Mdhamini aliyetambulishwa na viongozi wa chama cha mpira wilaya hiyo Wakili Sweetbert Nkuba akiwakilishwa na Conrad Nkuba upande wa kushoto akiwa na viongozi wa mpira wa miguu wilaya hiyo katika ni mwenyekiti Hussein Salum na kutoka kulia ni katibu Timoth Fabian
Na Kareny Masasy,Kahama
LIGI ya chama cha mpira wa miguu wilayani Kahama mkoani Shinyanga (KDFA) imepata mdhamini ambaye ametoa sh Milioni 40 kwaajili ya kuendesha ligi hiyo ikiwemo zawadi za mshindi wa kwanza,pili na watatu, kikombe na medani kwa wachezaji.
Mdhamini aliyetambulishwa na viongozi wa chama cha mpira wilaya hiyo Wakili Sweetbert Nkuba akiwakilishwa na Conrad Nkuba amesema atatoa zawadi hizo na yuko tayari kushirikiana na wadhamini wengine.
Mwenyekiti wa chama cha Mpira wa miguu wilayani hapo Hussein Salum amesema hayo leo tarehe 25,Novemba ,2023 mbele ya waandishi wa habari ambapo ameeleza kupitia fedha hizo mshindi wa kwanza atapata sh Milioni tano na kikombe ,wa pili Milioni tatu na wa tatu sh Milioni moja.
Salum amesema ligi ya wilaya ina timu kutoka vilabu 21 vya mpira wa miguu ambavyo vitashiriki kwenye mchezo wa ligi hiyo inayotarajia kuanza kuchezwa tarehe 27,Novemba ,2023 na timu zitagawanywa kwenye makundi manne.
“Mdhamini ametoa sh Milioni 40 ambazo zimetumika kuanzia upatikanaji wa jezi,vifaa vingine vya mchezo na pia atatoa zawadi kwa washindi hao watatu na kiingilio ni bure”amesema Hussein.
Hussein amesema siku ya ufunguzi timu mbili zitapewa nafasi ya kucheza katika uwanja wa taifa wa wilaya ya Kahama ambazo ni timu ya Eagle Sports na Aladini zote za Kahama.
Hussein amesema ligi ya wilaya inatakiwa ichezwe kwa ubora ambapo wamefanya vikao na timu zote wakishirikiana na waamuzi ili mwisho wa ligi kuweza kupata timu iliyobora kwa kufuata kanuni 17 za mchezo wa mpira wa miguu.
Hussein amesema amfurahi kujitokeza kwa mdhamini huyo ambaye walimuomba kusaidia ili kuweza kuendesha ligi kwani hali halisi ya vilabu vya timu zilizopo ni duni hazijiwezi kifedha.
Mwakilishi wa mdhamini wa ligi hiyo Conrad Nkuba amesema ameguswa kusaidia ligi kuweza kunyanyua vipaji na kama nafasi ikiwepo ataweza kuongeza zawadi zaidi ya hapo ikiwemo medani kwa wachezaji kikubwa ni kuboresha michezo ndani ya wilaya ya Kahama.
Nkuba amesema yeye hata akijitokeza mdhamini mwingine yuko tayari kushirikiana naye ili kuweza kunyanyua vipaji vya vijana wenye nia ya kutaka kufika mbali.Mdhamini wa ligi ya mpira wa miguu wilaya ya Kahama Wakili Conrad Nkuba upande wa kushoto akiwa na viongozi wa mpira wa miguu wilaya hiyo katika ni mwenyekiti Hussein Salum na kutoka kulia ni katibu Timoth Fabian
Mdhamini wa ligi ya mpira wa miguu wilaya ya Kahama Wakili Conrad Nkuba upande wa kushoto akiwa na viongozi wa mpira wa miguu wilaya hiyo katika ni mwenyekiti Hussein Salum na kutoka kulia ni katibu Timoth FabianMdhamini wa ligi ya mpira wa miguu wilaya ya Kahama Wakili Conrad Nkuba upande wa kushoto akiwa na viongozi wa mpira wa miguu wilaya hiyo katika ni mwenyekiti Hussein Salum na kutoka kulia ni katibu Timoth Fabian
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464