Na Kareny Masasy, Kishapu
UMOJA wa wanawake Tanzania wa chama cha Mapinduzi (UWT) mkoa wa Shinyanga umeeleza ukatili uliokuwa unapatikana kwa wanawake sababu ya ukosefu wa maji safi na salama Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzaia Samia Suluhu ameuondoa ukatili huo.
Hayo yamesemwa leo tarehe 29,Novemba,2023 na
wajumbe wa UWT mkoa wakiongozwa
na mbunge viti maalum Santiel Kirumba ambapo amesema wakala wa
maji safi na mazingira vijijini (Ruwasa) mkoa wa Shinyanga wamefanya kazi kubwa ya
kutekeleza miradi ambayo serikali imetoa fedha nyingi.
Kirumba amesema kero kubwa ilikuwa ni maji na kipindi cha
miakka miwili ya Rais Samia Suluhu ametoa fedha nyingi kwenye miradi ya maji lengo
kuondoa kero hiyo kwa wananchi na waisimamie vizuri kwani miradi inatakiwa kuwa
endelevu.
“Mradi huu ni mkubwa
kwa mkoa mzima wa Shinyanga kwa kutumia fedha nyingi na hatutaki Rais akwamishwe ila tunaipongeza
Ruwasa ndani ya mkoa huu haijamkwamisha Rais ipo bega kwa bega”amesema Kirumba.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Shinyanga Grace Bizuru
amesema kitu ambacho wamejivunia nikuona wanawake
hawateseki tena na utafutaji wa maji
hali ambayo ilikuwa ikiwafanya wapate changamoto ndani ya ndoa zao na wengine
kufanyiwa vitendo vya ukatili.
Katibu wa UWT mkoa wa Shinyanga Aisha Kitandala amesema lengo
la chama kuona wanawake wanatatuliwa kero zao hasa upande wa maji ambao ulikuwa
ukionekana ukosefu wa maji ni chanzo cha ukatili kwa wanawake nakuwashauri Ruwasa kutumia
vibarua wanatoka kwenye eneo hilo ili wanufaike.
Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniface Butondo amesema ilani ya chama cha Mapinduzi waliyokuwa
wakiinadi imetekelezwa vizuri kwa kumtua mama ndoo kichwani kwa vijiji hivyo kwani kilio kikubwa kwa wananchi wa vijiji
hivyo ilikuwa ni kupata huduma ya maji.
Meneja wa Ruwasa wilaya
ya Kishapu mhandisi Dicksoni Kamazima
amesema ujenzi wa mradi wa maji ya bomba
katika kijiji cha Seseko hadi Ngundangali unagharimu zaidi ya sh Bilioni 2.8 unatekelezwa na
mkandarasi M/S na
Otonde Costruction and General Supplier Ltd kwa mkataba wa mwaka mmoja.
“Mpaka sasa tanki la maji linautekelezaji wa asilimia
88.5 na linaujazo wa lita laki moja
katika mnara wa mita 15 na kujenga vituo
vya kuchotea maji 31 katika mradi huo”amesema Kamazima.
Wakati huo huo mhandisi Kamazima amesema wakazi 49,965 kutoka vijiji 13 vya kata tatu vya halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani
Shinyanga watanufaika na mradi wa maji wa ziwa victoria uliogharimu
zaidi ya sh Bilioni 6.6.
Mhandisi Kamazima amesema mradi huo unatekelezwa kwa fedha za
serikali na mkandarasi amelipwa malipo
ya awali huku akivitaja vijiji vitakavyo nufaika kuwa ni Igaga A na B, Isagala, Mwamashele, Busongo, Mwamanota,
Bubinza, Lwagalalo, Mwamadulu,Nyawa,Beledi,,Lagana na Mihama.
“Utakapokamilika mradi huo
utawapunguzia muda wa kufuata maji umbali mrefu na kuwaongezea muda wa
kushiriki shughuli za kiuchumi na kijamii pia kupunguza mlipuko wa magonjwa
yatokanayo na kutumia maji yasiyo safi na salama.”amesema Kamazima.
Meneja Ruwasa mkoa wa Shinyanga mhandisi Juliette Payovela amesema miradi hiyo ikikamilika itaweza kuwaondolea kero wananchi
kwani serikali imeleta fedha za utekelezaji na wakandarasi wapo kazini
Diwani wa kata ya Lagana Luhende Sana amesema kata yake ina vijiji vitano ambavyo vyote vitanufaika kwani awali walikuwa wakinunua maji ndoo moja sh 1000 au kufuata umbali wa kilomita tano mto tungu.
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kishapu Rahel Madundo
Mhandisi Dickson kamazima akitoa maelezo mbele ya viongozi waliotembelea miradi ya maji.
Mhandisi Dickson kamazima akitoa maelezo kwa viongozi wa UWT waliotembelea mradi wa maji
Asha Katandala ambaye ni katibu wa UWT mkoa wa Shinyanga akiwatambulisha viongozi wenzake
Mhandisi wa Ruwasa mkoa wa Shinyanga Juliette Payovela akiwa na mbunge viti maalum Santiel Chilumba kwenye mradi wa maji
Mbunge viti maalum Santiel Chilumba akipiga makofi kwa Ruwasa baada ya kufanya vizuri kwenye miradi
Tanki la maji lililopo kwenye kijiji cha Lagana wilayani Kishapu
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464