Header Ads Widget

SHUWASA WAKARABATI VYUMBA MADARASA SHULE YA MSINGI JOMU

SHUWASA WAKARABATI VYUMBA MADARASA SHULE YA MSINGI JOMU

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga(SHUWASA),wamekabidhi Rasmi vyumba vya Madarasa ambavyo wamevifanyia ukarabati katika Shule ya Msingi Jomu Manispaa ya Shinyanga.

Makabidhiano hayo yamefanyika leo Decemba 7,2023 katika shule hiyo na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali akiwamo Diwani wa Kambarage Hassani Mwendapole, Kamati ya Shuleni, Afisa Elimu Kata na Afisa Shule za Msingi Manispaa ya Shinyanga Mary Maka.
Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA Mhandisi Yusup Katopola, akizungumzia ukarabati wa vyumba vya Madarasa, amesema mwaka Jana walipofika kwenye Mahafali ya Shule hiyo alikuta hali si nzuri ya vyumba vya madarasa hivyo wakaguswa na kuvifanyia ukarabati.

Amesema wao Kama Mamlaka ya Maji ukarabati huo wa vyumba vya Madarasa katika shule hiyo ni sehemu ya kurudisha kwa jamii, ili kuwajengea mazingira mazuri wanafunzi ya kusoma na kupata ufaulu uzuri na kutimiza ndoto zao.
"Tumekarabati vyumba vitatu vya Madarasa katika shule hii ya Msingi Jomu, kwa kuziba nyufa, uwekaji sakafu na kuvipaka rangi na sasa watoto watasoma kwenye mazingira rafiki kabisa na kufanya vizuri kitaaluma,"amesema Mhandisi Katopola.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Jomu Pendo Peter, amewapongeza SHUWASA kwa ukarabati vyumba hivyo vya Madarasa shuleni hapo, hali ambayo itachangia wanafunzi kuendelea kufanya vizuri kitaaluma.
Amesema ufaulu mzuri katika shule hiyo umekuwa ukichangiwa pia na wadau wa Maendeleo, huku akimpongeza Rais Samia kwa kutoa fedha shuleni hapo na kujengwa vyumba vipya vitano vya madarasa.

Nao wanafunzi wa shule hiyo wameipongeza SHUWASA kwa kuwakarabatia vyumba hivyo vitatu vya madarasa, pamoja na Rais Samia kuwajenga vyumba vitano, na kuahidi watasoma kwa bidii na kutimiza ndoto zao.
Mkurugenzi wa SHUWASA Mhandisi Yusup Katopola (kulia) akipongezwa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Jomu Pendo Peter kutokana na kukarabati vyumba vya Madarasa shuleni hapo.
Mkurugenzi wa SHUWASA Mhandisi Yusup Katopola (kulia) akipongezwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Jomu Rosemary Malongo kutoka na kukarabati vyumba vya Madarasa shuleni hapo.
Diwani wa Kata ya Kambarage Hassani Mwendapole (kushoto) akimpongeza Mkurungenzi wa SHUWASA Mhandisi Yusuph Katopola kwa kukarabati vyumba vya Madarasa shuleni hapo.
Kamati ya Shule ikiwa kwenye Makabidhiano ya ukarabati wa vyumba vya Madarasa.
Muonekano wa vyumba vya Madarasa vilivyokarabatiwa.
Muonekano wa vyumba vya Madarasa vilivyokarabatiwa.
Muonekano wa vyumba vya Madarasa vilivyokarabatiwa.
Muonekano wa vyumba vya Madarasa vilivyokarabatiwa.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Jomu.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Jomu.
Makabidhiano ya vyumba vya Madarasa vilivyokarabatiwa yakiendelea.
Makabidhiano ya vyumba vya Madarasa vilivyokarabatiwa yakiendelea.
Makabidhiano ya vyumba vya Madarasa vilivyokarabatiwa yakiendelea.
Picha za pamoja zikipigwa.
Picha za pamoja zikipigwa.

Post a Comment

0 Comments