Viongozi na wananchi wa kijiji cha Kilimawe wakifurahi huduma ya maji
Na Kareny
Masasy, Shinyanga
WAKAZI wa kijiji cha kilimawe kata ya Mwantini halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wameanza kunufaika na mradi wa maji safi chanzo chake ni kutoka ziwa Victoria mbapo wameondokana na changamoto ya kununua maji ndoo sh 500 hadi 1000.
Hayo yamesemwa jana na wakazi hao mbele ya Mbunge viti Maalum mkoa wa Shinyanga Santiel Kirumba ambaye alikuwa ameambatana na viongozi wa umoja wa wanawake Tanzania (UWT) wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga kwaajili ya kujionea utekelezaji wa miradi ya maji vijijini.
Mbunge Kirumba amesema kazi imefanywa vizuri na wakala wa maji safi na mazingira vijijini (Ruwasa) ambayo mradi umekamilika kwa kutekelezwa siku 170 na fedha zimebaki na leo tarehe 30,Nomvemba,wananchi wananufaika rasmi. .
Mbunge Kirumba amesema kitu ambacho kimemfurahisha zaidi ni fedha kubaki katika mradi huo na amewaeleza wananchi maji hayo ni hazina wayatumie vizuri kwa kutunza miundombinu kwani Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa maono yake kipaumbele ni Elimu,afya na maji.
“Serikali imeleta fedha nyingi kwenye miradi ya maji tunachotaka maeneo yote kwenye taasisi kama shule na Zahanati yapate maji safi na salama waondokane na changamoto ya kutafuta maji ambayo siyo safi kazi imefanywa ya kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi”amesema Mbunge Kirumba.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Shinyanga Grace Samweli amesema wanasimamia ilani ya (CCM) kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama hivyo wanaume nao wanatakiwa kupongeza juhudi hizi ambazo zilikuwa zikiwafanya wanawake kutafuta maji nyakati za usiku nakucha kufanya shughuli za kijamii.
Katibu wa UWT mkoa wa Shinyanga Asha Kitandala amesema amefurahi kuona utekelezaji unaenda vizuri Zahanati imepata maji kama zipo changamoto ni ndogondogo zitaenda zikitatuliwa ila wanaipongeza Ruwasa kwa juhudi wanazozifanya kwa miradi ya maji.
Meneja wa Ruwasa wilaya ya Shinyanga mhandisi Emaeli Nkopi amesema mradi huo umetekelezwa ndani ya siku 170 na wakandarasi wa ndani ulianza rasmi tarehe 6,Juni,2023 na 30,Novemba,2023 umekamilka na umesanifiwa kuhudumia wanachi 2,262 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.
Nkopi amesema gharama ya mradi ni sh zaidi y ash Milioni 333 na fedha iliyotumika ni zaidi y ash Milioni 159 na kiasi kilichobaki ni zaidi ya sh Milioni 173 hivyo amewataka wananchi wajitokeze kuvuta maji kwa kwa kuwaona jumuiya za watumia maji (CBWSO) ambao watawapa utaratibu wa kuijiunga na fedha zinalipwa kwa njia ya mfumo.
Baadhi ya wananchi waliokuwa kwenye mkutano ulioongozwa na Mbunge Kirumba walihoji namna ya taasisi zitakavyolipia ankara za maji na wao kupata maji majumbani ambapo walipata ufafanuzi.
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga vijijini akiongea kwenye mkutano wa hadhara kutambulisha wageni.
Meneja Ruwasa wilaya ya Shinyanga Mhandisi Emaeli Nkopi akisoma taarifa
Mbunge Santiel Kirumba akiongea kwenye mkutano wa hadhara kijiji cha Kilimawe
Viongozi wakiteta kabla ya kukaribishwa kwenye kikao.
Katibu wa UWT mkoa wa Shinyanga Asha Kitandala akiongea kwenye mkutano wa hadhara
Mbunge vitimaalum Santiel Kirumba akitoa salamu kwenye mkutano wa hadhara
Wananchi wa kijiji cha Kilimamawe kata ya Mwantini halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Zahanati ya kijiji cha Kilimawe ikiwa na huduma ya maji
Mbunge Santiel Kirumba akiwa na wanawake wa kijiji cha Kilimawe kata ya Mwantini akishuhudia upatikanaji wa maji.
Wananchi wa kijiji cha Kilimamawe kata ya Mwantini halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464