KATAMBI AFANYA MKUTANO MKUBWA SHINYANGA,APONGEZWA KILA KONA KUCHOCHEA MAENDELEO

KATAMBI AFANYA MKUTANO MKUBWA SHINYANGA, APONGEZWA KILA KONA KUCHOCHEA MAENDELEO

-Madiwani wafunguka Jimbo la Shinyanga Mjini halijawahi kupata Mbunge kama Katambi ‘Mitano tena’

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, amefanya Mkutano Mkubwa Mjini Shinyanga, kwa kukutana na baadhi ya Wajasiriamali,Viongozi mbalimbali, Wafanyakazi, Watu wenye ulemavu pamoja na Wazee, na kupatiwa elimu mbalimbali kwa mustakabali wa maisha yao, pamoja na kuwatakia heli ya Sikukuu ya Christimas na Mwaka mpya 2024.

Mkutano huo umefanyika leo decemba 21, 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga, ambapo ilitolewa elimu mbalimbali za kijasiriamali, usalama mahali pa kazi, walemavu, pamoja na dhana ya hifadhi ya jamii kwa kujiwekea mafao ya uzeeni.
Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu, akizungumza kwenye Mkutano huo, amesema wao kama viongozi lazima wawe na machungu ya kuwatumika wananchi, na ndiyo maana amefanya Mkutano huo na kutolewa elimu mbalimbali, ikiwamo ya ujasiriamali ili wananchi wapate kuwa na uchumi mzuri licha ya kuwaletea maendeleo.

Amesema ndani ya uongozi wake Jimbo la Shinyanga Mjini ameleta maendeleo makubwa katika Sekta mbalimbali, huku akimpongeza pia Rais Samia kwa kutoa fedha za kutekelezwa miradi mingi, na kuwaomba wanashinyanga waendelee kuwaunga mkono viongozi, ili wapate kuwaletea maendeleo pamoja na kuwapatia elimu ya fursa mbalimbali zikiwamo za ujasiriamali.
Aidha, amewataka Wananchi wa Shinyanga katika chaguzi zijazo ukiwamo uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani na Uchaguzi Mkuu 2025, kwamba wachague viongozi makini wachapakazi na wenye kuwaletea maendeleo, na siyo kuuza maendeleo kwa kupewa pesa na kumchagua kiongozi asiye stahili sababu ya Rushwa.

“Kura yako ndiyo maendeleo yako, tuache kuuza maendeleo kwa pesa,”amesema Katambi.
Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi, akizungumza kwenye Mkutano huo, amewasisitiza wananchi kwamba katika chaguzi zijazo wasije wakachanganya gunzi na betrii kwenye tochi sababu haitawaka, bali wachague viongozi wote wanaotokana na CCM, ili wapate kuwatumikia vizuri na kuwaletea maendeleo sababu watakuwa na muunganiko mzuri..

“Uchaguzi 2024-2025 tunataka Mafiga Matatu ndiyo Chachu ya Maendeleo, msije kuchanganya gunzi na betrii kwenye tochi haitawaka,”amesema Samizi.
Pia ameipongeza Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan na timu yake yote akiwamo Katambi, kutokana na maendeleo makubwa ambayo wameyafanya, huku akihidi kuwa wataendelea kuisimamia miradi ya maendeleo pamoja na kutoa huduma stahiki kwa wananchi.

Samizi amewataka pia Wajasiriamali kwamba mikopo ya Serikali ambayo haina riba kupitia asilimia 10 za Halmashauri, kuwa itakapoanza kutolewa mwakani waichangamkie ili kupata mitaji na kujikwamua kiuchumi, sababu elimu tayari wameshapatiwa namna ya kufanya biashara.
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Zamda Shabani, amempongeza Katambi kwa kuandaa Mkutano huo pamoja na kutolewa elimu mbalimbali ikiwamo ya ujasiriamali, ambayo itainua uchumi wa wananchi wa Shinyanga, huku akimpongeza kwa hatua kubwa ya kuliletea maendeleo Jimbo la Shinyanga Mjini.

Diwani wa Mwawaza Juma Nkwambi, akizungumza kwenye Mkutano huo, amesema Jimbo la Shinyanga Mjini halijawahi kupata Mbunge kama Katambi, ambaye amekuwa mstari wa mbele kuleta maendeleo na kila Mwananchi anajionea mwenyewe, huku akiwasihi Wanashinyanga wasije wakajiribu kupoteza tena bahati ya kuwa na Mbunge kama huyo ambaye yupo kwa ajili ya maslahi yao.
“Kuna vitu vinaendelea lakini havina Afya, Mnyonge Mnyongeni lakini haki yake mpeni, Jimbo la Shinyanga Mjini halijawahi kuwa na Mbunge kama Katambi anachapakazi na Maendeleo Mnayaona akishirikiana vyema na Rais Samia, kijana huyu tumtunze tusimpoteze kapigwa Vita sana lakini Rais wetu amemuamini sababu ni mchapakazi, tunakata siku moja Waziri Mkuu aje atoke Shinyanga,”amesema Nkwabi.

Nao baadhi ya washiriki wa Mkutano huo wamempongeza Katambi kwa kuendelea kuwajali wananchi wake, na kumuomba aendelee hivyo hivyo katika kuwatumikia na kuwaletea maendeleo kwa kushirikiana na Rais Samia.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, vijana, Ajira na watu wenye ulemavu akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi (kushoto) akimpongeza Katambi kwa utendaji wake kazi na kuwatumikia wananchi katika kuwaletea Maendeleo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo, akizungumza kwenye Mkutano huo.
Katibu Siasa na Uenezi CCM Mkoa wa Shinyanga Richard Masele akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Anold Makombe akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mbunge wa Vitimaalumu Mkoa wa Shinyanga Christina Mzava akizungumza kwenye Mkutano huo.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza kwenye Mkutano huo.
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Zamda Shabani akizungumza kwenye Mkutanio huo.
Diwani wa Vitimaalum Shela Mshandete akizungumza kwenye Mkutano huo.
Diwani wa Mwawaza Juma Nkwabi akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mkurugenzi kutoka Shirika la Child Support Tanzania akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mackdonald Maganga kutoka NSSF akizungumza kwenye Mkutano huo.
Wawezeshaji wakiwa kwenye Mkutano huo.
Mbunge Katambi (kulia) akiwa na Mbunge wa Vitimaalum mkoani Shinyanga Christina Mzava wakiteta Jambo kwenye Mkutano huo.
Viongozi wakiwa kwenye Mkutano huo.
Washiriki wakiwa kwenye Mkutano
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Picha za Pamoja zikipigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464