mwenyekiti wa Senet Said Sultan ambayo iliendana sambamba na kuhamasisha kuongeza idadi ya Wanachama wapya,ili kuendelea kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Jumuiya zake.
Sultan akizungumza na Wanachama wa Senet katika Chuo hicho cha Sanyansi za Afya Kolandoto, amesema katika Mkoa wa Shinyanga wana Matawi 13 ya Senet, pamoja na mambo mengine wamekuwa wakitoa elimu Itikadi, Imani ya CCM, na ahadi Tisa za CCM, ili kuwajenga Vijana kuwa Wazalendo na Nchi yao.

Katika hatua nyingine Sultan amempongeza Rais Samia kwa kuridhia utoaji wa mikopo katika vyuo vya kati, hali ambayo imesaidia wanafunzi ambao Kaya zao hazina uwezo wa kuwasomesha vyuo wamepata  fursa ya kusoma na kutimiza ndoto zao na hata kuja kuwa viongozi wa Taifa hili.
"Dicemba 2 mwaka huu tutaandaa Kongamano la Asante Mama hapa Mkoani Shinyanga na Mgeni Rasmi tunatarajia awe Katibu wa NEC, Itikadi, Siasa na Uenezi Paulo Makonda, Rais wetu Samia amefanya Mambo makubwa ikiwamo Sekta ya Elimu," amesema Sultan.

Naye Mwenyekiti Mstaafu wa Senet kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Pius Mwandu, akitoa elimu ya Itikadi kwa kuanza na Imani ya CCM,amesema kuwa Imani ya CCM ni kujenga ujamaa, kuishi kwa usawa na kwamba binadamu wote ni sawa.
Akizungumzia ahadi Tisa za CCM ili kuwafanya vijana kuwa wazalendo na nchi yao, amesema zinaeleza kuwa Binadamu ni Ndugu wa Afrika Moja, kutumikia nchi kwa watu wote, kujitolea nafsi kuondosha umaskini, ujinga, na dhuruma.

Ametaka zingine kuwa Rushwa ni Adui wa haki, Cheo ni dhamana na kutokitumia kwa faida binafsi, kujitoa kwa elimu kwa faida ya watu wote, kushirikiana na watu wengine kujenga nchi, kusema ukweli fitina ni mwiko, pamoja na kuwa Mwanachama wa CCM na Raia Mwema.
Pia ametoa wito kwa viongozi wa Senet vyuoni kuyasema mambo mazuri ambayo yamefanywa na Rais Samia na kuliletea Maendeleo taifa katika Sekta mbalimbali ikiwamo ya elimu.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Sanyansi za Afya Kolandoto Paschal Shiluka ambaye ndiye mlezi wa Senet Chuoni hapo, amepongeza ziara hiyo huku akisema kuwa wao kama vyuo vya mafunzo wanaunga juhudi za Rais Samia katika utendaji wake kazi na Chama Cha CCM sababu wao ndiyo wanashika dola.
Mwenyekiti wa Senet ya vyuo na vyuo vikuu Mkoa wa Shinyanga kupitia UVCCM Said Sultan akizungumza kwenye Mkutano wa Senet katika Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto.
Mwenyekiti wa Senet ya vyuo na vyuo vikuu Mkoa wa Shinyanga kupitia UVCCM Said Sultan akizungumza kwenye Mkutano wa Senet katika Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto.
Katibu wa Senet Mkoa Masunga Mazoya akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mwenyekiti Msaafu wa Senet kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam Pius Mwandu akitoa elimu ya Itikadi kwenye Mkutano huo.
Mkuu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Paschal Shiluka ambaye ni mlezi wa Senet chuoni hapo katizugumza kwenye Mkutano huo.
Mwenyekiti wa Senet Tawi la Chuo cha Kolandoto Luge Deus akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mwenyekiti wa Senet Said Sultan (kulia) akiteta Jambo na Katibu wa Senet Masunga Mazoya wakiteta Jambo kwenye Mkutano huo.
Wanachama wa Senet Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto wakiwa kwenye Mkutano.
Mkutano wa Senet ukiendelea.
Mkutano wa Senet ukiendelea.
Mkutano wa Senet ukiendelea.
Mkutano wa Senet ukiendelea.
Mkutano wa Senet ukiendelea.
Mkutano wa Senet ukiendelea.
Mkutano wa Senet ukiendelea.
Mkutano wa Senet ukiendelea.
Mkutano wa Senet ukiendelea.
Mkutano wa Senet ukiendelea.
Mwenyekiti wa Senet Mkoa wa Shinyanga Said Sultan akitoa Kadi za CCM kwa Wanachama wa Senet Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto.
Mwenyekiti wa Senet Mkoa wa Shinyanga Said Sultan akiendelea kutoa Kadi za CCM kwa Wanachama wa Senet Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto.

Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya kumaliza kugawa Kadi za CCM kwa Wanachama wa Senet Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Burudani kwenye Mkutano wa Senet.
Mwenyekiti wa Senet Mkoa wa Shinyanga Said Sultan Awali akiwasili kwenye Mkutano huo akiwa amepanda kwenye Tela la Punda.

Awali Mwenyekiti wa Senet Mkoa wa Shinyanga Said Sultani akiwasili kwenye Mkutano katika Chuo za Sayansi za Afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464