Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiendelea kukagua kiwanda cha mafuta ya alizeti na pamba cha Gilitu enterprises
Suzy Luhende, Shinyanga
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme amewataka wakulima kulima mazao ya pamba Alizeti na ufuta kwa wingi ili kiwanda cha Gilitu enterprises kilichopo mjini Shinyanga.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme amewataka wakulima kulima mazao ya pamba Alizeti na ufuta kwa wingi ili kiwanda cha Gilitu enterprises kilichopo mjini Shinyanga kiweze kuendelea kufanya kazi na kuongeza uzalishaji wa mafuta.
Agizo hilo amelitoa leo wakati akifanya ziara ya kukagua baadhi ya viwanda vilivyopo Mkoani Shinyanga kwa lengo la kuonyesha mashirikiano kati ya serikali na makampuni , na kujionea kazi zinayofanuyika katika kiwanda hicho ambacho kinatengeneza mafuta ya alizeti na pamba .
Mndeme amesema amekagua kiwanda hicho lakini amekuta changamoto ya kutokuwa na Alizeti na pamba za kutosha, hivyo mashine wakati mwigine kutofanya kazi kutokana na mapungufu hayo.
"Lengo letu ni kuhakikisha viwanda vyetu vya kuzalisha mafuta vinaendelea kuzalisha vizuri ili serikali ipate mapato na wakulima waweze kujiinua kiuchumi pale wanapouza mazao yao,"amesema Mndeme.
"Ni vizuri wale wajasiliamali wakulima tuongeze kasi ya kilimo cha arizeti, tunaona kiwanda cha Gilitu enterprises inapata arizeti chache na pamba kidogo,hivyo tunatakiwa tuongeze kasi ya kilimo cha arizeti ambayo ni mafuta mazuri , hivyo tunatakiwa tulime ili tuweze kupata mafuta bora na mazuri amvayo hayachakachuliwi ambayo ni mafuta salama ya kujilimia sisi wenyewe, ili tujisikie fahari"amesema Mndeme.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kiwanda cha Gilitu enterprises Gilitu Makula amesema mashine ya kutengenezea mafuta ipo vizuri lakini kuna changamoto ya ya zao la alizeti watu we gi hawajafunguka katika kulima zao hilo hasa kwa Mkoa wa Shinyanga kwani nyingi wanafuata Mkoani Simiyu.
"Mashine tunazo za kisasakabisa kwa ajili ya kukamlia mafuta lakini alizeti hatupati za kutosha hivyo tuwaombe wakulima walime alizeti za kutosha na pamba ili tuweze kuzalisha mafuta safi yenye kiwango kwa sababu tuna mitambo ya kisasa ya kusafishia,"amesema Makula.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akiendelea na ukaguzi kwenye kiwanda cha Gilitu enterprises kilichopo Mkoani Shinyanga
Mkurugenzi wa Gilitu enterprises Gilitu Makula akieleza jinsi kiwanda hicho kinavyofanya kazi
Mkurugenzi wa Gilitu enterprises Gilitu Makula akieleza jinsi kiwanda hicho kinavyofanya kazi
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akionyesha mafuta yanayotengenezwa na kiwanda cha enterprises
Mkurugenzi wa kiwanda Gilitu enterprises Gilitu Makula akieleza jinsi kiwanda hicho kinavyofanya kazi
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akionyesha unga wa mahindi unaotengenezwa katika kiwanda hicho
Ukaguzi wa kiwanda ukiendelea katika Kiwanda cha Gilitu enterprises
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464