WANANCHI KIJIJI CHA NGUNGA WALIOPITIWA MRADI UMEME WA JUA KISHAPU WAMEPEWA PEMBEJEO ZA KILIMO
Na Marco Maduhu,KISHAPU
WANANCHI wa Kijiji cha Ngunga wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, ambao wamepitiwa na mradi wa umeme wa Jua, wamepatiwa Pembejeo za Kilimo.
Zoezi la ugawaji wa Pembejeo hizo za Kilimo limeanza kufanyika leo Decemba 13,2023 katika Kijiji hicho cha Ngunga na kuzinduliwa na Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude.
Kaimu Mkurugenzi wa Kishapu Dk.Sabinus Chaula awali akitoa taarifa kwa Mkuu wa wilaya kabla ya kuzindua zoezi la ugawaji Pembejeo za Kilimo kwa wananchi, amesema hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa shughuli za mradi wa umeme wa Jua, kwa urejeshaji wa hali za wananchi kiuchumi pamoja na kuwa na chakula ambao wamepitiwa na mradi huo.
Amesema Halmashauri ya wilaya ya Kishapu kwa kushirikiana na TANESCO katika mradi wa umeme wa Jua Kijiji cha Ngunga, kwamba licha ya wananchi kulipwa fidia kupisha maeneo ya mradi, pia wanawahakikishia wanarudisha hali zao za maisha na uhakika wa chakula, ndiyo maana wamewapatia Pembejeo za Kilimo.
“Pembejeo za Kilimo ambazo wanapatiwa Wakulima ni Mbolea za kupandia na kukuzia mazao,Viuatilifu, Mbegu za Choroko, Alizeti, Mtama, na vifaa vya Kilimo ambavyo ni Majembe, Panga, Visu, Pampu za kupulizia wadudu, na vifaa kinga Gambuti, Gloves na Ovaroli,”amesema Dk. Chaula.
Aidha, ametaja idadi ya Kaya ambazo zinanufaika na mradi huo kuwa zipo 75 zenye wananchi 556, kwamba licha ya kupewa Pembejeo za Kilimo, watalimiwa pia na mashamba yao jumla ya Hekali 516, na watapewa na elimu ya mbinu bora za Kilimo,Ufugaji, na utunzaji wa mazingira.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, akizungumza kwenye uzinduzi huo wa ugawaji wa Pembejeo, amewataka Maofisa Ugani wawe bega kwa bega na wananchi hao, kwa kuhakikisha wanawapatia Elimu ya Kilimo bora na kufanya Kilimo chenye Tija ili wapate mavuno mengi.
Amewataka pia wananchi vifaa ambavyo wamepatiwa kwa ajili ya Kilimo,wavitumie vizuri pamoja na kuvitunza, huku akitoa maelekezo kwamba Pembejeo hizo zigawiwe haraka kwa Wakulima ili waendelee na kilimo.
Nao baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Ngunga akiwamo Charles Nshoka, wameipongeza Serikali pamoja na TANESCO kwa kuendelea kuwajali na kuwapatia Pembejeo hizo za Kilimo, ili walime na kupata chakula.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwenye zoezi la Ugawaji Pembejeo za Kilimo kwa Wananchi wa Kijiji cha Ngunga.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Dk.Sabinus Chaula akisoma taarifa ya mradi.
Diwani wa Talaga Richard Dominick akizungumza kwenye zoezi hilo la Ugawaji Pembejeo za Kilimo kwa wananchi.
Meneja mradi wa Umeme wa Jua Kishapu kutoka TANESCO Mhandisi Emmanuel Mbando akizungumza kwenye zoezi hilo la Ugawaji wa Pembejeo za Kilimo kwa wananchi wa Kijiji cha Ngunga.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude (kushoto) akigawa Pembejeo za Kilimo kwa wananchi wa Kijiji cha Ngunga.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude (kushoto) akiendelea na zoezi la kugawa Pembejeo za Kilimo kwa wananchi wa Kijiji cha Ngunga.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude (kushoto) akiendelea na zoezi la kugawa Pembejeo za Kilimo kwa wananchi wa Kijiji cha Ngunga.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude (kushoto) akiendelea na zoezi la kugawa Pembejeo za Kilimo kwa wananchi wa Kijiji cha Ngunga.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude (kushoto) akiwagawa Vifaa Kinga.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude (kulia)akiangalia Pembejeo za Kilimo.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akiangalia Pembejeo za Kilimo.
Muonekano wa Pembejeo za Kilimo.
Muonekano wa Pembejeo za Kilimo.
Muonekano wa Pembejeo za Kilimo.
Muonekano wa Pembejeo za Kilimo.
Muonekano wa Pembejeo za Kilimo.
Muonekano wa Pembejeo za Kilimo.
Muonekano wa Pembejeo za Kilimo.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akipiga picha ya pamoja na wananchi.
Wananchi wa Kijiji cha Ngunga akiwa kwenye zoezi la kupewa Pembejeo za Kilimo.
Wananchi wa Kijiji cha Ngunga akiwa kwenye zoezi la kupewa Pembejeo za Kilimo.
Wananchi wa Kijiji cha Ngunga akiwa kwenye zoezi la kupewa Pembejeo za Kilimo.