WAZIRI WA TAMISEMI MOHAMED MCHENGERWA AKABIDHI MAGARI MANNE YA USIMAMIZI SEKTA YA AFYA KWA WAGANGA WAKUU SHINYANGA


WAZIRI WA TAMISEMI MOHAMED MCHENGERWA AKABIDHI MAGARI MANNE YA USIMAMIZI SEKTA YA AFYA KWA WAGANGA WAKUU SHINYANGA

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEM Mohamed Mchengerwa, amekabidhi Magari Manne ya usimamizi katika Sekta ya Afya Mkoani Shinyanga ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi kwa Waganga Wakuu wa wilaya na Mkoa.

Zoezi la kukabidhi Magari hayo limefanyika leo Decemba 14, 2023 lililoendana sambamba na kuzungumza na Watumishi wa Serikali mkoani Shinyanga, katika ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Waziri Mchengerwa akizungumza kwenye zoezi hilo la kukabidhi Magari hayo, amemtaka Mganga Mkuu wa Mkoa na Waganga Wakuu wa Halmashauri, kuyatumia kikamilifu kuwatembelea Watumishi wa Afya pamoja na kufanya nao vikao vya mara kwa mara, ili kuboresha utendaji kazi wa kuhudumia wananchi na kuokoa Afya zao, wakiwamo wajawazito na kupunguza vifo vya uzazi.

“Nakabidhi Magari haya Manne ya usimamizi katika Mkoa wa Shinyanga ambapo gari moja ni la Mganga Mkuu wa Mkoa, na Mengine Matatu ni ya Waganga Wakuu wa wilaya, hivyo yatumieni Magari haya kwenda kufanya vikao na watumishi na kukagua huduma za afya ili wananchi wapate huduma bora za matibabu,”amesema Mchengerwa.
Aidha, amewataka Watumishi wa Sekta ya Afya mkoani Shinyanga kuendelea kutoa huduma stahiki za matibabu kwa wananchi, pamoja na kuhudumia Wajawazito ipasavyo na siyo kutanguliza pesa mbele, bali wawapatie huduma kwanza ili kumuokoa yeye na mtoto wake.

Amesema kwa Mtumishi wa Afya ambaye atasababisha kifo cha Mjamzito kwa wasababu ya uzembe, atamchukulia hatua mara moja.

Naye Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dk. Willison Mhela, amesema vifo vingi vya Wajawazito hutokana na kuchelewa kupata huduma, huku akibainisha kuwa kwa taaifa ambayo wameitoa hivi karibuni, vifo vya uzazi vimepungua kutoka 556 kwa vizazi hai laki moja hadi 104.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuboresha huduma za Afya mkoani humo, kwa kutoa fedha nyingi na kujengwa Vituo vya Afya, Zahanati,Hospitali za Wilaya, Mkoa, kutoa Vifaa tiba, Madawa, na sasa ameleta Magari Manne ya usimamizi kwa Waganga Wakuu.

Aidha, amesema Magari hayo ya usimamizi ya Waganga Wakuu watayasimamia vizuri na kufanya kazi iliyokusudiwa, na kubainisha kuwa katika Mkoa wa Shinyanga upande wa Sekta ya Afya Rais Samia katika utawala wake ameshatoa Sh.bilioni 34.7 pamoja na kununua CT- SCAN ya kisasa na Digital X-RAY katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.
Nao baadhi ya Watumishi wa Sekta ya Afya mkoani Shinyanga, wamemuahidi Waziri huyo, kwamba maelekezo ambayo ameyatoa watayazingatia na kutoa huduma bora ya matibabu na kuwajali Wajawazito.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa akizungumza na Watumishi mkoani Shinyanga.
Naye Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dk. Willison Mhela kwenye kikao hicho cha Watumishi mkoani Shinyanga kabla ya kukabidhi Magari.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akisoma taarifa ya Mkoa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (kushoto)akimkabidhi Taarifa ya Mkoa Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (kushoto)akiteta Jambo na Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa.
Viongozi wakiwa Meza Kuu.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa akikata utepe kukabidhi Magari Manne ya usimamizi Sekta ya Afya Shinyanga kwa ajili ya Waganga Wakuu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akionyesha ufunguo mara baada ya kukabidhiwa Magari Manne ya usimamizi kwa Waganga Wakuu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (kulia)akimshukuru Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa kwa kumkabidhi Magari hayo kwa niaba ya Rais Samia.
Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa akizungumza na Watumishi wa Sekta ya Afya mkoani Shinyanga.
Awali Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa (kushoto) akiwasili mkoani Shinyanga na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Christina Mndeme.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464