Kaimu Mkuu wa Takukuru(M) mkoa wa Shinyanga ,Mwamba Masanja akitoa taarifa ya vyombo vya habari mkoani Shinyanga.
TAKUKURU YABAINI SHILINGI MILIONI 83.3/-ZA KODI YA ZUIO HAZIJAWASILISHWA TRA-SHINYANGA
Na Mwandishi wetu.
TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU)mkoa wa Shinyanga, imebaini kiasi cha Tshs million 83.3 za kodi ya zuio kutowasilishwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania kutoka wa wazabuni na watoa Huduma katika mkoa wa Shinyanga na Kufanya serikali kupoteza mapato.
Akizungumza na vyombo vya habari leo novemba 6, 2023, Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Shinyanga,Mwamba Masanja wakati akiwasilisha taarifa ya uchambuzi wa mfumo wa kodi ya zuio kwa kipindi cha julai-septemba 2023 ,anasema kiasi cha Shs milioni 83 za kodi ya zuio zimebainika kutowasilishwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania kutoka kwa wazabuni na watoa huduma katika wilaya za Shinyanga, Kahama na kishapu.
Masanja anasema, Takukuru ilifanya uchambuzi wa mfumo wa ukataji na uwasilishaji wa kodi ya zuio katika ununuzi na vifaa na utoaji wa huduma ili kuthibiti upotevu wa mapato na kuthibiti mianya ya rushwa katika Usimamizi wa ukataji wa kodi ya zuio(2%) ya thamani ya bidhaa na (5%) kwa watoa Huduma.
“uchambuzi umebaini kuwa ,kwa mwaka wa fedha 202/2023 jumla ya Shs 83,328,256.81 zilizokatwa kwa wazabuni na watoa huduma hazikuwasilishwa TRA kama sharia inavyoelekeza.anasema Masanja.
Aidha,Masanja anasema sababu zilizopelekea kutowasilishwa kwa fedha hizo ni mabadiliko ya mfumo wa TRA(Tax Payer Portal),uelewa mdogo juu ya makato,wazabuni na watoa Huduma kutodai stakabadhi ya makato ya kodi ya zuio,wahasibu kutokata kodi ya zuio kutoka kwa watoa Huduma au bidhaa kinyume na sharia ya kodi.
“Takukuru inajipanga kukaa na Mamala ya Mapato,Halmashauri za wilaya na manispa ili kujadili matokeo ya uchambuzi huu na kuweka mikakati ya pamoja ya kutatua changamoto zilizojitokeza”amesema Masanja
Kwa upande mwingine, Takukuru ilifatilia miradi ya maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya bulige chenye thamani ya Shs million 630 na ujenzi wa shule ya msingi maganzo yenye thamani ya Shs milion500.
“Mradi wa ujenzi wa kituo cha afya bulige haujakamilika na ujenzi wa shule ya msingi maganzo umebainika kuwa jengo la utawala halijawekwa vigae,roof board haina ubora,vyoo vya wavulana kukukosa ventilation,madarasa ya chekechea mikanda ya gypsum boadi imeanza kubanduka na bembea upande wa chekechea hazijawekwa”anasema Masanja.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464