CHAMA cha wafanya Biashara,Viwanda na Kilimo (TCCIA) Mkoa wa Shinyanga kimekabidhi misaada ya chakula na vitu vingine kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Chrsitina Mndeme kwa ajili ya waathirika wa tukio la mafuriko wilayani Kateshi.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga amewashukuru wakazi wa mkoa huo kwa kujitokeza kutoa misaada yao kwa ajili ya watu waliopatwa ma maafa ya Mafuriko Kateshi na kuwaomba waendelee na moyo huo.
kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha wafanya biashara mkoa wa Shinyanga Jonathan Manyama amesema wafanya biashara wa mkoa wa Shinyanga wameguswa na tukio hilo na kutoa pole kwa waathirika wote
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464