WAKALA wa maji safi na mazingira vijijini (Ruwasa) wilaya ya Shinyanga imekamilisha mradi wa maji Masengwa.
Na Kareny Masasy,Shinyanga
WAKALA wa maji safi na mazingira vijijini (Ruwasa) wilaya ya Shinyanga imeeleza ukamilishaji wa mradi wa maji Masengwa ya awamu ya pili kwa viongozi wa umoja wa wanawake Tanzania (UWT) wa Chama cha Mapinduzi wa mkoa Shinyanga.
Meneja wa Ruwasa Mhandisi Emael Nkopi amesema hayo jana tarehe 30,Novemba,2023 mbele ya viongozi hao ambao walikuwa wakiongozwa na Mbunge Santiel Kirumba katika kutembelea miradi ya maji iliyotolewa fedha na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Mhandisi Nkopi amesema ujenzi wa tanki la maji ishinabulandi umekamilika na linatoa huduma katika vijiji viwili vya Ishinabulandi na Bubale ikiwa tanki linaujazo wa lita 200,000 nalimekamilika.
Kuna vituo 46 vya kuchotea vimejengwa katika maeneo tofauti,vituo 15 vya Bubale na Ishinabulandi vnatoa huduma ya maji na vituo nane vya Isela,Idodoma,vinatoa huduma ya maji na vituo nane vya Ibingo na Ngwa’nghalanga viko kwenye majaribio na muda sio mrefu vitaanza kutoa huduma ya maji.
Mbunge Santiel Kirumba alipongea kwa kazi hiyo ambayo wananchi wengi sasa wanapata maji safi na salama hivyo waziri wa maji Juma Aweso na Wahandisi wa maji mkoa wa Shinyanga mungu awabariki kwa kazi nzuri yenye uaminifu kwani ukosefu wa maji umeanza kuwa historia.
“Mhandisi wa maji ni mwanake ambaye ni Juliette Payovela ameguswa kwelikweli na wanawake kumtua ndoo kichwani ametekeleza kwa vitendo kazi yake anayopaswa kuifanya kwa kusimamia fedha na anastahili kupongezwa ukatili wa wanawake kupitia maji sasa basi…”amesema mbunge Kirumba.
Katibu wa UWT mkoa wa Shinyanga Asha Kitandala amesema kazi nzuri imetekelezwa na serikali na ilani ya chama cha Mapinduzi imeenda vizuri wananchi wa maeneo ya vijiji na kwenye baadhi ya shule zinapata maji.
“Rais wetu Samia Suluhu Hassan mungu amubariki kazi amefanya kwa vitendo tunajionea tumepita kila maeneo yenye mradi wa maji imerizisha kweye utekelezaji na imekamilika”amesema Kitandala.
Mbunge vitimaalum Santiel Kirumba akifungua maji moja ya kituo cha kuchotea maji kilichopo shule ya msingi Masengwa.
Mbunge vitimaalum Santiel Kirumba akiongea na wanafunzi wa shule ya msingi Masengwa.
Tanki la maji lilojengwa nakusambaza maji kwenye vituo vya kuchotea maji.
Viongozi wakifurahishwa na utendaji wa Ruwasa mkoa wa Shinyanga.