Mkurugenzi wa kiwanda cha Jambo food Salum Hamis akielezea jinsi kiwanda hicho kinavyofanya kazi
Suzy Luhende Shinyanga press blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme amewataka wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kuanza kulima viazi lishe, nazi, ukwaju zabibu na kuanza kupanda mbegu za maembe ili kujiongezea kipato kwa sababu vina soko la uhakika Mkoani Shinyanga.
Hayo ameyasema kwenye ziara ya kukagua kiwanda cha kutengeneza juice cha jambo food kilichopo katika kata ya Ibadakuli manispaa ya Shinyanga, iliyokuwa na lengo la kujifunza na kudumisha uhusiano kwa wawekezaji.
Mndeme amesema baada ya kutembelea kiwanda cha jambo amegundua kuna fursa nyingi kwa wakulima wanaweza kuzipata, kwani kiwanda hicho kina mashine za kisasa ambazo zinaweza kutengeneza juice za nyanya, juice za viazi na parachichi, hivyo amewaomba wakulima kuanza kulima mazao hayo kwa sababu kuna soko la uhakika.
"Kwa kweli tumejifunza mengi tunakupongeza sana ukiwa kama Mtanzania mzawa ukiwa miongoni wa walipa kodi wazuri na umeajiri watanzania asilimia 99.9 ambao wanajipatia riziki hapa tunakushukuru sana, umetangaza Tanzaniana kumwinua mkulima hivyo uwekezaji huu unaenda kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja "amesema Mkuu wa Mkoa Mndeme.
"Wito wangu niwaombe wanashinyanga watanzania tupende kula vya kwetu kwani vina thamani sana tunakunywa maji ya kwetu juice za kwetu, hivyo serikali itaendelea kuwaunga mkono ili uzalishaji usikwame kiwanda hiki kiendelee kufanya kazi bila kuchoka ili Taifa letu lisonge mbele,"ameongeza Mndeme.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa jambo food Salumu Hamis (maalufu salumu Mbuzi)amesema tayari anatengeneza juice za zabibu, nazi,embe, nanasi na ukwaju lakini havijitoshelezi inafika wakati vinakosekana hasa nanasi, hivyo ana mpango wa kuanza kutengeneza juice ya viazi lishe na parachichi ili kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja hivyo amewaomba wakulima kuchangamkia fursa hiyo.
"Tuwaombe vijana wa kike wa kiume sasa wachangamkie fursa tunahitaji kupata viazi vingi tutanunua viazi, tulizungumza na watu wa ukiligulu jinsi ya kupata mbegu ya viazi lishe walisema wataanzisha mbegu bora,ili mkulima aweze kupata na kulima"amesema Hamisi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akiendelea kukagua kiwanda cha jambo food
Mkurugenzi wa kiwanda hicho Salum Hamis akielezea
Mkuu wa Mkoa Christina Mndeme akizungumza
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akinywa juice ya nazi iliyotengenezwa na kiwanda cha Jambo food