KANISA LA WASABATO MTAA WA SHINYANGA MJINI WAMEMUAGA MCHUNGAJI LAZARO MBOGO


WAAMINI WAADIVENTISTA WASABATO SHINYANGA MJINI WAMUAGA MCHUNGAJI WAO LAZARO MBOGO BAADA YA KUHAMISHWA UTUMISHI


Na Mapuli Misalaba, Shinyanga.

WAUMINI wa Kanisa la Waadiventista Wasabato Shinyanga mjini Jumamosi Disemba 9,2023 wamemuaga mchungaji wao Lazaro Mbogo baada ya kuhamishwa utumishi wake kwenda mtaa wa Katungulu Sengerema Mkoani Mwanza.

Sabato maalum ya kumuaga Mchungaji huyo imefanyika katika eneo la kanisa la Waadiventista Wasabato Shinyanga mjini na kwamba, Mchungaji Mbogo amefanya utumishi wake kwa muda wa takribani Miaka mitatu akiwa anatoa mafundisho na huduma mbalimbali za kiroho kwa upendo na furaha bila kuchoka.

Wakimuelezea mchungaji Mbogo waamini Waadventista wasabato wamesema kuwa alikuwa mlezi mzuri ambaye alikuwa mstari wa mbele katika kuchochea maendeleo na kuwaimarisha kiimani.

Wamesema wataendelea kumuenzi na kuyaishi yale mema na mazuri aliyokuwa akiyafundisha kwao,na hivyo kumtakia matashi mema na utumishi uliotukuka kule aendako kadri ya mapenzi ya mwenyezi Mungu.

Kwa upande wake mchungaji Lazaro Mbogo ametumia nafasi hiyo kuwashukuru waamini waadventista wasabato wa kanisa hilo, kwa ushirikiano wao na maombezi katika utumishi wake kwa kipindi chote ambacho amekuwepo pamoja nao.

Hata hivyo mchungaji Mbogo amewaasa kuendelea kutoa ushirikiano kwa mrithi wake atakayekuja kuchukua nafasi yake, na kuwashukuru kwa zawadi walizompatia kwani ni sehemu ya upendo mkubwa waliouonyesha kwake.

Waamini waadventina wasabato Jumamosi Disemba 09 mwaka 2023 wamemshukuru mungu kwa ajili ya zawadi ya mchungaji lazaro mbogo katika kuwalea, kuwaongoza na kuwafundisha misingi ya imani, ambapo wamemzawadia vitu mbalimbali ikiwemo nguo,chakula na fedha.





Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464