NBS IMETOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI USAMBAZAJI NA UHAMASISHAJI WA MATUMIZI YA MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2022
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
OFISI ya Taifa ya Takwimu Tanzania (NBS)imetoa Mafunzo kwa Waandishi wa habari, kuhusu usambazaji na uhamasishaji wa matumizi ya matokeo ya Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2022.
Mafunzo hayo ambayo yatachukua muda wa siku mbili, yameanza kutolewa leo Decemba 18, 2023 mkoani Shinyanga, ambayo yameshirikisha Waandishi wa habari 120 kutoka Klabu za Waandishi wa Habari Mikoa ya Simiyu,Tabora,Geita na wenyeji Shinyanga.
Akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni Rasmi kufungua Mafunzo hayo Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi 2022 Anne Makinda, amesema Waandishi wa habari ni muhimu sana kupata uelewa juu ya usambazaji na matumizi ya matokeo ya Sensa ya watu na makazi hasa wanapokuwa katika majukumu yao ya kuhabarisha umma.
“Waandishi wa habari tulianza kushirikiana na nyie tangu mwanzo kwa kutoa elimu kwa wananchi kushiriki kuhesabiwa Sensa ya watu na Makazi, na hadi siku yenyewe ya tukio, na awamu hii ni mrejesho wa Sensa kwa wananchi ndiyo maana tumewapatia mafunzo sababu nyie mpo karibu na wananchi muda wote,”amesema Makinda.
Aidha, amewasihi Waandishi wa habari kwamba kwenye mafunzo hayo ya siku mbili, wayachukuliwe kwa umuhimu’Serious’ ili wapate uelewa mpana katika Uandishi wao wa Takwimu kwa Maendeleo endelevu ya Taifa.
Naye Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amesema Sekta ya habari ina mchango mkubwa wa Maendeleo ya nchi, sababu ni daraja kati ya Serikali na wananchi.
“Sensa ya watu na makazi ni mfano mkubwa kwa kazi ambayo imefanywa na vyombo vya habari katika, kuhamasisha wananchi kushiriki kuhesabiwa na elimu hiyo iliwafikia watu wote hadi ngazi za chini,”amesema Mndeme.
“Mafunzo haya yatumieni vizuri ili kupata uelewa na kwenda kuhabarisha Umma na kuwapatia matokeo ya Sensa kwa weledi kupitia Taaluma yenu ya habari,”ameongeza Mndeme.
Aidha, ameviomba vyombo vya habari kuanzisha Mijadala kuhusu matokeo ya Sensa ya watu na makazi, na kushirikisha Jamii, Wataalum mbalimbali ili kudadavua matokeo ya Sensa na Matumizi yake.
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga Greyson Kakuru, akizungumza kwenye mafunzo hayo, amesema niya muhimu kwa Waandishi wa habari katika Uandishi wao wa habari wa kuhabarisha Umma na kuandika Takwimu kwa Usahihi.
Amesema Sensa ya watu na Makazi ni muhimu katika Taifa, na kutolea mafano Maafa yaliyotokea Hanang’ mkoani Manyara kwamba Takwimu za Sensa za mwaka 2022 zilitumika kutambua watu na Makazi yao na kufanya uokozi na waandishi wa habari walitumia vyema taaluma yao kuhabarisha na kutoa takwimu sahihi.
Aidha, zoezi la uhesabuji Sensa ya watu na Makazi lilifanyika Agosti 23 mwaka 2022 ikiwa ni Sensa ya Sita ambayo ni muhimu katika utungaji Sera na kupanga mipango ya maendeleo kwa wananchi kwa uwiano sawa sababu ya kuwa na idadi yao kamili.
Sensa ya mwaka 2022 imetaja Idadi ya Watanzania kwa sasa tupo Milioni 61,741,120.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi 2022 Anne Makinda akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Meneja wa Takwimu Mkoa wa Shinyanga Elius Kamendu akizungumza kwenye Mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa NBS Taifa.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru akizungumza kwenye Mafunzo hayo.
Viongozi wakiwa meza kuu kwenye mafunzo hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (kulia) akiwa na Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi 2022 Anne Makinda wakiteta Jambo kwenye Mafunzo hayo.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye Mafunzo.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye Mafunzo.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye Mafunzo.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye Mafunzo.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye Mafunzo.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye Mafunzo.
Mafunzo yakiendelea.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye Mafunzo.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye Mafunzo.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye Mafunzo.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye Mafunzo.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye Mafunzo.
Picha ya Pamoja ikipigwa kwa viongozi wa Klabu za Waandishi wa Habari kutoka Mikao ya Shinyanga,Simiyu,Geita na Tabora.