RC MNDEME AMEONGOZA KIKAO CHA RCC SHINYANGA,ATOA MAAGIZO MAZITO

RC MNDEME AMEONGOZA KIKAO CHA RCC, ATOA MAAGIZO MAZITO

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme,ameongoza Kikao cha Kamati cha Ushauri (RCC) mkoani humo nakutoa maagizo mbalimbali.

Kikao hicho cha RCC kimefanyika leo Decemba 15, 2023 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwamo Wabunge wa Mkoa wa Shinyanga wakiongozwa na Mwenyeji wao Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na watu wenye ulemavu.
Akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho, amewaagiza Wakuu wa wilaya,Wakurugenzi, Wenyeviti wa Halmashauri, Watendaji pamoja na Maofisa Elimu, kwamba shule zitakapo funguliwa Januari mwakani, wahakikishe wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wanaripoti shule.

“Nawapongeza wasimamizi wote wa elimu mkoani Shinyanga pamoja na Wadau wa elimu kwa kusimamia vizuri taaluma za wanafunzi na kuufanya Mkoa wetu wa Shinyanga kufaulisha wanafunzi wa Kidato cha Sita kwa asilimia 100,”amesema Mndeme.
Kwa upande wa Sekta ya Kilimo,amewaagiza Maofisa Ugani kuwatembelea Wakulima na kutoa elimu ya Kilimo cha Kisasa, pamoja na wanaosambaza Mbolea ya Ruzuku iwafikie Wakulima kwa wakati.

Aidha, amewataka pia viongozi mbalimbali pamoja na kuwaomba viongozi wa Madhehebu ya Kidini, kuhamasisha wananchi kupanda Miti katika Kaya zao, na kwenye Taasisi za Serikali na Binafsi ili kuifanya Shinyanga kuwa ya Kijani, na kwamba kwenye vikao vyao ajenga ya kupanda miti iwe ya kudumu.
Katika hatua nyingine Mndeme,
ameeleza kusikitishwa na kitendo cha Wakandarasi ambao wanatekeleza Mradi wa umeme wa REA mkoani humo kwa kusua kwao, na kuzitaka Mamlaka husika ziwachukulie hatua ikiwamo kuvunja mikataba yao,huku akiwataka Kashwasa kutoa huduma stahiki ya maji kwa wananchi.

Nao baadhi ya wajumbe wakichangia ajenda kwenye kikao hicho akiwamo Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga DK. Luzila John, wameomba huduma ya Maji ipatikane muda wote Hospitalini hapo, pamoja na Matengenezo ya Barabara kwa kiwango cha Lami ambayo inatoka Kata ya Ndala kwenda katika Hospitali hiyo.
Meneja wa TARURA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Oscar Mlekwa, akijibu hoja hiyo, amesema Barabara hiyo ipo kwenye mpango wa Matengenezo kwa kiwango cha Lami Kilomita 4.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, amesema yale yote yaliyojadiliwa kwenye kikao hicho cha RCC ni muhimu kwa maendeleo ya Mkoa wa Shinyanga kwa ujumla, na kuwaomba viongozi na watendaji wa Serikali, waendelee kuchapa kazi kwa ushirikiano. na kwamba Mkoa huo kwa upande wa kisiasa upo salama.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza kwenye kikao cha RCC.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu,akizungumza kwenye kiko cha RCC
Viongozi wakiwa kwenye kikao cha RCC.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC Mkoa wa Shinyanga.
Kikao cha RCC Mkoa wa Shinyanga kikiendelea.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464