Header Ads Widget

TANROAD -MARA YAANZA KUTENGENEZA BARABARA YA NATA HADI MUGUMU YENYE KILOMITA 126.73

TANROAD -MARA YAANZA KUTENGENEZA BARABARA YA NATA HADI MUGUMU YENYE KILOMITA 126.73

Meneja wa Tanroads mkoa Mara Mhandisi Vedastus Maribe  akizungumza na vyombo vya habari.

 Na Kareny Masasy,

Mara

WAKALA  ya barabara nchini (Tanroads) mkoa wa Mara imeanza matengenezo  ya Barabara ya Sanzate kupitia Nata Hadi  Mugumu yenye urefu wa kilomita 126.73  kwa kutumia zaidi ya sh Bilioni 39

Meneja wa Tanroads mkoa huo Mhandisi Vedastus Maribe  ameyasema hayo novemba 9,2023 alipokuwa akiongea na waandishi wa habari  wa kanda ya ziwa waliokuwa wakitembelea miradi mbalimbali ikiwemo ya kimkakati iliyotumia fedha za  ndani.

Mhandisi Maribe amesema barabara hiyo ilianzwa kutengenezwa  mwaka 2020  itakuwa kwa kiwango cha lami pina sasa imefikia  asilimia 41 ya ujenzi na pindi ikikamilika itakuza uchumi  kwa wananchi wa mkoa huu.

"Barabara hii ni kiungo  muhimu  kati ya wilaya ya Musoma,Butiama na Serengeti na itakapo kamilika  hata mikoa jirani  itanufaika na Ile ya mali  itafahisishiwa kwenye Shughuli za utalii katika mbuga za wanyama Serengeti"amesema Mhandisi Maribe.

Pia Mhandisi  Maribe amesema  barabara ya Tarime  kwenda Mugumu yenye urefu wa kilomita  87.14 na Mogabiri  kwenda Nyamongo yenye urefu wa  kilomita 25 itajengwa kwa kiwango cha lami.

 "Ambapo vipande hivyo vya Barabara vitagharimu zaidi ya sh Billioni 34 ulianza mwaka 2022 na kutarajia kukamilika mwaka 2024 Fedha hizo zimetolewa na Serikali kwa asilimia 100 na wakandarasi wanaotekeleza  kazi hiyo no watanzania"amesema Mhandisi Maribe.

Post a Comment

0 Comments