MANISPAA YA SHINYANGA KUHAMASISHA VIJANA KUJIUNGA CHUO CHA MATANDA VTC
Na mwandishi wetu.
Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga imeahidi kuweka mikakati ya kuhamasisha vijana wa manispaa ya Shinyanga kujiunga na Chuo cha matanda VTC ili kuweza kupata mafunzo ya fani za ushonaji, ufundi wa magari,umeme na udereva ili
kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa kamati ya afya,elimu na uchumi ya manispaa ya Shinyanga, ambaye pia ni diwani wa kata ya Lubaga,Reuben Masanja wakati akifungua mahali ya tatu ya chuo cha matanda vtc leo novemba 17,2023 kwa niaba ya meya wa manispaa ya Shinyanga,
Kauli hiyo ameitoa kutokana na vijana wa manispaa ya Shinyanga kutokuwa
miongoni mwa wahitimu wa kozi hizo kwa mwaka huu
na wengi kukosa fursa za ajira
kutokana na kutokuwa na ujuzi ili kukabiliana na mahitaji ya soko la ajira.
Reuben anasema,anasikitishwa kwa kutoona hakuna hata kijana moja anayetoka manispaa ya Shinyanga aliyehitimu mafunzo kutoka chuo hicho licha ya kuwa kipo ndani ya manispaa.Vijana wengi waliohitimu katika chuo hicho wametoka mikoa ya mbali na halmashauri zingine ndani ya mkoa wa Shinyanga.
Reuben alisitiza uongozi wa chuo hicho kuweka jitihada zaidi za kujitangaza ili kutoa fursa kwa wana jamii kuweza kupeleka watoto wao katika chuo hicho ili kusaidia vijana kupata ajira kadri ya kozi zinazotolewa na chuo hicho.
Mwenyekiti wa kamati ya afya,elimu na uchumi ya manispaa ya Shinyanga, ambaye pia ni diwani wa kata ya Lubaga,Reuben Masanja akizungumza katika mahafali ya chuo cha matanda VTC."Hatuna budi,manispaa kutumia majukwa yetu kufanya
kampeni ya matangazo zaidi ili vijana wajiunge na chuo hiki kwa ajili ya kozi
zinazotolewa kwani kuna mambo mazuri na jamii haifahamu uzuri wa chuo cha
matanda,ni masikitiko kwa kuwa vijana wengi wanatoka mikoa ya mbali na vijana
wetu hawachangamkii fursa hii" anasema Reuben.
Kwa upande wake, Mkuu wa chuo cha matanda,Joaster Thomas Kisanko aliomba,Halmashauri hiyo kuweza kufadhili wasicha 17 kutoka kata za manispaa ya Shinyanga ili kusaidia wasichana katika kujikuwamua kiuchumi na kutoa wito kwa wazazi na walezi kupeleka watoto chuoni hapo.
"Ni wakati muhimu wa kuleta vijana katika chuoni kwa kuwa ziko fursa za ajira kwa maeneo mbalimbali baada ya kuhitimu kozi zinazotolewa na chuo chetu na tunaomba Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga kufadhili wasichana 17 pekee kutoka katika kata zao ili tuwapatie mafunzo ya kuweza kujiinua kiuchumi kwa maisha ya badaye"anasema Kisanko
Aidha ,Mkurugenzi wa Central Link logistic Tanzania, Wiliam James ,anasema wameamua kushirikiana na chuo kwa kutoa mafunzo ya umeme na kuwatumia vijana hao katika miradi ya REA kwa kushirikiana na Tanesco.
Mkurugenzi wa Central Link logistic Tanzania, Wiliam James akizungumza kuhusu ushirikiano wa mafunzo ya umeme wanayotoa katika chuo cha matanda VTC." Vi vema vijana kupata ujuzi ili kuweza kupata fursa ya ajira ,hiki ni chuo cha pili Tanzania kukipatia mafunzo na hata Tanesco mkoa wa Shinyanga walifurahi kuona ujio wetu kwa kuwaanda vijana kwa ajili miradi ya umeme"anasema william
Mratibu wa mafunzo chuo cha matanda VTC, Malia Elisapetha akizungumza na kutoa shukrani kwa wahitimu wote.Nao baadhi wanafunzi waliohitimu chuo hicho walisema wataweza kuendesha maisha yao na kujenga uchumi wa nchi baada ya kuhitimu mafunzo kwa miaka miwili kwa yale waliojifunza.