MAFUNZO YA NBS KWA WAANDISHI WA HABARI YALIYOHUSU USAMBAZAJI NA UHAMASISHAJI MATUMIZI YA MATOKEO YA SENSA 2022 YAMEHITIMISHWA
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imehitimisha Rasmi Mafunzo ya Siku mbili kwa Waandishi wa Habari kutoka Mikoa Nne, yaliyohusu kuwapatia uelewa Waandishi hao kuhusu Usambazaji na Uhamasishaji wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022.
Mafunzo hayo yalishirikisha Waandishi wa Habari 120 kutoka Mikoa Minne ambayo ni Geita, Simiyu, Tabora na wenyeji Shinyanga, ambayo yamechukua muda wa Siku mbili yalianza Jana na kuhitimishwa leo Decemba 19, 2023.
Akihitimisha Mafunzo hayo Mtaalamu wa Habari na Mawasiliano kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) Said Ameir ambaye pia alikuwa mwezeshaji, amewataka Waandishi wa habari wakatumie Kalamu zao vyema katika usambazaji na uhamasishaji wa matumizi ya matokeo ya Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2022.
“Vyombo vya habari ni muhimu katika kusambaza Matokeo ya Sensa na matumizi yake,na mnapoandaa machapisho yenu au kutangaza mfanye kazi zenu kwa usahihi, sababu Jamii ina viamini sana vyombo vya habari,”amesema Ameir.
Aidha, Jana Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi mwaka 2022 Anne Makinda, akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni Rasmi kufungua Mafunzo hayo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amesema Waandishi wa habari ni muhimu sana kupata uelewa juu ya usambazaji na uhamasishaji matumizi ya matokeo ya Sensa ya watu na makazi hasa wanapokuwa katika majukumu yao ya kuhabarisha umma.
“Waandishi wa habari tulianza kushirikiana na nyie tangu mwanzo kwa kutoa elimu kwa wananchi kushiriki kuhesabiwa Sensa ya watu na Makazi, na hadi siku yenyewe ya tukio, na awamu hii ni mrejesho wa Sensa kwa wananchi ndiyo maana tumewapatia mafunzo sababu nyie mpo karibu na wananchi muda wote,”amesema Makinda.
Naye Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo,amesema Sekta ya habari ina mchango mkubwa wa Maendeleo ya nchi, sababu ni daraja kati ya Serikali na wananchi.
“Mafunzo haya yatumieni vizuri ili kupata uelewa na kwenda kuhabarisha Umma na kuwapatia matokeo ya Sensa kwa weledi kupitia Taaluma yenu ya habari,”amesema Mndeme.
Aidha, ameviomba vyombo vya habari kuanzisha pia Mijadala kuhusu matokeo ya Sensa, na kushirikisha Jamii, Wataalamu mbalimbali ili kudadavua matokeo ya Sensa na Matumizi yake.
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga Greyson Kakuru, akizungumza kwenye mafunzo hayo, amesema niya muhimu kwa Waandishi wa habari katika Uandishi wao wa habari wa kuhabarisha Umma na kuandika Takwimu kwa usahihi.
Amesema Sensa ya watu na Makazi ni muhimu katika Taifa, na kutolea mfano Maafa yaliyotokea Hanang’ mkoani Manyara kwamba Takwimu za Sensa za mwaka 2022 zilitumika kutambua watu na Makazi yao na kufanya uokozi, na waandishi wa habari walitumia vyema taaluma yao kuhabarisha na kutoa takwimu sahihi.
Aidha, zoezi la uhesabuji Sensa ya watu na Makazi lilifanyika Agosti 23 mwaka 2022 ikiwa ni Sensa ya Sita ambayo ni muhimu katika utungaji Sera na kupanga mipango ya maendeleo kwa wananchi kwa uwiano sawa sababu ya kuwa na idadi yao kamili.
Na Sensa hiyo imetaja Idadi ya watanzania kwa sasa tupo Milioni 61,741,120.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mtaalamu wa Habari na Mawasiliano kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) Said Ameir, akiwasilisha Mada kwenye Mafunzo hayo kabla ya kuyahitimisha.
Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu Cha Morogoro Abubakari Rajab akiwasilisha Mada kwenye Mafunzo hayo.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.