RC MNDEME AMTAKA MKANDARASI KUKAMILISHA MRADI WA USAMBAZAJI UMEME KATIKA VIJIJI 146 KAHAMA


RC MNDEME AMTAKA MKANDARASI KUKAMILISHA MRADI WA USAMBAZAJI UMEME KATIKA VIJIJI 146 KAHAMA
NA MWANDISHI WETU 

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme amemtaka Mkandarasi anayetekeleza mradi wa kusambazaji umeme vijijini awamu ya tatu mzunguko wa pili ndani ya wilaya ya Kahama TONTAN PROJECT COMPANY TECHNOLOGY LTD kwa kushirikiana na mkandarasi GROUP PROJECT INTERNATIONAL LTD kuwasha umeme katika kwenye vijiji vyote 146 vya wilaya ya Kahama ifikapo Desemba 31, 2023.

Amesema hayo jana Desemba 11, 2023 katika ziara yake ya kikazi alipofika kuzindua mradi wa usambazaji umeme katika vijiji 17 kwenye kata ya Igunda Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama.

Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Mkandarasi kutoka Shirika la usambazaji umeme Tanzania TANESCO Antoni Tarimo amesema mpaka sasa mradi huo umefikia asilimia 64 huku kaya 699 zimeunganishiwa nishati ya umeme mpaka sasa.

“Mnamo Oktoba 2021 wakandarasi hawa walisaini mkataba wakufikisha umeme katika vijiji 146 vya wilaya ya Kahama ukiwa na gharama za utekelezaji Bilioni 32.8 ambapo kwa sasa umefikia asilimia 64 za utekelezaji huku jumla ya vijiji 13 vipo kwenye hatua ya mwisho kukamilika, vijiji 58 kazi inaendelea na kaya 699 zimeunganishwa na huduma ya umeme mpaka sasa, mradi huu unatarajia kumalizika ifikapo Desemba 31, 2023”, amesema Antoni Tarimo.

Akieleza hali ya upatikanaji wa huduma ya umeme katika kijiji cha Zobogo mwenyekiti wa kijiji hicho Sumuni Muhangwa amesema zipo baadhi ya taasisi ikiwemo za kidini kukosa huduma ya umeme kutokana na uchache wa nguzo zilizopo na kuiomba serikali kuongeza nguzo za kusambazia umeme kwenye kijiji hicho cha Zobogo.

“Tunashukuru sana siku ya leo kwa kuja kutuwashia umeme katika kijiji chetu, tunaipongeza sana serikali kwa kutuona wanakijiji wa kijiji cha Zobogo lakini tungeomba kuongezewa nguzo kwa sababu mpaka sasa yapo baadhi ya maeneo mbayo hayajafikiwa na huduma hii kutokana na uchache wea nguzo za kusambazia umeme ikiwemo makanisa na sehemu zingine”, amesema Sumuni Muhangwa.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la ushetu Emmanuel Cherehani amempongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwaajili ya utekelezaji wa mradi huo pamoja na miradi mingine inayoendelea kutekelezwa ndani ya halmashauri ya Ushetu.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme amemtaka mkandarasi kuongeza kasi ya ukamilishaji wa mradi huo hadi ifikapo Desemba 31, 2023 awe ameshamaliza kusambaza umeme kwenye vijiji vyote 146.

“Umeme vijijini ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi na leo tumeshuhudia tangu tumepata uhuru leo wakazi wa kijiji hiki wananufaika na huduma ya umeme, wote tumesikia kwenye taarifa ya utekelezaji wa mradi huu vipo vijiji ambavyo bado havijafikiwa na huduma hii ya umeme, maelekezo yangu kwako mkandarasi ifikapo Desemba 31, 2023 uwe umekwisha sambaza umeme kwenye vijiji vyote 146 vilivyopo ndani ya wilaya ya Kahama kama mkataba unavyoelekeza, usipomaliza vijiji hivyo hatua zingine zitafuata”, amesema RC Mndeme.

Aidha Rc Mndeme ametembelea miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa ofisi za halmashauri ya Ushetu unaotekelezwa katika kata ya Nyamilangano uliogharimu takribani shilingi bilioni 5, ujenzi wa kituo cha afya Ushetu kilichopo kijiji cha Mbika kata ya Ushetu pamoja na ujenzi wa kituo cha polisi kata ya Ulowa.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa usambazaji umeme katika kijiji cha Zobogo Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (kushoto) akitembelea mradi wa usambazaji umeme kijiji cha Zobogo.
Mwenyekiti wa kijiji cha Zobogo Sumuni Muhangwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo.
Mradi wa usambazaji umeme uliopo katika kijiji cha Zobogo halmashauri ya Ushetu.
Mkandarasi Kampuni ya TONTAN PROJECT COMPANY TECHNOLOGY LTD, JONH ZENG akieleza hali ya utekelezaji wa mradi huo.
Mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani akizungumza wakati wa ziara hiyo ndani ya halmashauri ya Ushetu.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza mara baada ya kuwasha umeme kwenye kijiji cha Zobogo.






Mradi wa ujenzi ofisi za halmashuri ya Ushetu ukiendelea.

Ujenzi wa kituo cha afya Ushetu ukiendelea.
Miongoni mwa vifaa vilivyopo kituo cha afya Ushetu.



Ujenzi wa kituo cha afya kata ya Ulowa.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza kwenye mradi wa ujenzi wa kituo cha polisi kata ya Ulowa.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita akizungumza wakati wa ziara hiyo.
Diwani wa kata ya Ulowa Gabliela Kimalo akizungumzia hali ya usalama kabla ya ujezi wa kituo cha polisi kwenye kata hiyo.

Mratibu mwandamizi wa polisi SSP. Chrisantus Kavishe akisoma taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa kituo cha polisi kata ya Ulowa.



Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emmmanuel Cherehani akizungumza wakati walipotembelea kujionea ujenzi wa kituo cha afya Ushetu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akikagua ujenzi wa kituo cha afya Ushetu.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa ofisi za halmashauri ya Ushetu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akikagua ujenzi huo.




Afisa Mipango halmashauri ya Ushetu Alfred John akisoma taarifa ya utekelezaji wa ujezi wa ofisi za halmashauri ya Ushetu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akipika ugali wakati alipotembelea mradi wa ujezi wa kituo cha polisi kata ya Ulowa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464