WANANCHI WA KINAGA WAMSHUKURU RAIS SAMIA KUWAJENGEA KITUO CHA AFYA


WANANCHI WA KINAGA WAMSHUKURU RAIS SAMIA KUWAJENGEA KITUO CHA AFYA

WANANCHI wa Kata ya Kinaga katika Manispaa ya Kahama mkoani shinyanga wamemshukuru 
 Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea Kituo cha Afya Kinaga.

Hayo yamebainishwa Jana kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme wakati akiweka jiwe la Msingi kwenye Kituo hicho cha Afya.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Kata ya Kinaga, Diwani Mary Joseph Manyambo amesema kuwa, awali wananchi wa kata hii walikuwa wakitembea umbali wa zaidi ya Kilomita 15 kwenda Kahama mjini kufuata huduma ya afya ambapo hivi sasa wanapata hapo kinaga.

 Amesema wanamshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha za ujenzi wa kituo hichi cha afya ambacho kimekuja kuwa mkombozi kwa Wananchi.

"Tunamshukukuru sana Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha za ujenzi wa kituo hiki, na leo wananchi wa Kinaga wanapata huduma zote muhimu hapahapa kinaga," amesema Mary.

Akitoa salamu za mkoa, RC Mndeme amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha na kuwajengea Kituo hicho cha Afya.

Aidha, amewapongeza pia Manispaa ya kahama kwa kujazia zaidi ya Sh. Milioni 169 na kufanya Jumla ya Sh.milioni 669 kugharamia ujenzi huo ambao unaotarajiwa kukamilika Desemba 31, 2023.

Awali akisoma taarifa kwa mgeni rasmi Mganga Mfawidhi kituo cha afya kinaga Bi. Maria Chaeka amesema,kukamilika kwa kituo hicho kunakwenda kuwanufaisha wananchi 22,243 wa Kata ya Kinaga na vijiji jirani ambapo kituo kinajumuisha majengo ya wangonjwa wa nje (OPD), wodi ya kujifungulia akina mama wajawazito, upasuaji, maabara, kichomea taka, kitengo maalumu cha VVU, kifua kikuu pamoja na kkiniki ya baba, mama na mtoto.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464