Header Ads Widget

DC KISHAPU AZINDUA UWEKAJI ALAMA KULINDA VYANZO VYA MAJI

DC KISHAPU AZINDUA UWEKAJI ALAMA KULINDA VYANZO VYA MAJI

Na Marco Maduhu, KISHAPU

MKUU wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude,amezindua zoezi la uwekaji Alama kwenye mipaka ya vyanzo vya maji katika Mabwawa ya Songwa na Mhumbu wilayani humo, ili kuvilinda vyanzo hivyo vya maji kwa kuzuia shughuli za kibinadamu.

Zoezi hilo la limefanyika Jana Novemba 13,2023 likiambatana Sambamba na upandaji miti, ambalo limeratibiwa na Bodi ya Maji Bonde la Kati.
Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa wilaya kuzindua uwekaji wa Alama hizo, Mhandisi wa Mazingira kutoka Bodi ya Maji Bonde la Kati Nyacheli Mramba, amesema wameweka Alama hizo za mipaka na Mabango ili kuzuia wananchi wasifanye shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo hivyo ili kuvilinda visitoweke.

Naye Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, ametoa wito kwa wananchi wasifanye shughuli za kibinadamu kwenye Mabwawa hayo, ikiwamo na kufanya shughuli za kilimo na uchimbaji madini, bali wavitunze vyanzo hivyo vya maji kwa faida yao na vizazi vijavyo.
“Natoa wito kwa wananchi vitunzeni vyanzo hivi vya maji msifanye kabisa shughuli za kibinadamu, na katika Mabwawa haya yamejengwa Matangi kwa ajili ya kunyweshea mifugo yatumieni na msiingize tena mifugo ndani ya maji,”amesema Mkude.

Katika hatua nyingine, amewataka wananchi wa Kishapu kuzitumia ipasavyo Mvua ambazo zinanyesha hivi sasa, kwa kupanda miti ili kuifanya Kishapu kuwa ya kijani.
Nao baadhi ya wananchi wa Kata ya Songwa, wamesema uwekaji huo wa Alama za mipaka katika Mabwawa hayo,utasaidia kuvilinda vyanzo hivyo vya maji ambavyo vilikuwa hatarini kutoweka, kutokana na shughuli za kibinadamu ikiwamo kilimo, uvuvi na uchimbaji madini.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza mara baada ya kuzindua uwekaji Alama na Mabango kwenye mipaka ya vyanzo vya maji katika Bwawa la Songwa na Mhumbu ili kulinda vyanzo hivyo visitoweke sababu ya shughuli za kibinadamu.

Mhandisi wa Mazingira kutoka Bodi ya Maji Bonde la Kati  Nyacheli Mramba, akizungumza kwenye zoezi la uwekaji Alama mipaka kwenye vyanzo vya Maji Bwawa la Songwa na Mhumbu wilayani Kishapu.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akipanda Mti ili kulinda vyanzo vya Maji.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akipanda Mti ili kulinda vyanzo vya Maji.
Mhandisi Mazingira kutoka Bodi ya Maji Bonde la Kati Nyanchel Mramba akipanda Mti ili kulinda vyanzo vya Maji.
Diwani wa Songwa Abdul Ngolomole akipanda Mti ili kulinda vyanzo vya maji.
Afisa Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Kassim Said akipanda Mti ili kulinda vyanzo vya maji.
Afisa Mahusiano Mgodi wa Almasi Mwadui Benard Mihayo akipanda Mti ili kulinda vyanzo vya maji.
Mhandisi Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui Shagembe Mipawa akipanda Mti ili kulinda vyanzo vya maji.
Meneja Mazingira Mgodi wa Almas Mwadui Catherine Mrandaja akipanda Mti ili kulinda vyanzo vya Maji.
Zoezi la upandaji Miti likiendelea ili kulinda vyanzo vya maji.
Zoezi la upandaji Miti likiendelea ili kulinda vyanzo vya maji.
Muonekano wa chanzo cha Maji katika Bwawa la Songwa wilayani Kishapu.
Muonekano wa Chanzo cha Maji katika Bwawa la Songwa wilayani Kishapu.
Muonekano wa Chanzo cha Maji katika Bwawa la Mhumbu wilayani Kishapu.
Picha ya pamoja ikipigwa Watumishi wa Bodi ya Maji Bonde la Kati na Jumuiya za watumiaji Maji Songwa wilayani Kishapu.

Post a Comment

0 Comments