Header Ads Widget

MVUA YA MAWE NA UPEPO YALETA MAAFA KIJIJI CHA IBANZA WILAYANI SHINYANGA,NYUMBA 51 ZAANGUKA WANANCHI WANUSURIKA KIFO

MVUA YA MAWE NA UPEPO YALETA MAAFA KIJIJI CHA IBANZA WILAYANI SHINYANGA, NYUMBA 51 ZAANGUKA WANANCHI WANUSURIKA KIFO

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MVUA ya Mawe na Upepo imeleta maafa katika Kijiji cha Ibanza Kata ya Mwamala wilayani Shinyanga, na kuleta maafa kwa wananchi huku nyumba 51 zikianguka na kukosa makazi, pamoja na kuathiri mashamba na mifugo.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Decemba 6,2023 majira ya saa 9 usiku.
Mmoja wa waathirika wa tukio hilo Jilala Dutu, amesema mvua ilianza kunyesha majira hayo ya usiku huku wakiwa wamelala, lakini ghafla walisikia mabati yakibebwa na upepo na kutupwa pembeni na nyumba yao, na wakati huo huo nyumba ikianguka kwa ndani na kujeruhi mtoto na Mama Mkwe wake.

“Nyumba ilivyoanguka tofari lilimpiga mtoto kichwani akachanika, huku mama mkwe naye akipigwa na tofari na kuvunjika mguu lakini hakuna kifo ambacho kimetokea,”amesema Dutu.
Muathirika Mwingine Nkuba Jigadi, amesema  nyumba yake mmoja imeaguka pamoja na shamba lake la Mahindi Hekali Moja limeharibiwa vibaya na mvua hiyo ya Mawe.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, ametoa pole kwa waathirika wote wa mvua hiyo, huku akibainisha kuwa kwa Wananchi ambao wote wameumia Serikali itagharamikia matibabu yao.
Amesema mbali na kugharamia matibabu, pia wananchi ambao mashamba yao yameharibika watapewa mbegu bure ili wapande upya kwa sababu mvua bado zinaendelea kunyesha,na kubainisha kuwa wale ambao watahitaji Maturubai watapewa, na kuwapongeza wananchi ambao wamejitolea kuwahifadhi ndugu zao kwa muda.

Katika hatua nyingine, ameagiza Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA)kufika katika Kijjiji hicho cha Ibanza kuangalia utaratibu wa wananchi kupata huduma ya majisafi na salama, baada ya kisima walichokuwa wakitumia kufunikwa na maji ya bwawa, huku akiwataka pia viongozi kuzuia watoto wasichezee kwenye maeneo hatarishi yaliyojaa maji.
Aidha, Mndeme ameawaagiza pia Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA)kutengeneza miundombinu ya Barabara Kilimita 2 kutoka Kijiji hicho cha Ibanza hadi Kizumbi Manispaa ya Shinyanga.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Simon Berege, awali akitoa taarifa ya Maafa hayo ya Mvua kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, amesema Nyumba 51 zimeanguka, Mashamba ya Mahindi Hekali 10 yameathirika, kuku 20 zimekufa na Mbuzi Mmoja na hakuna kifo, na Bibi ambaye amevunjika Mguu anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza eneo la tukio la Maafa ya Mvua ya Mawe na Upepo Kijiji cha Ibanza wilayani Shinyanga.
Diwani wa Mwamala Hamis Masanja akizungumza Athari za Mvua hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashari ya wilaya ya Shinyanga Simon Berege akitoa taarifa za athari wa Mvua hiyo.
Muathirika wa Mvua hiyo Jilala Dutu akielezea namna familia yake ilivyonusurika Kifo baada ya nyumba kuanguka wakiwa wamelala.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akifariji Waathirika wa Mvua hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiangalia nyumba ambazo zimeanguka.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiangalia namna Mashamba yaliyoathirika na Mvua hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiangalia namna Mashamba yaliyoathirika na Mvua hiyo.
Namna Mazao yalivyo haribika na Mvua ya Mawe na Upepo.
Muonekano wa Baadhi ya Nyumba ambazo zimeanguka.
Muonekano wa Baadhi ya Nyumba ambazo zimeanguka.
Muonekano wa Baadhi ya Nyumba ambazo zimeanguka.
Muonekano wa Baadhi ya Nyumba ambazo zimeanguka.
Maji yakiwa yamefunika Kisima cha Maji.
Bwawa likiwa limejaa Maji ambalo lipo jirani na Makazi ya watu.
Viongozi wakiangalia Maafa ya Mvua.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiwa na viongozi mbalimbali wakifika eneo la tukio kuangalia maafa ya mvua katika Kijiji cha Ibanza Kata ya Mwamala wilayani Shinyanga.

Post a Comment

0 Comments